Rwanda kushinda kiti cha usalama katika UN, kwa kigezo kipi na Tanzania tuko wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rwanda kushinda kiti cha usalama katika UN, kwa kigezo kipi na Tanzania tuko wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Miwatamu, Oct 19, 2012.

 1. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Yawezekana sina kumbukumbu nzuri kama nasi tayari tunacho kiti kama hicho katika umoja huo wa kimataifa, lakini swali la msingi ni, Je, Rwanda imepita vigezo gani na kushinda nchi nyingine za bara hili la afrika hadi kupata nafasi hiyo wakati ni nchi ambayo inaonekana kuwa katika hali tete kila wakati ikiwa ni pamoja na kusaidia mwendelezo wa vita katika nchi jirani ? Naomba elimu yenu wanajamii.
   
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hicho kiti kinakwenda kwa mzunguko, japo kuna 'permanent members'. Tanzania nasi tulishakuwa na zamu yetu na tuiliitumia vema kupiga upatu wa kumuingiza Ban-Ki moon. Na aliyekuwa anatuwakilisha ni Balozi Mahige.
   
 3. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Tulishakalia hicho kiti kipindi cha Dr Asha Rose Migiro akiwa pale kwa karibu na balozi Augustino Mahiga.

  Kwahiyo sio big deal ni zamu zamu kukaa kwenye hicho kiti. Lakini kwa mtazamo wangu naona hicho kiti sio kizuri sana kwa sisi nchi changa unaweza kujikuta unawakorofisha wakubwa. Maana kipindi kile sisi tupo pale mambo ya Iran yalishika kasi kweli hadi nikaogopa.
   
 4. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,418
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 180
  jf ni shule tosha,we ambaye hujajiunga shauri yako
   
 5. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mheshimiwa kweli tupewe kiti wakati tunapiga raia mabom ya tumboni kweli??? Tunachoma manyumba na makanisa kweli???. Trekta za kulima kuzalisha chakula tunaziteketeza kweli????? Sasa hicho kiti mkuu nani atakikalia wakati kiti cha usalama hapa nyumbani sijui kakikalia nani? Hivi kiti cha usalama wa nchi na raia Tanzania kakikalia nani? kama kiko wazi tuambiwe. Watu wanakufa watu wanavamia mipaka, watu wanahamisha raslimali za nchi, watu wanahamisha fedha za nchi, watu wanajichulia sheria mikononi.Acha Rwanda wawe na kiti manake wamejifunza kutokana na vita vya kimbari sasa wanajenga taifa lenye kujali utaifa wa watu wao. Labda baada ya hii vita ya kimbari ambayo inapikwa ndo tutajifunza Najiuliza maswali sipati majibu labda Mkuu wa Nchi atatupa majibu Mwisho wa mwezi kama atakuwepo nchini.
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,098
  Trophy Points: 280
  Miwatamu, Maundumula, FJM, Kiona,

  ..ni kweli nafasi hii ni ya mzunguko kama walivyoeleza wana JF wengine.

  ..Tanzania tuliwahi kupata nafasi hiyo wakati Dr.Salim akiwa balozi wetu, na hivi karibuni wakati Dr.Mahiga akituwakilisha.

  ..tatizo nililoliona mimi ni kwa Rwanda kupewa nafasi hiyo wakati kuna ripoti ya UN inawatuhumu kwa kufadhili uasi mashariki mwa DRC.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Inaonesha ni umahiri wa rais Kagame - whatever the weather! Sijui kama ulishafuatilia safu ya watu wanaomshauri huyu rais, nikutajie wawili Tony Blair (waziri mkuu wa zamani UK) na Michael Porter - the father of 'competitive advantage....". Na pia swaiba mkubwa wa Bill Clinton.

  Kwa kiupi, Kagame hana muda na magumashi na hata kwenye giza anajua akimpigia simu mmoja wa maswaiba wake taa zitawashwa. Na ili upate hint, UK licha ya kusema watasitisha misaada waligeuka na kutoa pounds 16m. Kulikuwa na kelele lakini ndiyo hivyo tena.

  Tuangaze macho huku kwetu maana mgogoro wa Malawi bado.
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,098
  Trophy Points: 280
  FJM,

  ..kuna kipindi nadhani Sudan ilipewa nafasi kwenye kamati ya haki za binadamu ya UN wakati huohuo walikuwa wanatuhumiwa kwa genocide ya Darfur.

  ..nilichokuwa najaribu kumuonyesha mtoa mada ni kwamba hizi nafasi huwa hazina maana yoyote ile.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Niwemugizi

  Niwemugizi JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 15, 2012
  Messages: 909
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Du huyo ndo Kagame bwana, nyie mnabwabwaja na DRC yenu yeye anapaa tu, sie tujipange namna ya kupambana na Waislamu maana naona Rwanda sasa ni salama kuliko Tanzania
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,098
  Trophy Points: 280
  Niwemugizi,

  ..kule estern DRC kunaitwa "the rape capital of the world". thanks to Paul Kagame na magaidi wenzake.

  ..unazungumza frm the point of view of pro-Kagame, lakini wananchi wa eastern DRC r going thru something totally different.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. K

  Kirokolo Senior Member

  #11
  Oct 19, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 196
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Hongea Comrade Paul Kagame. Songa mbele, wacha wapiga filimbi wa Amelini waendelee kupiga domo.
   
 12. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  Tanzania nadhani walikuwa na nafasi kama hiyo kipindi kile cha kumchagua Katibu mkuu na kura yao ilikuwa muhimu kwa Korea kupata nafasi hiyo ndio tukaongwa nafasi ya Katibu mkuu msaidizi. Wazungu walitumind sana tu nakumbuka magazeti Uk yaliandika sana kuhusu kura za nchi za Afrika na ahadi za misaada kutoka Korea na nafasi za upendeleo
   
 13. Niwemugizi

  Niwemugizi JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 15, 2012
  Messages: 909
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Sasa kama dunia ipo kimya tufanyeje sasa, Kagame is so powerfully and for sure in this race he is not standing on his feet alone naona kuna watu wa nje wanambackup tu
   
 14. Johas

  Johas Senior Member

  #14
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mimi nadhani wametumia akili ndogo tu , yaani " Mchwawi mpe mwana amlee', kwa kupewa kitu hicho Rwanda itathibitisha kwamba si kwa bahati mbaya kwani itajitahidi kuleta na kujikita zaidi katika diplomansia za Amani hasa katika ukanda wa maziwa makuu ambapo Rwanda inahusishwa na kuunga mkono ( kuwasaidia) kundi la waasi masharki mwa Congo, DRC.
   
 15. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Wanajamii wote mliojibu na mliosoma thread yangu hii naomba nikushukuruni kwa jinsi mlivyoweza kuidadavua vilivyo na kutoa weledi mpana zaidi. Jamvi hili litaonekana la maana zaidi ikiwa tutakuwa tunapeana elimu namna hii. Nawashukuruni sana.
   
 16. StayReal

  StayReal JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2012
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 519
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hawa Rwanda si ndio tulioambiwa wanaeneleza vita DRC! Then how come wamepewa hii kitu au it was not true!
   
 17. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #17
  Oct 22, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ukimuona Kobe juu ya mti ujue...
   
Loading...