Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,865
- 3,801
1. Unaishi kwenye nyumba nzuri lakini pembeni yako kuna choo kinatililisha kinyesi,harufu mbaya kila kona
2. Nyumba nzuri zinajengwa hovyo hovyo kwenye skwata msimu wa mvua zinageuka madampo ya maji taka.
3. Nyumba zinajengwa juu milimani , siasa chafu na za kishamba ole wake atakaewafukuza wapiga kura wangu.
4. Barabara nzuri zinajengwa zikimalizika tu machinga wanazigeuza masoko. Ole wake atakaewagusa wapiga kura wangu.
5. Wafugaji na wakulima wanavamia vyanzo vya na hifadhi tengefu. Ole wake atakaewasumbua wapiga kura wangu.Km unaona kilimo rahisi kalime na ww!
5. Unajenga barabara za mwendo kasi wakati mabasi yapo hoi bin taabani,watu wanajazana kama magunia ya korosho. WatanzaniaTuko vizuri tembeeni kifua mbele!
Rwanda wanajenga nchi yao huku wakizingatia taratibu na sheria za kisekta na nchi kwa ujumla. Usafi unazingatiwa, ujenzi holela haupo, bodaboda hawaingii katikati ya mji.
Ndio maana hata wakijenga chochote kile kinaonekana kinang'aa. Sisi hata mji ujengwe vipi hauwezi kupendeza kamwe kwa sababu tumeamua taifa lote kuwa gulio.
Hata Dodoma ni suala muda tu, na wenyewe utakuwa kama Kariakoo tu. Watalii (Wazungu) ni watu wa utaratibu. Mtu hawezi kuvutiwa kutembelea taifa ambalo kila kitu kinaendeshwa hovyo hovyo.
Uchafu kila kona. Ndio maana Rwanda wanaingiza zaidi ya dola Mil.4 kwa mwaka wakati sisi hata hesabu haieleweki. Sijui alivyoenda Rwanda alienda kujifunza nini?
Nadhani kama Taifa tunahitaji Rais mjanja anaejua nini maana ya maendeleo. Mwenye plan zinazoeleweka na za muda mrefu sio mkurupukaji.
La sivyo tutaendelea kutia aibu tu.