Rwanda to use English in schools. What's wrong with Swahili or French? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rwanda to use English in schools. What's wrong with Swahili or French?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by JokaKuu, Oct 11, 2008.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Oct 11, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,762
  Likes Received: 4,977
  Trophy Points: 280
  ..Rwanda wamepitisha uamuzi kutumia Kiingereza toka shule za chekechea mpaka chuo kikuu.

  ..wanadai uamuzi huo ni maandalizi ya kuingia ktk soko la Afrika Mashariki.

  ..sasa nikajiuliza ni kwanini wasifundishe Kiswahili? labda wameona kuna hasara zake.

  ..kama wakifundisha Kiswahili watapata hasara/faida gani?


  ..vilevile, Tanzania tumefaidika vipi kielimu na kiutaalamu kwa ku-adopt Kiswahili kama medium of instruction ktk shule za msingi?
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Oct 11, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jokakuu,
  Rwanda hawawezi kujifunza kiswahili kwa sababu wao wana lugha moja pamoja na kwamba wana makabila tofauti..Kwa hiyo hawana haja ya kujifunza lugha mpya kwa sababu za mawasiliano kati yao.

  Kisha sidhani kama wamepitisha Kiingereza kuwa lugha ya kufundishia toka chekechea ikiwa asilimia 100 ya wanafunzi hao wahatumii kiingereza kama lugha yao!.. Watajifunza ama kuelewa vipi kinachofundishwa... haya ndio maajabu ya mtu mweusi.

  Ikiwa wamefanya hivyo siwezi kushangaa kwa sababu NDIVYO TULIVYO... Kiingereza kinatakiwa kufundishwa chekechea kama Lugha na sio kutumika kama medium..kisha watakapo fahamu kiingereza kama lugha ya mawasiliano ndipo unakuja na utaratibu wa kubadilisha lugha ya kufundishia masomo yote.
  Ni ulimbukeni ambao kama kawaida tunaiga -Ndivyo tulivyo!
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Oct 11, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,762
  Likes Received: 4,977
  Trophy Points: 280
  Mkandara,

  ..wameamua kutotumia Kifaransa kama medium of instruction. badala yake watatumia Kiingereza kuanzia chekechea.

  ..sasa kama suala ni azma yao ya kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki, kwanini wasifundishe kwa Kiswahili? kwa sababu wanapozungumzia Afrika Mashariki, nia yao ni kuunganika au kujichanganya na Tanzania.

  ..kutokana na kauli yako kwamba wana lugha yao ya Kinyarwanda. kwanini wasifute Kifaransa, na badala yake kutumia Kinyarwanda?

  ..mwisho, badala ya kutumia tu msemo "Waafrika ndivyo tulivyo," ni vizuri ukatueleza kwanini unafikiri uamuzi waliochukua hautakuja kuwa na manufaa kwao.

   
  Last edited: Oct 11, 2008
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,167
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu ni uamuzi mzuri katika dunia yetu ya sasa. Na hasa ukitilia maanani kutakuwa na ushindani mkubwa katika ajira ndani ya nchi za Afrika Mashariki (Tanzania, Uganda, Kenya na Rwanda) maana waajiri wa nchi zote hizo watakuwa na haki ya kuajiri popote pale katika nchi hizo. Hivyo wanajiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kutoa ushindani wa hali ya juu katika soko la ajira ndani ya Afrika Mashariki. Ni waajiri wachache sana watatafuta mtu ambaye yuko fluent kwenye kiswahili ukilinganisha na kiingereza.
   
 5. N

  Nsunza Member

  #5
  Oct 11, 2008
  Joined: Jan 21, 2008
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  It is not getting ready for East Africa guyz! In this world of globalization, you don't speak English you are out. Companies in the Western world are trying to find cheap soucers of labor for them to reduce cost and stay competitive the world market. Now most companies that i know they are outsourcing their business from customer service call centers to financial and accounting activities. The US companies are sending jobs to India and Phillipines and Hongkong. British companies on the other hand, are sending their jobs to former Russian states. If you look at the trend of Globalization it started in Mexico, moved to China,then India and guess who is next? Africa whoever is ready will benefit from it. Rwanda is positioning it self ready for that role. They don't have land, so they are focussing on services. Language is the key here and we need to know that it is not just English, French is also part of the program. We need education reform faster than we think. Our president is notorious in forming comissions and getting reports but when it comes to action well, we all know what happens. We need english from "vidudu". It is not just Rwanda that is doing that, China and Japan are doing the same!
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,167
  Trophy Points: 280
  Globalization inakufa taratibu maana kazi zimehamishwa kutoka nchi za magharibi na kupelekwa India, China, Urusi n.k. Hizo bidhaa zinazotengenezwa huko zinapelekwa katika soko la nchi za magharibi ambako Wananchi hawana kazi maana kazi zao zilihamishiwa India, China n.k. na hivyo hawana uwezo wa kununua bidhaa hizo.

  Pia nchi nyingi kama US, UK na nyinginezo Wananchi wameshashtuka hizi kazi zinazohamishiwa katika nchi hizo. Kama kampuni inahamisha kazi kwa mfano za call centers na kupeleka China au India wananchi wakigundua wanaanza kampeni ya kuyatenga makampuni hayo.

  Pia Rais atakayeingia sasa hivi US atakuja na incentives za hali ya juu ili kuhakikisha makampuni ambayo yamehamisha kazi toka US kwenda India au China yanazirudisha kazi hizo na wale ambao walikuwa wana mpango wa kuzihamisha hawafanyi hivyo.

  Pia wafanyakazi wa makampuni ya US au UK ambao inabidi wafanye kazi na na wafanyakazi wao waliokuwa India au China wameanza kulalamika kwamba inabidi wafanye kazi masaa mengi zaidi kutokana na tofauti ya masaa. Kwa hiyo hii globalization ya kuhamia kwenye nchi zenye cheap labour inaanza kufa taratibu.
   
 7. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2008
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Hasara tupu!!!

  Linganisha ukubwa wa lugha. Wangapi duniani wanazungumza Kiswahili. Wangapi wanazungumza English. Jibu ni hilo.

  Eti tunajilinganisha na wachina, angalia population ya china.

  Usiamini Usanii wa serikali hii ya wahuni. Angalia watoto wa katibu mkuu wa Wizara au kamishina yeyote pale Elimu wanasoma shule zipi.
   
 8. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Waafrika ndivyo mlivyo. Malawi, Zambia na nchi nyingine zilizotawaliwa na Mwingereza zinatumia English na bado nchi zinajinye@. Hivyo suala sio lugha.
   
 9. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #9
  Oct 12, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Maybe we should also ask what is wrong with using English? By the way, hata Zanzibar walishaamua kutumia English tangu darasa la 4!!
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kiingereza kinatambulika kama lugha rasmi ya Afrika Mashariki
   
 11. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2008
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Nadhani this is in line with kagame's plane to make Rwanda the silicon Valley of East Africa. Amewekea emphasis kubwa sana information technology hivi karibuni ametangaza kwamba serikali inamnunulia kila mtoto laptop (the 100 USD laptop). Kaeni mkiwabeza majirani zetu, watatuacha mbaliiii!
  I think despite mapungufu yake kama binadamu, kagame has proven himself to be a leader with some vision and some strategic thinking, siyo kula, lala faulu kama huyu Ze Comedy wetu!!!
   
 12. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  All right!
  What about the long term plans? Idadi ya wanaojua kiswahili ni wengi E.A. Ni kama vile kuwaambia wachina waweke kichina pembeni.


  South Africa wao wana lugha rasmi kadhaa, je, kwa utaratibu wao huo wamekumbana na matatizo yepi?
  Je, Tanzania tunajua tunachotaka ili tunufaike katika ushirika huu wa Africa Mashariki?
  .
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,167
  Trophy Points: 280
  Ni very rare katika nchi zetu za kiafrika kusikia asilimia kubwa ya Wananchi wa nchi wanamfagilia sana Rais wao. Nina marafiki zangu wanyarwanda wanasema wanyarwanda wanampenda sana Kagame maana anafanya mambo mbali mbali ambayo yana maslahi kwa nchi yake na wananchi wanaona tofauti kubwa katika maisha yao ya siku, in a positive way.

  Sasa kuna haja ya Kikwete akaongee na Kagame ili ajue siri ya mafanikio yake labda miaka miwili iliyobaki anaweza kurudisha credibility yake. Miaka michache tu iliyopita Wahutu na Watutsi waliuana kwa wingi sana lakini baada ya nchi yao kutengemaa wamepiga hatua kubwa sana katika kipindi kifupi wakati sisi bado tunamangamanga tu kwa kuwa na viongozi wasio na uwezo wa kuiongoza nchi.
   
 14. R

  Rubabi Senior Member

  #14
  Oct 13, 2008
  Joined: Nov 30, 2006
  Messages: 174
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndivyo tulivyo, wengi wanafikiri kujua kiingereza ndio usomi,China medium yao ni kichina Je mbona wanakuja juu?Wanyarwanda afadhari wangefanya kiswahili na Kinyarwanda kidogo kuwa lugha za kufundishia primary school na baadae kutumia kiingereza secondary school.

  Tanzania tunapoteza talent nyingi sana hasa kwa kuwa wanafunzi wa sekondari wanapata shida sana na wanafeli form 4 kwa sababu wanasoma masomo kwa kiingereza, Kiswahili ni lugha ya kibantu kwa hiyo ni rahisi makabila ya kitanzania kukielewa.

  Waafrika kweli ndivyo tulivyo.Kama alivyosema nyerere,Afrika ni uozo mtupu,mawazo tegemezi,uchumi tegemezi na hata lugha tegemezi afrika uozo mtupu!!We are so foolish!!
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Bak,
  Wallahi natamani tungekuwa na kiongozi caliber ya Kagame Tanzania.
  The guy is serious and he knows what leadership is all about.
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Oct 13, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,762
  Likes Received: 4,977
  Trophy Points: 280
  Rubabi,Zakumi,Mkandara,Jasusi,...

  ..je, Malawi,Zambia,Uganda,Kenya,....wanaofundisha Kiingereza toka primary wanapoteza wanafunzi wengi wanapofika form 4 kama inavyotokea Tanzania?
   
 17. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Suala sio kupoteza au kupata. Suala liwe je lugha ya mafunzo inawanya elimu iwe DEEP ROOTED katika jamii.

  Malawi, Zambia, Uganda, Kenya inasomesha watu kwa kiingereza hili watu hao wafanye kazi lakini sio wawe watu wenye kufikiri na kuweza kutumia elimu katika mazingira yao.

  Tanzania inasomesha kwa kiswahili na inachofanya watu wavunjike moyo na kutoshindwa kutofautisha maarifa na lugha.

  Kwa upande mwingine China, Korea zimeweza kufanya elimu iwe DEEP ROOTED katika jamii zao na suala la lugha linakuja kama chombo cha mawasiliano tu na sio maarifa yenyewe.

  Tamati.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jokakuu,
  Mkuu samahani sana sikupata kufikiria kupitia tena hapa kujibu swali lako...
  nakuomba unielewe vizuri napotokea...nakumbuka sana kuwa haya ni marudio ya mada iliyokwisha zungumzwa sana humu miaka iliyopita.
  Sintazungumzia kwa nini rwanda wasijifunze Kiswahili kwa sababu nitakuwa nachanganya kati ya Kiswahili kama Lugha ya mawasiliano na Kiswahili kama lugha ya kufundishia..Kumbuka tu tunachozungumzia hapa ni lugha ya kufundishia hivyo Kiswahili kama Kiingereza kitakuwa bado ni lugha ngeni kwao (Rwanda) na kuna hitilafu nyingi ktk kiswahili kama lugha ya kufundishia kuliko hata kiingereza.
  Mkuu naomba sana unielewe hivi, unapochukua lugha ya nje kama Kiingereza ambayo asilimia 100 ya wananchi na watoto wote nchini hawazungumzi kuwezi kabisa kuifanya lugha hiyo kuwa ndio lugha ya kufundishia watoto.. Kwa sababu mtoto utakapo mfundisha kuhesabu wakati hajui ONE ni kitu gani utazidi kumpoteza zaidi hivyo ni muhimu kwanza uwafundishe lugha yenyewe kabla ya kufundisha masomo kwa lugha ya kigeni. Akisha fahamu One ni sawa na Moja ama EMO then ndio unaanza kumpa vitu..hapa lugha kwanza.
  Ni sawa na kutazama sinema ya Kihindi na pengine kwa sababu sisi tumezoea kuona hizo sinema za Kihindi, Kichina na kiingereza na wajuzi wa kufuatilia vitendo inakuwa vigumu sana kufikiria nje ya hapo. Nimeyaona Bongo nilipokwenda watu wanashinda ktk TV wakisikiliza as if wanaelewa kitu kumbe wanafuata tu vitendo vinavyokwenda na ajabu wanaziweza kweli!

  Mkuu hata huku nje immigrants wanapofika tu kitu cha kwanza hufundishwa lugha iwe kiingereza ama lugha inayotumika nchini humo kisha ndio unaweza kuja mpango wa kwenda shule...Na hata vijana wetu wanapopata scholarship nje hujifunza kwanza lugha za huko kabla hawajaanza muhula wa masomo yaliyowapeleka...It's just logic mkuu...Kozi ya miaka mitatu huitwa miaka minne ama mitano kwa sabahbu ya kujifunza lugha..
  Ni vigumu sana kwa nchi kama Rwanda ambayo asilimia kubwa ya walimu wake toka chekechea hadi chuo kikuu wanazungumza Kifaransa kuliko kiingereza na pengine asilia 80 ya walimu hawajui kiingereza.. sasa nashindwa kuelewa nani atamfundisha mwenziwe.
  Jambo jingine ELIMU haipatikani kwa lugha isipokuwa mawasiliano. Kama vile ktk kijiwe hiki tunazunguza kiswahili lakini kuna elimu tosha kwa mtu ambaye hazungumzi kiingereza, lakini kam ataweza kuzungumza kiingereza anawezxa kabisa kutafsiri yaliyomo humu kwa kiingereza na akafahamika vizuri tu kwa huyo Muingereza ama mzungu anayetaka kufahamu..
  Kwa hiyo huwezi kunambia kwamba kufundisha kwa kiingereza kuna ubora fulani zaidi ya Kifaransa ikiwa majority ya Wanyarwanda wanazungumza Kifaransa!... hakika hizi zote ni lugha za kigeni isipokuwa kwa sababu sisi sote NDIVYO TULIVYO - hatuna imani na lugha zetu wenyewe kwa sababu tunaamini kabsia hazijitoshelezi, wakati tazama lugha kama ya Kifaransa maneno yao mengi yametokana na Kiingereza. na hakuna mtu humu anaweza kunambia graduate wa Uingereza ama marekani ni mbora kuliko yule wa Sweden kwa sababu tu huyu kafundishwa kwa kiingereza..
  Kitu muhimu kwa nchi kama Sweden hufundisha kiingereza kama lugha (mawasiliano) ili kumwezesha msomi kuwasiliana na watu wa nje iwe kwa kutumia elimu aliyoipata kwa Kiswidish..na wapo wanaozungumza zaidi ya lugha mbili ama tatu hizi zote hazihusianani na elimu yake kwani wapo Kabuntas wanaoweza kuzungumza lugha mbili ama tatu na hawajawahi kwenda shule.
  Mkuu mimi nimekwenda Tanzania hivi majuzi, kuna vijana wanazungumza vizuri sana kiingereza lakini kichwani ni zero!...Na wengi sana wamesoma kwa kiingereza lakini usiombe wakifumbua mdomo kuzungumza kiingereza...sababu kubwa hawakujifunza lugha hii kama ya mawasiliano ila masomo yenyewe yamekuwa ya kiingereza..
  Kuamini kwamba kiingereza ni muhimu ktk kufundishia Chekechea badala ya kiingereza kuchukuliwa kama lugha ni mwanzo wa kukubali kwamba sisi NDIVYO TULIVYO!..
  Nasema ndivyo tulivyo kwa sababu kwa miaka mingi sana Afrika imekuwa ikitoa wataalam wengi wakizungumza lugha za kigeni lakini wameshindwa kabisa kutafsiri elimu zao kwa kiswahili ili zipate kutumika ktk mazingira yetu badala yake ndio tumekuwa tukijaribu kubadilisha WATU na MAZINGIRA ili yapate kufanana na yale ya Ulaya..
  Jambo muhimu kuliko yote ni kwamba ELIMU tunayoitafuta ni kwa ajili ya ku serve nchi yako!.. sasa kuna manufaa gani unapopata elimu kwa kiingfereza lakini unashindwa kuitumia elimu hiyo kwa sababu asilimia 80 ya wananchi unaokutana nao kila siku hawafahamu unachokizungumza!...Elimu inatolewa ili upate kuhudumia wananchi ama nchi yako na sio kwa sababu tunafanya biashara na Ulaya...biashara na Ulaya kinachotumika ni lugha ya mawasilino, hivyo ni muhimu kwa msomi kujifunza kiingereza..

  Niarudia kusema hivi:- Kinachotangulia hapa ni kwenda kwa hatua za mabadiliko ambayo yatawawezesha watu na mazingira kubadilika kutokana na maendeleo yanayopatikana. Unapowawezesha wananchi kutumia vifaa vya kisasa katika kilimo cha kileo unakuwa umebadilisha fikra za watu hao ktk kilimo na mazingira yake kuwa yale yanayowezesha kilimo kilichokusudiwa.
  Unapojenga barabara nzuri unawawezesha wananchi mazingira kubadilika ktk matumizi ya barabara hizo lakini unapojaribu kuwabadilisha watu na mazingira ili yafanane na ya Ulaya hali huna nyenzo za kufanyia kazi ndio Ulimbukeni wenyewe..
  Kiingereza kama lugha ifundishwe toka Chekechea kwani kuna uwezekano mkubwa kwa mtoto kushika lugha mbili ama zaidi na hii itawasaidia sana watoto hao kama watafikia darasa la Tano ambapo unaweza kuchukua Kiingereza kama lugha ya kufundishia..
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  jokaKuu,
  Point nyingine ambayo naweza kuongezea ni kwamba serikali ya Kagame imechukua sera za makusudi kuachana na Franco-phone hasa baada ya mauaji ya 1994 na Ufaransa kuonekana ikiunga mkono serikali ya Kihutu. Rwanda itaelekeza nguvu zake zaidi katika mahusiano na English speaking countries kama vile Marekani na Uingereza badala ya Ufaransa. Utakuta Wanyarwanda wengi waliokuwa makimbizini walirejea nyumbani wakizungumza Kiswahili na Kiingereza kwa sababu wengi walikuwa Uganda Tanzania na Kenya. Na it goes without saying kuwa Mnyarwanda yeyote anayezungumza Kiingereza anaelewa pia Kiswahili kwa hiyo hapo hamna haja ya kuweka msisitizo katika lugha ya Kiswahili. Kiswahili kitaendelea kuwa lugha muhimu Rwanda licha ya sera za kuhimiza Kiingereza.
   
 20. K

  Koba JF-Expert Member

  #20
  Oct 13, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ..point hapo ni kuwafuta wafaransa katika Rwanda,wamevunja ubalozi na hawana nao uhusiano wowote kwa sasa,sasa ni kuondoa hiyo lugha maana france wameonekana ni poison kwa Rwanda kwa miaka mingi sana!
   
Loading...