Rwanda nchi ya mwisho kwa rushwa ukanda wa Africa Mashariki Tanzania ya tatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rwanda nchi ya mwisho kwa rushwa ukanda wa Africa Mashariki Tanzania ya tatu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CPA, Oct 21, 2011.

 1. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 737
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Orodha iliyotolewa jana na shirika moja la utafiti juu ya rushwa . imeonyesha jeshi la polisi ndio kinara wa rushwa, Uganda ikiongoza, ikifuatiwa na Burundi huku Tanzania ikiwa ya tatu kwa rushwa katika ukanda wa Africa mashariki. Ripoti hiyo imeitaja Rwanda kuwa ni nchi iliyofanikiwa kwa kupambana na rushwa katika ukanda wa Africa mashariki, ikiwa ni nchi ya mwisho katika orodha ya vinara wa rushwa.
  MAONI YANGU: Kwanini Rwanda inapiga hatua sana kwa kira Nyanja, sisi tumeshindwa nini? Juzi katika ripoti ya world Bank imeonyesha Rwanda ni miongoni mwa nchi ambao uchumi wake unakuwa kwa kasi sana. WHY RWANDA AND NOT TANZANIA?
   
 2. the grate

  the grate JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania wenzangu hebu tuone wivu jinsi ambavyo wenze2 wanapga hatua na 2jitahd kufanya vitu vya maendeleo kwa kushirikiana kila mmoja kwa nafasi yake.GOD blec tz
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Wale Rwanda walizipiga kwanza ndo heshima ikawepo, inavyoonekana hawa viongozi hawana nguvu ya kuleta mapinduzi au hata kusimamia zile sheria tulizojiwekea wenyewe. Kilichobaki hapa ni wote kwa pamoja kusema hapana, tumechoka wapisheni wengine! Lakini hilo la kusema pamoja naona nalo ni ngumu kwani wananchi wengi tuna njaa, na tunapopata wali dagaa kama ule wa igunga tunaona inatosha.

  Sitaki tuende huko walikopitia rwanda ila inavyoonekana viongozi wetu ndo wanakotaka kwani hawataki kukubali kuwa mfumo wao uongozi hauwezi kututawala kizazi cha dot.com, we need realistic things! hatuhitaji mzungu kutujengea kila kitu, kutufundia wadogo zetu, kujenga barabara ambazo nazo niza kututia umasikini kila mwaka mwajenga barabara ileile, what is the logic behind?

  Viongozi wetu hawasoma alama za nyakati kama alivyoshindwa Gaddaf kuona nyuma ya pazia nini kingemtokea!! Watch out!
   
 4. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Nafikiri wamekosea,Tz ni ya kwanza.
   
 5. h

  hajoma Member

  #5
  Oct 21, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  [TABLE="class: MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD="width: 100%, bgcolor: transparent"] Rushwa yazitafuta nchini za EAC
  [/TD]
  [TD="width: 100%, bgcolor: transparent"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  [TABLE="class: MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"] Thursday, 20 October 2011 21:03

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Waziri mstaafu wa Awamu ya Kwanza, Ibrahim Kaduma, akizindua ripoti ya hali ya rushwa katika nchi za Afrika Mashariki, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Fordia, Buberwa Kaiza na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Uwazi kutoka Kenya, Samuel Kimeu. Picha na Michael Jamson
  Gedius Rwiza
  TAASISI ya kutetea shughuli za Maendeleo Nchini (Fordia), imezindua ripoti yake ya mwaka kuhusu hali ya rushwa katika Ukanda wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, inayoonyeshwa kwamba
  Burundi, ndiyo nchi inayoongoza kwa rushwa ikifuatiwa na Tanzania na Rwanda ni ya mwisho.

  Ripoti hiyo ya mwaka 2011, iliyotolewa jijini
  Dar es Salaam jana inayonyesha kuwa kiwango cha rushwa nchini Burundi, kimeongezeka hadi kufikia asilimia 37.9 ikilinganishwa na asilimia 36.7 mwaka jana.


  Kuhusu
  Tanzania, ripoti hiyo ilisema kiwango cha rushwa, kimeongezeka kutoka asilimia 28.6 mwaka jana hadi kufikia asilimia 31.6 ya mwaka huu.Kwa mujibu wa ripoti, Jeshi la Polisi nchini, ndilo lilaongozwa kwa vitendo vya maofisa wake kuomba na kupekea rushwa ikilinganishwa na taasisi nyingine.

  Hii si mara kwanza kwa jeshi
  hilo kutajwa kuwa ni kinara katika rushwa. TAasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) katika ripoti zake , imewahi kulitaja jeshi hilo kuwa maofisa wame wanaongoza kwa vitendo vya rushwa.


  Moja ya ripoti za Takukuru iliwahi kuibua mjadala baada ya baadhi ya vigogo wa Jeshi la Polisi kuipinga.Akizungumzia kiwango cha rushwa kwa
  Uganda, ripoti hiyo ilisema nayo imeongezeka hadi kufikia asilimia 33.9 kutoka 28.8 ya mwaka jana 2010.

  Hali kadhalika ripoti ilizungumzia rushwa nchini Kenya, ambako imeelezwa kuwa inaonekana kushuka hadi kufikia asilimia 28.8 ikilinganishwa na asilimia 31.9 mwaka jana.Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Rwanda inayotajwa kuwa na mafanikio makubwa kiuchumi na nyanja nyingine za maendeleo, ndiyo yenye kiwango cha chini cha rushwa.

  Nchi hiyo ambayo mwaka 1994 ilikumbwa na mauaji ya kimbari yaliyoivuruga kiuchumi na kijamii, imezidi kung’ara baada ya ripoti kuonyesha rushwa imepungua kutoka asilimia 6.6 ya mwaka 2010 hadi 5.1 mwaka huu.

  Polisi vinara nchi zote
  Akisoma ripoti hiyo, Mkurungenzi wa (Fordia), Buberwa Kaiza, alisema Jeshi la Polisi katika nchi zote zilizofanyiwa utafiti bado kiwango cha rushwa kinaonekana kuwa cha juu tofauti na taasisi zingine.

  Kaiza alisema kutokana na utafiti huo taasisi ambazo zimeonekana kuwa na kiwango kikubwa wahusika wakuu wanaotakiwa kubadili mifumo inayotumika ambayo ni ya zamani na kutumia mifumo ya sasa.

  Mzee Kaduma
  Kwa upande wake waziri mstaafu wa awamu ya kwanza, Ibrahim Kaduma aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa ripoti hiyo, alisema watu wanaokula rushwa wanalitia aibu taifa na kwamba Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alikemea vitendo hivyo mwaka 1962.

  Takukuru

  Naye Mdhibiti na Mtafiti katika Takukuru, Yohana Madadi alisema taasisi hiyo imekuwa ikifanya jitihada za kupambana na vitendo hivyo mara kwa mara lakini bado jitihada za zaidi zinahitajika.

  Alisema vitendo hivyo vinaweza kupungua kama sio kuisha kabisa endapo wananchi na taasisi husika watashirikiana na kujua athari za kutoa na kupokea rushwa kuliko kuiachia Takukuru, peke yake kupambana na vitendo hivyo.


  Source :Mwananchi

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

   
 6. h

  hajoma Member

  #6
  Oct 21, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Inaonekana polisi wanaongoza katika kila nchi ya Afrika Mashariki. Hawa ndio tutategemea watende haki katika shughuli zao sijui tunaelekea wapi!
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Rwanda Unamjua Rais Wao; Hana Mchezo kama unapokea au unatoa rushwa unapotea.... get shot au kunyongwa - hana mchezo Kagame, ana damu za watu mikononi mwake kila mtu lazima amuogope

  Bongo sisi ni salama Unaiba unaitwa Ndugu wacha ulanguzi na wizi utakwenda jela
   
 8. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mimi hata sishangai. angalia wengi wa hao maaskari, elimu yao ni duni, kimaadili ni sifuri sasa jumlisha na mishahara yao jibu utaliona lilivyowazi.
  kuliboresha ni kufanya kinyume chake. 1. waajiriwe watu wenye elimu zao, 2. wawe na maadili mazuri, 3. waboreshewe mishara yao, 4. au angalao hata mawli kati ya hayo matatu
   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hapa kwe2 ni mpaka chama cha magamba king'oke hapo kileleni tofauti na hapo itakuwa hadithi. Tuipe nchi chama yenye uzalendo na wa2 wake,,,,,,,sisiem ni janga la Taifa letu lenye kitu cha asili lakini maganda wameamua kuburudisha nayo mioyo yao. Lakini hakika tumtaje MUNGU akawageuze hawa magamba mioyo wanayoifanya kuwa migumu na yaliyojiri na yanayojiri mpk hivi sasa yasitoke wajamen. UONGOZI WOTE WA JUU WA SERIKALI HUSIKA IACHIE NGAZI KABLA YA NGUVU YA UMMA HAWAJACHAFUKWA NA MIOYO na wanaona haitatokea lakini Mi naona hali ikiendelea kihivi nawaambia hapa hapatatosha kwa hawa mapapa na sekta zao zote na ya kwa Marehemu Garddafi ni cha mtoto,wanaendeleza wizi tu.
   
 10. m

  mwana wa africa JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 490
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  tatizo la tanzania ni kila kitu kufanywa siasa hata mambo ya kiutaalam yanafanywa kisiasa. rwanda ni kazi kwa kwenda mbele. hongera kagame !
   
 11. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Cheki GAPE kwenye nyekundu kutoka 5% mpaka 30% duh!
  Kumbe VITA vinasaidia,
  Lakini mimi naamini U- Dictator pia ni mzuri maana hivi vishgeria sheria hivi ndio wanavyovipindisha na kutuibia waziwazi,
  -Embufikiria mikataba ya MADINI.
  Fikiria DOWANS, RICHMONDULI, IPTL nk.
  Haya yote tungepata mtu kichwa ngumu yasingekuwepo!
   
Loading...