Rwanda yasema itafungua mpaka wake na Uganda pale itakapojisikia kufanya hivyo na wala sio kwa kushurutishwa na watu wala nchi yoyote

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Rais wa Rwanda Paul Kagame, alisema Jumatano kwamba serikali yake itafungua mpaka na Uganda wakati itajihisi kufanya hivyo akisisitiza kwamba hakuna mtu wala nchi yoyote itamshurutisha kufanya hivyo.

Akihutubia mabalozi katika mkutano wa kila mwaka na waakilishi wa nchi za nje pamoja na mashirika ya kimataifa katika ikulu ya raia mjini Kigali, Kagame alizungumzia swala la Uganda na Rwanda, akigusia kwamba maafisa wake wanajitayarisha kwa mkutano wa Angola kuzungumzia uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Hata hivyo, rais huyo alisisitiza kwamba hakuna litakalobadilika iwapo matakwa ya Rwanda hayatazingatiwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya rais mjini Kigali, iliyowekwa kwenye ukurasa wa twitter wa serikali ya Rwanda, rais Kagame amesema mgogoro wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, ni jirani wake Uganda akielezea kwamba tatizo lililopo ni kubwa kuliko kufungwa kwa mpaka kama inavyoripotiwa.

“Hata iwapo tunafungua mpaka wa Rwanda na Uganda, swala kuu ni kukamatwa na kuzuiliwa kwa raia wetu nchini Uganda”, amesema rais Kagame.

Mwezi Desemba mwaka uliopita 2019, Uganda iliachilia huru raia kadhaa wa Rwanda, waliokuwa wanazuiliwa kwa maadai ya kuifanyia Rwanda ujasusi.

“Swala hili sio la kufunga wala kufungua mpaka. Ni swala la raia wetu kukamatwa wakiwa Uganda. Tumefunga mpaka kwa sababu hatutaki raia wetu kuingia Uganda kwa sababu watakamatwa. Lakini raia wa Uganda wapo huru kuingia Rwanda”, aliendelea kusema rais Kagame.

Uganda imekuwa ikikanusha madai ya kuakamata raia wa Rwanda wanaotii sheria, ikisisitiza kwamba wanaokamatwa wanashukiwa kufanya uhalifu.

Kagame alitaja hatua ya Uganda ya kuachilia huru raia wa Rwanda kuwa nzuri lakini akawa mwepesi wa kuongezea kwamba haitoshi na kwamba ni idadi ndogo sana ya raia wa Rwanda waliachiliwa huru, akidai kwamba raia wawili wa Rwanda walikufa wakiwa kizuizini Uganda kutokana na mateso.

Kagame pia alisema kuongoza jumuiya ya Afrika mashariki ni kazi ngumu sana kuliko kuongoza umoja wa Afrika – AU.

“Na wakati haya yote yanaendelea, tunazungumza sana kuhusu ushirikiano katika jumuiya ya Afrika mashariki. Tutaendelea tu kuzungumza kuhusu ushirikiano huo bila mafanikio kama tunayofanya ni tofauti na tunayosema. Tunastahili kufanya yaliyo sawa”, aliendelea kusema Kagame.

Rwanda inaishutumu Uganda kwa kuunga mkono makundi ya wapiganaji yenye lengo la kupindua serikali ya Kagame, kuwakamata raia wa Rwanda, na kuhujumu uchumi wake.

Rwanda imeweka marufuku ya biashara na kufunga mpaka wake na Uganda tangu Februari mwaka uliopita 2019 na kuwaonya raia wake kutoingia Uganda.

Uganda nayo inaishutumu Rwanda kwa kuiwekea marufuku ya kibiashara, kufanya upelelezi dhidi ya serikali ya rais Yoweri Museveni kwa lengo la kutatiza usalama wake, kuwafuta kazi maafisa wa ngazi ya juu raia wa Uganda waliokuwa wakifanya kazi Rwanda na kueneza habari za chuki dhidi ya Uganda na maafisa wake serikalini.

Rwanda imekuwa na uhusiano mbaya na majirani wake Burundi na Uganda, huku Burundi ikiishutumu kwa kuyapatia silaha makundi yanayopinga utawala wa rais Piere Nkurunziza na kupanga njama za kuangusha utawala wake katika mapinduzi yaliyofeli ya mwaka 2015.

Uganda imekataa kuzungumzia mgogoro wake na Rwanda katika vyombo vya habari.

VOA
 
Kufungwa kwa mpaka huo ni hasara sana kwa Uganda kuliko kwa Rwanda(sababu Rwanda haina bidhaa nyingi za kupeleka Uganda).

Uganda ilikua inapata $200mil kwa mwaka kwa ku-trade na Rwanda na baada ya kufungwa kwa mpaka kumefanya sasa Uganda inapata only $12.4mil kwa mwaka.

Na pia Uganda mpk sasa hawezi kulifikia soko lake kubwa kabisa la bidhaa zake huko kongo mashariki maana lazima apitie kwny huo mpk uliofungwa na Rwanda.

Kenya nao pia wanaisoma No. Maana maana mizigo inayotoka Mombasa kupitia Uganda kwenda Rwanda nayo inaisoma no. Vzr sana.

Bongo wafanyabiashara sasa hivi wanapeleka bidhaa huko Rwanda balaa ku-cover hilo gap la Uganda na Rwanda kwa sasa zaidi ya 90% ya mizigo yake yote inapitia bandari ya dar,so bongo imepiga bao vzr kwny mgogoro huo.

dodge
 
Bas huo mgogoro ni mzuri sana usiishe hayo ni kwa mawazo yangu

Kheri yao wapatanishi wa Aman
Asema Bwana wa Majeshi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa mkuu,na Magu wala hana muda wa kuwasuluhisha hahah,yeye anafurahi bandari yake kupiga hela,kuwauzia misosi kwa wingi na pia Tz kuendelea kua strategic country(influence yake kuongezeka).
Bas huo mgogoro ni mzuri sana usiishe hayo ni kwa mawazo yangu

Kheri yao wapatanishi wa Aman
Asema Bwana wa Majeshi

Sent using Jamii Forums mobile app

dodge
 
Kufungwa kwa mpaka huo ni hasara sana kwa Uganda kuliko kwa Rwanda(sababu Rwanda haina bidhaa nyingi za kupeleka Uganda).

Uganda ilikua inapata $200mil kwa mwaka kwa ku-trade na Rwanda na baada ya kufungwa kwa mpaka kumefanya sasa Uganda inapata only $12.4mil kwa mwaka.

Na pia Uganda mpk sasa hawezi kulifikia soko lake kubwa kabisa la bidhaa zake huko kongo mashariki maana lazima apitie kwny huo mpk uliofungwa na Rwanda.

Kenya nao pia wanaisoma No. Maana maana mizigo inayotoka Mombasa kupitia Uganda kwenda Rwanda nayo inaisoma no. Vzr sana.

Bongo wafanyabiashara sasa hivi wanapeleka bidhaa huko Rwanda balaa ku-cover hilo gap la Uganda na Rwanda kwa sasa zaidi ya 90% ya mizigo yake yote inapitia bandari ya dar,so bongo imepiga bao vzr kwny mgogoro huo.

dodge
pointi nzuri na mchambuzi mzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fursa hii Tanzania mbona hatuichangamkii mpaka malori mengi yamekwama Holili

Jan 2020
HATARI! Magari Ya Kwama Mpakani Mwa Kenya na Tanzania Siku 7

Madereva "TUNAKUFA NJAA" Magari ya mizigo 46 kutoka nchi za Rwanda na Burundi yamekwama kwa zaidi ya siku saba mpaka sasa Mpakani mwa Tanzania na Kenya (Holili) wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro kutokana na taarifa zao kutoonekana kwenye mfumo wa TRA Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Source: Global TV online
 
Kana siku 4 zimepita niliona hio taarifa tbc,hivi mpk leo inshu yao haijawa solved?

Back
Top Bottom