Reginald L. Ishala
JF-Expert Member
- Jun 18, 2011
- 3,811
- 6,780
Utalii
Kama ilikuwa ni kwa ajili ya ndege basi wangetangaza ndege.Siyo waste of money kwasababu Rwanda wana ndege yao ambayo sasa inaenda London Gatwick, hivyo pamoja na kampeni hii, pia itawasaidia watalii kukata tiketi za moja kwa moja kwenda Kigali badala ya kuunganisha ama Dar au Nairobi.
Pili, kumbuka wamesema fedha zinazotumika ni sehemy ya fedha ya mapato yatokanayo na utalii huohuo, hivyo kuonyesha kwa kiasi kikubwa kwamba wanaweza kutumia fedha za aina hii kwa nidhamu badala ya kuzitapanya huku na kule.
Dah! haya mkuu, unazungumzia demokrasia.
Lakini Rwanda inapiga hatua mbele, Tanzania je tuliweza kuweka mabango huko London kutangaza vivutio vyetu vya utalii kwa angalau miezi sita?
Yaani watu wataangalia neno "visit Rwanda" na suddenly wawe interested kwenda Rwanda kwa Kagame!!? Kuna "kivutio" kipi kwenye maneno hayo? Hawa Rwanda walifanya kweli investigation ya kutosha? Kwa nini wasingeingia deals na famous sports channels na kuonyesga vivutio vyao, au deal la Arsenal ndo cheap zaidi compared na alternatives nyingine?
Nimekaa chini nikaandika uzi kwa juhudi zangu mwenyewe na nyie mkaona kwa mamlaka yenu muugeuze uwe post kwenye uzi mwingine. Haya ndo mambo yanayochosha kuweka uzi humu. Jirekebisheni! Maxence Melo Paw Moderator Invisible JamiiForumsHabari,
Hivi karibuni nchi ya Rwanda ambayo kitalii ikijinasibu kama nchi ya vilima maelfu (the land of a thousand hills) imejipambanua zaidi kwa kuwekeza kwenye sekta ya utalii kwa manufaa na tija kuu. Nchi hii ya Afrika Mashariki pasipo kujali udogo wake na hata basi tuseme uhafifu wa vivutio vyake ukilinganisha na nchi kama Tanzania, imeonyesha 'tamaa na uchu' wa kutaka kupiga hatua kubwa ya kimapinduzi kwenye kuujuza ulimwengu juu ya uwepo wake lakini pia urithi wake wa asili.
Bwana Kagame, raisi wa Rwanda, ambaye ni mfuasi mkubwa wa timu ya mpira ya Arsenal yenye maskani yake jiji la London, Uingereza, aliona asiishie tu kuipenda timu hiyo bali pia aitumie kwenye 'kuipendezesha' zaidi nchi yake kwa kupitia fursa ya kibiashara ya kimatangazo, na kwakuwa basi Arsenal ni moja ya timu inayocheza kwenye ligi inayotazamwa zaidi Duniani, pia ina wapenzi maelfu na maelfu ulimwenguni kote, basi ni bayana faida ingalikuwapo kwa uhakika.
Kuthibitisha hilo tunaambiwa kwa kupitia mtandao NEW TIMES AFRICA kwamba tangu bandiko la 'VISIT RWANDA' liwekwe kwenye sare za Arsenal kumekuwa na ongezeko kubwa sana la watu 'kusearch' neno Rwanda mtandaoni ili kupata kujua yaliyomo huko, kwa takwimu idadi hiyo ni kubwa kuliko idadi ya mwaka mzima wa 2017 (January to December) wakati bandiko hilo halijadumu msimu mzima! Lakini pia Rwanda imepata 'media coverage' kubwa ulimwenguni kutokana na kufaidika na vyombo vyote vitakavyorusha matangazo ya timu ya Arsenal.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Hall & partners, asilimia 71% ya mashabiki wa Arsenal hawakuwa wanaiwazia Rwanda kama sehemu ya kufikia kiutalii kabla ya kuanza kuiona kwenye 'jerseys' zao. Zaidi katika asilimia hiyo, 51% walikiri kuwa ushirikiano baina yao na Rwanda umewafanya wafikirie kwenda huko kitalii kitu ambacho kimeanza kubadili taratibu mawazo ya watu juu ya nchi hii ya Rwanda (People's perception on Rwanda).
Zaidi, chaneli za mitandaoni za Rwanda zimefaidika kwa kiasi kikubwa na 'partnership' hii (Instagram +577%, Twitter +72% and Facebook +44%) ambapo huko pia wanatumia nafasi hiyo kuonyesha kila kitu ambacho kinaweza kuwashawishi watu ulimwenguni kutembelea nchi hiyo kitalii. Leo hii warwanda 142,000 (idadi inaweza ikawa imeongezeka) wameajiriwa moja kwa moja kwenye sekta ya utalii kutokana na mpanuko wa sekta hiyo ingali mwaka 2017 waajiriwa wa moja kwa moja walikuwa 90,000 tu!
Kama haitoshi, Rwanda sasa wanaangazia ligi yingine ya Ufaransa wakiwa wameadhimia kuteka 'French Market' na hata Ulaya nzima pia kwa kupitia mgongo wa klabu ya PSG kwa mtindo wa udhamini. Karibuni sasa utaona 'jerseys' za PSG zenye chapa 'VISIT RWANDA' na pia baadhi ya watu wake mashuhuri kufunga safari kuja kuitembelea Rwanda kwa ajili ya motisha ya kitalii.
Vipi kuhusu sisi? Ardhi ya mlima mrefu kuliko yote barani Afrika kupigwa kikumbo na Ardhi ya vilima (Land of a thousand hills)? Tunatumiaje fursa kuinua zaidi utalii wetu kwenye ulimwengu huu wa ushindani?
Hapa Tanzania walikuja wasanii na hata wanamichezo wengi mashuhuri duniani, mfano muigizaji Will Smith, je tulifyonza nafasi hiyo tukapata kila bora lake? (The best out of it)?
Ama hatuna 'njaa' kihivyo?
View attachment 1281797View attachment 1281810