ELI-91
JF-Expert Member
- Aug 24, 2014
- 3,583
- 9,666
Jarida la Financial Times (FT) linaripoti kuwa baada ya uchunguzi wa muda mrefu limegundua kuwa nchi ya Rwanda imekuwa ikichakachua takwimu zake za umasikini nchini humo, ikumbukwe kuwa France24 ilisharipoti mwaka 2015 kuwa serikali ya Kagame inachakachua takwimu zake za uchumi.
Uchakachuaji mkubwa zaidi ulifanyika mwaka 2015 punde kabla ya kura ya maoni iliyomwongezea Kagame (ambaye alishakuwa madarakani kwa miaka 15) muda wa kukaa madarakani kwa miaka mingine karibu ishirini! katika mazingiza hayo Kagame alikataa katakata kukubali takwimu zilizo onesha kuwa umasikini unaongezeka nchini Rwanda.
FT pia lilichapisha kwa mara ya kwanza barua ya ndani ambayo wafanyakazi watano wa benki ya dunia waliwaandikia viongozi wa taasisi hiyo mwaka 2015, katika barua hiyo wafanyakazi hao walilalamikia kile walicho kiita "uchakachuaji wa takwimu na kushindwa kwa Rwanda kutoa data za uhakika kwa uwazi", pia waliendelea kuandika kuwa "kile kilichokua kinaendelea kilikua na hatari ya kuichafua heshima ya benki ya dunia ikiwa nchi ya Rwanda itaendelea na mchezo wake".
=====
Tuhuma hizi ziliwahi kuripotiwa na Shirika la Habari la Fance24
My take: naona kila siku mambo yanazidi kujijidhihirisha kuwa ni wapi mheshimiwa wetu anachota 'idea' zake za ajabuajabu na zisizo za kitanzania.