Rwanda na Urusi waingia kwenye makubaliano ya nyuklia

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,744
48,385
Hongera sana Rwanda, kainchi kadogo kiasi cha mkoa lakini kanaskika na kutikisa...

Raisi wa Urusi, Vladmir Putin amesema kuwa nchi yake inaweza kuisaidia Afrika bila masharti ambayo huambatanishwa kwenye misaada ya mataifa ya magharibi.

''Tunaona jinsi mataifa ya magharibi yanavyotoa mashinikizo na vitisho dhidi ya serikali huru za kiafrika,'' Putin ameeleza katika mahojiano na shirika la habari la Urusi TASS, kabla ya mkutano na viongozi wa Afrika.

''Wanatumia njia hizo ili kurejesha nguvu ya ushawishi na utawala kwenye makoloni yao ya zamani na kulinyonya bara la Afrika,'' aliongeza.

Urusi inatarajia kuwa mwenyeji wa viongozi 47 wa Afrika katika mkutano wa tarehe 23 -24 mwezi Oktoba mjini Sochi.

Bwana Putin amesema mahusiano na Afrika yemeimarika, akiainisha makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya silaha, ambapo Urusi imefanikiwa kushawishi mataifa zaidi ya 30 kuwasambazia silaha.

Rwanda ni moja ya nchi ambazo zimekuwa na mahusiano mazuri sana na Urusi

Baraza la mawaziri la Rwanda hivi karibuni liliridhia makubaliano na urusi katika masuala ya matumizi ya nishati ya nyukilia kwa ''matumizi ya amani'',Gazeti la The East Africa limeripoti.

Teknolojia hii itatumika katika uzalishaji wa nishati na utunzaji wa mazingira, ripoti imeeleza.

==============================================================
The Rwandan Cabinet has approved an agreement with Russia to advance the use of nuclear energy for “peaceful purposes,” a move that is expected to bolster relations between the two countries and advance the latter’s interests in the region.

This comes ahead of the first Russia-African Forum next week in the city of Sochi, which President Paul Kagame has confirmed attendance, accompanied by a delegation of senior government officials.
The nuclear power deal was first signed in Moscow last December and will see Russian scientists set up a Centre for Nuclear Science and Technology in Kigali.

The deal was boosted in May when a Russian government nuclear parastatal, Rosatom Global, reached an agreement to set up the nuclear plant by 2024—that the government says will help in the advancement of technology in agriculture, energy production and environment protection.

It has signed similar co-operation agreements with Kenya, Uganda and Tanzania even as questions over the appropriateness of the technology loom large.

In June Rwanda commenced negotiations to purchase Russian missile defense systems, as reported by the Russian press, as well as signed agreements to develop a military simulation and training centre in Kigali.

Hebu wewe mtaalamu nieleze kivipi ?
Sababu nyuklia ina ku offer mambo mengi sana

Ukiachana na kua na silaha za nyuklia ambazo mataifa makubwa hsa RUSSIA US na CHINA Wananufaika kwaajili hio

Lakini pia kuna faida mbali mbali ikiwemo kuzalisha umeme tena wakutosha kiasi kwamba kwa kanchi kama RWANDA Kanaweza kufaidika na kinu kimoja 2 cha Nyuklia kama wata amua kueka mtambo mkubwa tena umeme wa nyuklia maranyingi hua ni wa uhakika kuliko huu wamaji cjui na mwengineo

Pili Nyuklia inazalisha Mionzi ambayo inatumika kutibu(kupunguza kasi) yamaradhi ya kansa

N.k

Hakuna nchi ambayo haihitajii kua na vinu vya nyuklia kwa namna moja ama nyengne ukiachana na kuzalisha silaha za nyuklia
 
Kuna mwaka Taka za mabaki ya Nuclear toka France yalikuwa yanapelekwa Ujerumani ili kuteketezwa, sasa kama France wanapeleka Ujerumani Rwanda wataweza au ndo kujimwambafai kusiko na sababu, kwanz kanchi kana migogoro ya ndani wasijetumia kwa waasi wao
 
Sababu nyuklia ina ku offer mambo mengi sana

Ukiachana na kua na silaha za nyuklia ambazo mataifa makubwa hsa RUSSIA US na CHINA Wananufaika kwaajili hio

Lakini pia kuna faida mbali mbali ikiwemo kuzalisha umeme tena wakutosha kiasi kwamba kwa kanchi kama RWANDA Kanaweza kufaidika na kinu kimoja 2 cha Nyuklia kama wata amua kueka mtambo mkubwa tena umeme wa nyuklia maranyingi hua ni wa uhakika kuliko huu wamaji cjui na mwengineo

Pili Nyuklia inazalisha Mionzi ambayo inatumika kutibu(kupunguza kasi) yamaradhi ya kansa

N.k

Hakuna nchi ambayo haihitajii kua na vinu vya nyuklia kwa namna moja ama nyengne ukiachana na kuzalisha silaha za nyuklia
Katika mantiki hii ya mawazo yako (Inclusivity) basi kila nchi duniani ina uhalali wa kupata kila aina ya teknolojia ambayo nchi nyingine kubwa inao.

Ulivyotoa hoja hapo juu ni sawa na kusema kwamba Rwanda anaweza kumiliki vinu vya kurushia roketi na satelaiti angani kwasababu ana nchi zilizoendelea zinapata faida nyingi sana kutokana na miradi hiyo.

Hoja yako ni husishi (Inclusive) na linganishi (Comparative) lakini haiangalii uhalisia (Reality) wa nchi husika. Ukiangalia uchumi wa Rwanda, Usalama wake na Kiwango chake cha kiteknolojia. Hivi kweli Rwanda wanahitaji nishati ya kinyuklia wakati hata umeme wa kawaida tu wanazalisha kwa kiwango hafifu.

Upande mwingine wa shilingi ni kwamba uzalishaji wa nishati ya nyuklia ni gharama sana ndiyo maana mataifa mengi duniani hayataki. Gharama za ujenzi tu siyo chini ya dola za kimarekani Bilioni 5 ambazo ni sawa 13 za kitanzania. Ukijumlisha gharama zote (Financial Cost) kinaweza fika hadi dola bilioni 23 ambazo ni sawa na trilioni 50 za Tanzania. Unadhani Rwanda ana huu mtaji ?

Hapo bado hujaongelea gharama za kukiendesha na kukifanyia ukarabati, ambazo ni tofauti kabisa na gharama za ujenzi. Kinu cha nyuklia hupewa maisha ya miaka 10 hadi 15 (Life Span), ambapo kila baada ya miaka hiyo 15 inabidi kifanyiwe marekebisho makubwa na kufunga vifaa vipya. Rwanda unadhani ana hiyo pesa ?

Mwaka 2017 Marekani aliahairisha mradi wake wa kutengeneza vinu cha nyuklia kule California kwasababu ya gharama ya uzalishaji pamoja na kukwepa madhara mengine. Hivi vinu vina kawaida ya kupata hililafu, na gharama zake huwa kubwa sana, kule Japan kumaliza lile tatizo la Fukushima serikali yao iliweka bajeti ya dola za Kimarekani Bilioni 202 ambazo ni sawa na trilioni 500 za kitanzania.

Hii wanasema bado haitoshi zinatakiwa dola Bilioni 400 hadi 600. Sasa unadhani Rwanda wamejiandaa vya kutosha kukabiliana na tatizo kama hili endapo kinu kitapata hilirafu ? Japana ina wataalamu wengi wa nyuklia lakini bado wanahangaika. Rwanda ina wataalamu wangapi wa nyuklia mpaka sasa ?

Mwisho kabisa, Rwanda bado haijakaa sawa kisiasa (Not politically stable) hadi iaminiwe na teknolojia kubwa na hatari hivyo. Kipindi cha Raisi Jakaya Tanzania ilikuwa na mpango wa kuzalisha umeme wa nyuklia lakini zilitolewa hoja nzito sana na wataalamu wa mambo ya usalama. Wakasema kwamba jinsi Tanzania ilivyo na rushwa haitashindikana teknolojia ya namna hiyo kuazwa na kuangukia mikononi mwa nchi hatari au makundi ya kigaidi.

Israeli alipewa teknolojia ya nyuklia na akawauzia makaburu wa Afrika Kusini na wakatengeneza bomu la kiatomiki ili kuendelea kutawala, Uchina alipewa teknolojia ya nyuklia na Urusi yeye akawauzia Pakistan na wakatengeneza bomu, Korea Kaskazini alipewa na wachina na warusi na yeye akawauzia Syria. Unadhani ni jambo la busara kuwapa nchi changa kama Rwanda teknolojia hatari ambayo inaweza kutumika kuzalisha silaha za maangamizi ?

Ningewalewa kidogo kama wangesema Urusi ndiyo ambaye ameamua kuja kuwekeza hapo Rwanda, ili kuzalisha umeme na kuuzia nchi za Afrika. Lakini Rwanda kama yeye hana huo uwezo, na hawezi kuwa nao leo wala kesho. Hata hivyo bado ni jambo la hatari sana kiusalama kuruhusu teknolojia kama hiyo kuwekwa nchi yoyote ya maziwa makuu kwa kipindi hiki.
 
Yaani umeongelea masuala mengi na wala sijapingana na wewe

Ila kuhusiana na teknolojia haijalishi nani anayo wala nani hana ila kama ina maslahi kila taifa linahitajia kua nayo

Kuhusiana na suala la usalama na nn haya sikutaka kuyaongelea sio kama hayana maana hapana ila nlitaka kuelelezea kwamba kwakiasi gani

Nyuklia ina umuhimu napia ina nufaisha taifa lolote

Kuhusiana na madhara hakuna jambo lolote ambalo halina madhara ila una angalia hasara na faida ipi kubwa maana ukiachana na FUKUSHIMA nyuklia REACTOR Gan nyengne ulisikia ime pata madhara

Na ile ya JAPAN Iliripuka Koz Ya janga la kimaumbile 2 sio kaka iliripuka 2 yenyewe

Kuhusiana na suala la RWANDA Kuweza kuimanage hili jambo sikutaka kulizungumzia hili na usalama wake sababi tu nlitaka kutoa faida ambayo inapatikana na hizo nyuklia facilities

Umeongelea upungufu wa umeme RWANDA Unadhani wakiwa na hv vinu vya nyuklia watapata tena hio shida ya umeme halaf pia watakua na umeme wakuuza mpaka kwa nchi jirani

Unahisi watakua na ulazima sana wakuwapeleka wagonjwa wamaradhi ya kansa INDIA

Nb:sijasema RWANDA Wamiliki ama wafanye jitihada zakua nazo ila nime elezea umuhimu wake 2
 
NEEMA KWA AFRICA
Vladmir Putin ana mipango kabambe kwa Afrika?

Raisi wa Urusi, Vladmir Putin amesema kuwa nchi yake inaweza kuisaidia Afrika bila masharti ambayo huambatanishwa kwenye misaada ya mataifa ya magharibi.

''Tunaona jinsi mataifa ya magharibi yanavyotoa mashinikizo na vitisho dhidi ya serikali huru za kiafrika,'' Putin ameeleza katika mahojiano na shirika la habari la Urusi TASS, kabla ya mkutano na viongozi wa Afrika.

''Wanatumia njia hizo ili kurejesha nguvu ya ushawishi na utawala kwenye makoloni yao ya zamani na kulinyonya bara la Afrika,'' aliongeza.

Urusi inatarajia kuwa mwenyeji wa viongozi 47 wa Afrika katika mkutano wa tarehe 23 -24 mwezi Oktoba mjini Sochi.
Bwana Putin amesema mahusiano na Afrika yemeimarika, akiainisha makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya silaha, ambapo Urusi imefanikiwa kushawishi mataifa zaidi ya 30 kuwasambazia silaha. Rwanda ni moja ya nchi ambazo zimekuwa na mahusiano mazuri sana na Urusi.

Baraza la mawaziri la Rwanda hivi karibuni liliridhia makubaliano na urusi katika masuala ya matumizi ya nishati ya nyukilia kwa ''matumizi ya amani'',Gazeti la The East Africa limeripoti.
Teknolojia hii itatumika katika uzalishaji wa nishati na utunzaji wa mazingira, ripoti imeeleza.
 
Waje wao sasa

Hata wachina walikuja Africa kwa kigezo hicho hicho
Ila wao wamekuwa wabaya mara mia zaidi

Pamoja na uzungu wake Putin Sio mnafki ila ndio hivyo lao moja
 
Kama wanatuletea nuclear energy kutumika kwenye umeme sawa, ila kama shida zao ni kutuuzia silaha, hatuna bif na ncho yoyote sasa hivi, hela ya kuinvest kwenye silaha mara miia iende kwenye mambo ya muhimu kama elimu ambapo tuko nyuma sana.

Huyu ni sawa na mchina tu, wanapondea sana west huku alafu wanajichomeka polepole, in the end wote wanataka wanyonye hela zilizobaki basi. In fact kama wachina ni even worse, hate those mf
 
Kwahiyo ameona demand ya Africa ni silaha. Ameona Arabuni na Africa Niko silaha sinahitajika ili wakachinjane vizuri.
 
Hivi nani anagharamia hivyo vikao,mfano nauli,malazi na chakula? Kama ni waafrika wenyewe basi wanashida vichwani,kama ni Mrusi basi atueleze gharama itarudi vipi,coz as much as I know,there is no free lunch.
Kama wanatuletea nuclear energy kutumika kwenye umeme sawa, ila kama shida zao ni kutuuzia silaha, hatuna bif na ncho yoyote sasa hivi, hela ya kuinvest kwenye silaha mara miia iende kwenye mambo ya muhimu kama elimu ambapo tuko nyuma sana.

Huyu ni sawa na mchina tu, wanapondea sana west huku alafu wanajichomeka polepole, in the end wote wanataka wanyonye hela zilizobaki basi. In fact kama wachina ni even worse, hate those mf
 
Huyu jamaa na wenzake wa magharibi hawana tofauti.
Kutuuzia Silaha ndiyo ufanisi unaotakiwa na bara la Afrika ?
Tunafikiria namna ya kujikomboa kiafya ili kuondokana na maradhi ya kutisha kama Malaria, HIV /AIDS, Ebola nk.
Unatuletea silaha ili iweje?
 
afadhali mrusi na mchina ila sio marekani na uingereza. west wanapenda kupandikiza serikali za vibaraka kwa mgongo wa haki za binadamu na utumbo mwingine, wemejaa uchonganishi na kupenda vita. tofauti na mchina yeye anafanya biashara tu, hana masuala ya kuingilia serikali wala mambo ya ndani ya nchi... ni bora waje hawa wajamaa wa zamani
 
Heheee Warusi nao wamekuwa marafiki wa Afrika sasa
Nchi inayoogopwa duniani kote kwa ubaguzi na mauaji nao sasa wanawapenda Waafrika.. Na Waafrika tutawaamini kisa madikteta wetu wakikubaliana na huyo dikteta

Urusi na China ndio chanzo cha udikteta na mifumo ya kijamaa iliyofukarisha Africa miaka 60 sasa baada ya Uhuru.China ndie rafiki na dalali wa madikteta wote duniani
 
Back
Top Bottom