Rwanda wameweza wanasonga mbele, 85% ya nyumba zote tayari hazina nyasi ndani ya mwaka mmoja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rwanda wameweza wanasonga mbele, 85% ya nyumba zote tayari hazina nyasi ndani ya mwaka mmoja

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BONGOLALA, Oct 31, 2011.

 1. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  Jirani zetu wa rwanda wameshajenga nyumba za kisasa kwa raia wake ndani ya mwaka 1 kwa asilimia 85.lengo ni kuondoa kabisa nyumba za nyasi ktk nchi yao.Huwezi amini hapo bagamoyo kuna shule ya msingi ina nyasi darasa moja na mwalimu mmoja tuu wanafunzi wapo 150 kuanzia la kwanza mpaka la saba.shule ya tangu mwaka 1979.hivi kweli watanzania tuna serikali au li dubwana?
   
 2. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,721
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  hii ni bongo lala kama ilivyo id yako hivyo isistaajabu mkuu. subiri kwanza tuwalipe dowans ndio tupange mambo mengine,shule na nyumba za raia si muhimu ndugu hapa tz.
   
 3. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Slaa akisema atajenga nyumba bora za bati magamba wanabeza, Rwanda wameweza pamoja na kuwa na bajeti ndogo sana kulinganisha na Tanzania
   
 4. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2011
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Hivi kweli mko sahihi kulinganisha maendeleo ya nchi yenye watu million 5 na nchi yenye watu million 45?, kweli? Rwanda ni kama mkoa wa Dar es salaam kwa ukubwa, japo watu walioko dar es salaam wanaweza kuwa wanazidi watu wa rwanda kwa wingi. kama mnataka kutenda haki katika hilo basi chagua mkoa mmoja ndani ya tanzania halafu linganisha na rwanda. mfano chukua mkoa wa kilimanjaro halafu linganisha na rwanda uniambie wapi pako juu kwa maisha bora. Rwanda sio saizi yetu bwana!, Linganisha tanzania na nchi nyingine zote ila sio Rwanda, Burundi, Swaziland na Lesotho.
   
 5. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,121
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Haya mambo yanawezekana sema ufisadi na uroho wa viongozi wetu ndo unaturudisha nyuma.
   
 6. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,990
  Likes Received: 2,649
  Trophy Points: 280
  I hate sisiemu hivi kukua kwa uchumi anaouzungumzia JK ni upi?wakati %80 wananchi wake wanaishi kwenye nyumba za nyasi na udongo?natamani kama huyu jamaa wa msoga angekuwa anaingia humu ili tumhoji,aaah napata hasira sana huyu jamaa anapotudanganya.
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  china,urusi na india wana eneo dogo? ukubwa wa nchi ni advantage kwetu kwani kila mahali kuna dhahabu,lakes,misitu,wanyama etc rwanda wanalima chai kahawa tuu!
   
 8. CHE GUEVARA-II

  CHE GUEVARA-II JF-Expert Member

  #8
  Nov 1, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 531
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Kwa kusema hivyo umeangalia pia vyanzo vya mapato?
  Utakuwa sahihi kama uta-assume: "If income is kept the same in both countries (Rwanda & Tz) while Rwanda has got a population of 5 million people and Tz with a pop. of 40 million people then people in Rwanda are relatively reacher (maisha yao ni bora) than Tz.

  Unaangalia population tu! Basi angalau ungejaribu kuangalia kulinganisha mikoa hiyo inayolingana na Rwanda kwa ukubwa na ulinganishe hiyo mikoa imefaidia vipi na rasilimali zilizomo, nd'o unge-judge kama ulivyo-judge!
   
 9. CHE GUEVARA-II

  CHE GUEVARA-II JF-Expert Member

  #9
  Nov 1, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 531
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Shinyanga kuna machimbo ya dhahabu (at least two gold mining sites - Bulyanhulu & Buzwagi) na Almasi. Ni matajiri kuliko Rwanda?
   
Loading...