Rwanda yamfukuza Mhubiri wa Injili aliyewaita Wanawake ‘Ibilisi’

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Rwanda imesema Mhubiri na mmiliki wa kituo cha redio cha Amazing Grace, Gregg Schoof, raia wa Marekani aliyekamatwa mapema wiki hii jijini Kigali, amefukuzwa nchini humo.

Schoof amekuwa nchini Rwanda tangu mwaka 2003, kuhubiri lakini mwaka uliopita, kituo chake che redio kilifungwa baada ya kuhubiri kupitia redio yake kuwa, wanawake ni malaya na ibilisi.

Alikamatwa siku ya Jumatatu, akiwa na mwanaye wakati alipokuwa anataka kuwahotubia wanahabari jijini Kigali akilenga kuishtumu seirkali ya Rwanda.

Idara ya uhamiaji inasema, mtoto wake ambaye hakutajwa jina aliachiliwa huru lakini, baba yake amefukuzwa kwa sababu mbili, kwanza, kibali chake cha kufanya kazi kilikuwa kimeisha lakini pia hakuwa na sababu ya kuwa Rwanda kwa sababu kituo chake cha redio kilishafungwa.

Kanisa la Mhubiri huyo ni miongoni mwa Makanisa 700 yaliyofungwa mwezi Februari, baada ya kushindwa kutimiza masharti ya serikali kuhusu kufungua kanisa.
 
Halafu siku hizi baadhi ya wanaohubiri wanapotosha ukweli. Unakuta mhubiri anaamini na kutangaza kwamba wasomi wote wanampuuza Mungu kwa7bu wao wamesoma na wanaelewa na hawataiona mbingu. Sasa nikajiuliuza hivi huyu mhubiri anaona wivu? au ameamua kuniambia mim kisa yeye shule ilimshinda? na kwanini Mungu kasema asiefanya kazi na asile? inamaana kazi hizo zisiwe za kisomi???

Kiukweli siku hizi DINI imeingiliwa tofauti na Maandiko ya Mungu.

MUNGU ANASEMA👉 USIHUKUMU UKAHUKUMIWA. MWENYE KUHUKUMU NI YEYE.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom