RWANDA: Rais Paul Kagame afanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri ambapo Wizara 8 zimepata Waziri wapya

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais wa Rwanda Paul Kagame amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri na kumteua Dkt Richard Sezibera kuwa waziri mpya wa mashauri ya nchi za nje.

Jenerali James Kabarebe aliyekuwa mtu wa karibu sana na Rais Kagame amepoteza wadhifa wake kama waziri wa ulinzi na badala yake akateuliwa mshauri wa rais katika masuala ya usalama.

Katika mabadiliko makubwa na ya kushtukiza aliyofanya Rais Kagame wizara 8 kati ya 23 zimepata mawaziri wapya zikiwemo wizara nyeti tatu, wizara ya ulinzi ambayo sasa inaongozwa na Meja jenerali Albert Murasira aliyechukua nafasi ya Jenerali James Kabarebe.

Mwandishi wa BBC Yves Bucyana anasema si wengi walitarajia mabadiliko haya.

Jenerali Kabarebe ambaye amepewa nafasi ya kuwa mshauri maalumu wa rais wa maswala ya ulinzi na jeshi alikuwa mshirika wa karibu sana na Rais Paul Kagame tangu vita vilivyong'oa utawala wa rais Juvenali Habyarimana miaka ya 1990.

Mkuu wa majeshi Rwanda na Congo
Jenerali Kabarebe ndiye mtu aliyewahi kuwa mkuu wa majeshi ya nchi mbili Rwanda na Congo wakati wa utawala wa hayati Laurent Desire Kabila; kabla ya kuwa waziri wa ulinzi wa Rwanda kuanzia mwaka 2010.

Mwanajeshi huyo ni miongoni mwa maafisa saba wakuu wa Rais Kagame ambao walikuwa wamefunguliwa mashtaka na Ufaransa kuhusiana na kuuawa kwa aliyekuwa rais Juvenal Habyarimana, mauaji ambayo yanadaiwa kuanzisha mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo watu zaidi ya 800,000 waliuawa, wengi wao Watutsi walio wachache.

Hakuna sababu iliyotolewa ya kuondolewa kwa Kabarebe kutoka kwenye wizara ya ulinzi lakini kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, kuondoka kwake kunaonekana kama hatua kubwa katika kutaka kurejesha tena uhusiano mwema kati ya rwanda na Uganda.

Uhusiano wa Rwanda na jirani yake Uganda umekuwa ukidorora kwa miaka mingi, ambapo Rwanda imekuwa ikiituhumu Uganda kwa kuwakamata kiholela raia wake nchini humo na pia kwa kutoa hifadhi kwa waasi na wapinzani.

Chanzo: BBC Swahili
 
mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo watu zaidi ya 800,000 waliuawa, wengi wao Watutsi walio wachache.

Chanzo: BBC Swahili
Hii para imeharibu uzi mzima.....otherwise hayo mabadiliko hayana jipya maana bado anaendeleza kujiimarisha kwenye utawala. Mabadiliko ambayo tungeyaelewa ni pale atakapokubali kuachia ngazi na kuachia kizazi kipya na maono mapya kuongoza nchi ila hii tabia ya kuhodhi madaraka siku anaanguka ghafla huku hajaandaa watu kuchukua nafasi yake ndio inaacha nchi kwenye mapigano makali hasa ukizingatia tension za ukabila zilizopo Rwanda.

Anyway muda ndio utaamua ila lazima atavuna alichopanda
 
Aliuliwa na PK?
Hizo ndio habari nilizopo chini ya kapeti mkuu na ndio maana walikuwa wanambana kayihura asisafiri nje ya nchi maana mpango ulikuwa akazamie Rwanda kama mapandikizi wengine kama Ntaganda au Laurent nkunda mambo yalivyovurugika wakakimbilia Rwanda!!! Alafu nashangaa kuna watu bado wana imani hadi kumfanya kagame rafiki yao!! Museveni na nkuruzinza walishastuka ndio maana hawataki mazoea naye ya kijinga jinga tena otherwise leo hii nchi zao zisingekalika tena!!
 
Teh sasa mkuu mseveni si alishapewaga kichapo na Rwanda na hata sasa akizingua anaweza kuchezea tena,Nkurunzinza yeye ndo awe mpole aendelee kuikumbatia Tz tu la sivyo atatolewa mkuku asiamini.

By the way kipindi kile walikua wanasema waasi wanakaribia Kigali waliishia wapi mkuu?
 
Itakuwa wamevurugana baada ya mtandao wao UG chini ya Gen. kayihura kubumburuka.... Hiki kifo cha kirumira kitaondoka na wengi.

Cc Malcom Lumumba Wick

Embu unieleze vizuri hapa maana na mimi baba ni wa kule tena mtutsi nusu.

Hii para imeharibu uzi mzima.....otherwise hayo mabadiliko hayana jipya maana bado anaendeleza kujiimarisha kwenye utawala. Mabadiliko ambayo tungeyaelewa ni pale atakapokubali kuachia ngazi na kuachia kizazi kipya na maono mapya kuongoza nchi ila hii tabia ya kuhodhi madaraka siku anaanguka ghafla huku hajaandaa watu kuchukua nafasi yake ndio inaacha nchi kwenye mapigano makali hasa ukizingatia tension za ukabila zilizopo Rwanda.

Anyway muda ndio utaamua ila lazima atavuna alichopanda

Natamani kujua lakini embu fafanua
 
Embu unieleze vizuri hapa maana na mimi baba ni wa kule tena mtutsi nusu.
Mkuu ni kwamba Gen kale kayihura ni pandikizi wa kagame na alikwisha panga kumpindua museveni muda "muafaka" ukifika sasa kuna polisi kama kina kirumira na kaweesi wakshtuka ndio bifu likaanza kati yake na vibaraka wa kayihura hivyo ndio inasemekana akamalizwa na ''shooters'' wa kitutsi yeye pamoja na kaweesi.

Hivyo kayihura haya mashtaka mengine ya kisiasa tu ila kinachomfanya abanwe na museveni ni sababu amegundua alimsaliti kwa ku-ally na kagame
Natamani kujua lakini embu fafanua
Ndio hivyo kagame alipanga kumpindua Nkuruzinza ila TZ ndio ilimuokoa ndio maana waliretaliate kwa kuua watutsi walioside na kagame mfano yule waziri wa habari aliyeshiootiwa akiwa anarudi kwake.... hata museveni ameshtuka kuwa alitaka kupinduliwa toka 2001 hivyo uhusiano wao umevurugika kiasi tokea hapo

Kwa ufupi kagame ni kansa hapa Afrika mashariki ukitaka kufahamu hilo subiri uchaguzi wa Congo kama chama cha kabila kikishindwa nchi haitotawalika tena hadi pandikizi waliompanga ashinde!!

Kazi kwelikweli
 
zitto junior

Hawa watu watutsi kweli ni cancer nilikufuatilia kule kwenye ule uzi wa the bold nikagundua kitu. Asante sana mkuu maana JF ni darasa.

Lini Kagame atatolewa madarakani yaani nataka achinjwe kabisa maana anasura ya damu kabisa
 
Hii para imeharibu uzi mzima.....otherwise hayo mabadiliko hayana jipya maana bado anaendeleza kujiimarisha kwenye utawala. Mabadiliko ambayo tungeyaelewa ni pale atakapokubali kuachia ngazi na kuachia kizazi kipya na maono mapya kuongoza nchi ila hii tabia ya kuhodhi madaraka siku anaanguka ghafla huku hajaandaa watu kuchukua nafasi yake ndio inaacha nchi kwenye mapigano makali hasa ukizingatia tension za ukabila zilizopo Rwanda.

Anyway muda ndio utaamua ila lazima atavuna alichopanda
Nlidhani atamuandaa Kabarebe kama mrithi
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom