Rwanda: Hizi ndizo hatua zinazochukuliwa na serikali kukabiliana na janga la Corona

CityHunter1

JF-Expert Member
Feb 25, 2016
668
500


Neno Corona, hakika sitakuwa nimekosea nikisema linatawala vinywani mwa wanadamu kwa sasa kuliko maneno mengi tunapoongelea magonjwa ya mlipuko. Hii imetokana na uzito wa maradhi yenyewe, hasa kwa vifo vinavyotokea kila dakika ulimwengu mzima kufuatia mlipuko wa ugonjwa huu.

Kuna badhi ya watu walioichukulia kimzaha mzaha, lakini ukweli usiopingika ni kwamba ni ugonjwa hatari. Mbali kuogopesha watu, hasa matajiri na viongozi wakubwa dunia nzima, wapo waloanza kujinyonga hata kabla hawajafikiwa. Vifo vya hapa na pale, matajiri, madaktari, watu wa kila rika.

Rwanda, kama nchi ndogo, imepiga hatua kadhaa nzuri na za kufurahisha kuwalinda raia wake na madhara makubwa yatokanayo na janga hili. Mimi nimeishi hapa na nimeona kuna funzo kwa nchi nyingine jirani.

Mwanzoni, hata Rwanda makosa yalifanyika, waliruhusu watu kutoka safari za uarabuni kuingia bila kuwekwa karantini. Baada ya siku tu zisizozidi 5, wale wageni walikuwa tayari na dalili. Serikali ililazimika kufunga mipaka ya anga na ardhini.

Navyoandika hivi sasa (Aprili 11, 2020) ni wiki ya tatu sasa hakuna ndege kuruka, isipokuwa kwa sababu maalum na zisizoepukika. Magari ya abiria toka siku serikali ilipotangaza hali ya dharura, yamepigwa stop, watu wote wamelazimika kubaki majumbani kwao kasoro tu wale wanaouza vyakula, maduka ya madawa, na benki. Sekta nyingine zisizo na utoaji huduma wa haraka zimesitishwa.

Ni kweli kusitisha ghafla huduma imeathiri wananchi kwa kiasi kikubwa. Lakini, kipi bora kati ya njaa inayoweza kuzuilika na ugonjwa ambao kwa hali zetu si rahisi kutibu kwani hauna tiba wala kinga?

Hapa Rwanda tulianza na mgonjwa mmoja tu, lakini mpaka sasa idadi imefika watu 118. Hii imetokana na nini? Mtu anapokuwa na virusi na bado yuko huru kuungana na jamii, ni dhahiri kwamba atakutana na watu wengi na humo humo wengi wao wataathirika. Kwa wale ambao wana uelewa mdogo, ugonjwa huu wataufananisha na magonjwa mengine (kama mafua au malaria); wanakosea sana!

Serikali ya Rwanda iliona baadae itaelemewa na mzigo wa wagonjwa na vifo, ikaamuwa kuunda timu ya kuwasaka na kuwaweka sehemu zilizotengwa wanaohofiwa kuwa na virusi hivyo. Haikuwa kazi rahisi, lakini mpaka sasa bado serikali inakabiliana na usambaaji wa virusi hivi. Cha ajabu sasa, wale walotengwa ndo humo humo inatoka hiyo idadi niliyotaja juu, kila kukicha.

Bahati nzuri na kwa jitihada hizo, kwa sasa hapa Rwanda hatuna mauti au mgonjwa mahututi.

Jana, hapa Rwanda wamepatikana wagonjwa 5 waliokuwa uraiani na imegundulika walikutana na baadhi ya watu waliopo huko walikotengewa.

Kwenye suala la misaada kwa walioathirika, hasa wale vibarua wapatao mlo mmoja tena baada ya kutumia nguvu zao kila siku, Serikali imejitolea kuwagawia chakula cha msaada mpaka pale watakapojiridhisha kutokuwa na maambukizi mapya. Wanyarwanda wenye uwezo (raia) wamejitolea kuwasaidia majirani zao. Viongozi mbalimbali wa Serikali mishahara yao ya mwezi mmoja imetolewa kuisaidia Serikali kuwalisha wananchi.

Kwa sasa safari za mikoani ni marufuku, jambo ambalo limewapa kikwazo walalahoi, lakini kuliko kupeleka ugonjwa huko, ubinadamu umetumika na siku zinasonga.

Kubaki nyumbani, imekuwa ni amri. Polisi kuanzia wa ngazi za juu mpaka wa chini, mgambo na 'reserve force', wako mitaani kuzuia safari za hapa na pale. Jambo ambalo kwa sasa ni muhimu.
Sokoni(kumbuka, imeruhusiwa kufanya tu biashara ya vyakula),kila mlango unaopokea watu,maji safi na sabuni kwa ajili ya kunawa mikono yapo.

Wenzetu huko Tanzania, mmejipangaje kukabiliana na janga hili?

Corona unaifata wewe, haikufuati kwako - BAKI NYUMBANI, USALAMA KWANZA
 

CityHunter1

JF-Expert Member
Feb 25, 2016
668
500
Bakhresa kawapa Rwanda msaada wa unga wa ngano tani 20 kusaidia wasio na uwezo!

Corona haijaja kwa ajiri ya masikini, wanaposema janga, halichagui.
Kama kweli usemalo lipo, ni neema pia na tunamuombea Mungu amuongezee.
Huu si mda wa kujifikilia, corona ni mdudu hatari, haogopi kupanda ngome za matajiri na viongozi.
Ulichonacho, kula na wenzio.
 

CityHunter1

JF-Expert Member
Feb 25, 2016
668
500
Ungekuwa na akili usingeuliza habari za Tanzania. Sababu wanyarwanda shopping yao kubwa ya chakula ni kahama. Mchele na bidhaa nyingi wananunua kahama. Rwanda sio nchi ya kuifananisha na Tz. Kaa kimya ulale.
Asante,
sijafananisha Rwanda na Tanzania, lakini, kumbuka, Corona si ya Rwanda tu
 

COTANGENT

JF-Expert Member
Nov 24, 2012
449
250
Tanzania tumeambiwa Covid-19 ni kaugonjwa kadogo sana, hivyo tuchape kazi, ndege ziruke, mipaka iko wazi yani business as usual. Tahadhari yetu ni kunawa mikono na kuendelea kumuomba Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

CityHunter1

JF-Expert Member
Feb 25, 2016
668
500
Najua ila mada yako ilihusu hasa uwezo wa kuwa na chakula. Rwanda sio kama unvyoielezea. Leo hii wakiruhusu watu kuhama Rwanda nafikiri 50% watahamia Tanzania.
Umenielewa vibaya ndugu yangu.Nilichokiongelea ni hatuwa zilizochukuliwa na serikali.
Swala la chakula, ntakuwa muongo nikisema kinatosha(japo sijaandika popote). Wamejitahidi kuwachangia wale ambao hawana uwezo wa kuweka akiba,na si kwamba wote wamepewa, ila angalau ni moja wapo wa hatua za kuwasaidia wananchi
 

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
11,032
2,000
Nchi ukubwa wake mikoa 3 ya Tz hata hela Arizonazo MO anaweza kawalisha miaka 2 hata wakizuia safari sio mbaya
 

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,126
2,000
Umenielewa vibaya ndugu yangu.Nilichokiongelea ni hatuwa zilizochukuliwa na serikali.
Swala la chakula, ntakuwa muongo nikisema kinatosha(japo sijaandika popote). Wamejitahidi kuwachangia wale ambao hawana uwezo wa kuweka akiba,na si kwamba wote wamepewa, ila angalau ni moja wapo wa hatua za kuwasaidia wananchi
Kwa hiyo unadhani Tanzania ikiwa katia critical condition haiwezi kuwasaidia wasiojiweza? Rwanda ni kama wilaya flan tu ya Tanzania. Kwa hiyo tulia. Acha fitina za kisiasa.
 

Kesaboso

JF-Expert Member
Apr 16, 2019
426
500
Na wale wamarekani walioanza kufa wakiwa wamejiweka lockdown nani aliwapelekea ndani mwao?
Hili gonjwa ni kuomba mungu na kufata tu njia za usafi, kama swedeni bado shule hazijafungwana lockdown hakuna wao pia hawajali watu wao?
Super power marekani pamoja na interejensia na technology walio nayo bado yamewakuta, ndo ujue hakuna cha rwanda wala nni, tufate taratibu lakini kusema nani kafanya vema ni uongo.
 

THE LOST

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
1,074
2,000
et mishara imekatwa ili inunulie chakula zinakutosha kweli wewe? Mauaji ya kimbali hamkujizuia mkauana Leo et corona hamuitaji duh..
 

CityHunter1

JF-Expert Member
Feb 25, 2016
668
500
et mishara imekatwa ili inunulie chakula zinakutosha kweli wewe? Mauaji ya kimbali hamkujizuia mkauana Leo et corona hamuitaji duh..
Mpo na mtakuwepo tu. Corona na mauaji wapi na wapi? Wewe au ndugu zako mmeua na kukimbia, sasa mema ya nchi ni kidonda kwako eh! Huna la kusema,pita tu
 

Tz mbongo

JF-Expert Member
Mar 12, 2015
8,146
2,000
Mie bado nauliza ikiwa huku afrika nako tulichelewa kufunga mipaka kama wenzetu huko na wengine hadi sasa bado hawajafunga mipaka,kwanini sasa corona imesambaa sana huko kwa wenzetu na kusababisha madhara makubwa tofauti na afrika ambapo tunaambiana kuwa tusitishane?
 

Marry Ngowi

JF-Expert Member
Sep 6, 2013
262
1,000
mtoa mada hiyo mada yako inaitwa fake news au propaganda! wallah nimeona kwa macho yangu France24English channel kuna mama Rwanda anahojiwa kiwiziwizi anasema ndani kwake hana chakula yeye na watoto wanne wamefunga shule wako home wanakufa na njaa!

na pia ikaendelea stori kwa hiyo channel kuwa kuna watu waliuwawa wakijaribu kutoka nje kusaka chakula na wazungu walipohoji serikali ikadai askari waliwaua walifanya self defence!! pia kuna stori za watu kubakwa na askari!! tuma email kwenye hiyo channel utumiwe hiyo habari!! hamna hela nyie maskini tu kama sisi mnaiga wazungu subiri mfe na njaa kwa kufunga mipaka na lockdown yenu!!njaa ikizidi watu watatoka nje kibishi na fujo yake hamtaiweza na Interahamwe walioua watutsi miliioni moja wa Rwanda na kuwazika makaburi ya halaiki watapata loophole!

Karl Peters wenu wa Rwanda (mkono wa damu) ukisema habari yoyote kinyume na mtazamo wake atakusaka hata ujifukie shimoni kwa wahadzabe huko Manyara atakufukua na kukunyonga! ukipanda juu hewani na ndege kama Habyarimana unatunguliwa huko huko! conspirancy theories wanasema kuna mifano mmepewa mtulie ni wale marais Habyarimana na Ntaryamira waliotunguliwa, yule wa hotelini South Africa , yule wa Kenya, yule wa Norway na yule mlimuua na kumtupa mbele ya nyumba yake Kigali!! waulize wenzako majina yao wanao!

Tanzania ni nchi pekee Africa yenye special minds na full information for almost everything!! watafute wa kuwadanganya sio watz!!

Iran wanakufa watu mia kila siku ila leo wamesema lockdown haina faida wanaachia! Japan wamesema uchumi wao hauruhusu lockdown business as usual masks tu wote kazini sasa nyie Rwanda mna uchumi kama Japan? Zimbabwe wamefungia watu ndani kutokana na umaskini wamechemsha njaa kali watu wametoka zao nje wote na serikali haina la kufanya haina hela haijawafanya kitu imepotezea lockdown , business as usual now!! South Korea kuna wagonjwa wa Covid19 walipona hospital wakarudi ndani wamepata Coronavirus upyaaa ngoma inaanza tena!! Norway watu wanakufa ila na wao wanafikiria kulegeza kamba!! Sweden na Brazil business as usual , watoto wa kizungu Sweden wanapanda baiskeli zao wanaaga home wanasema ’we go out to town to drink Corona’!!!Trump amepagawa watu wanakufa elfu mbili kwa siku ila anataka kufungua geti kibishi watu watoke coz uchumi unashuka kwa kasi watu 17m hawana kazi wanataka wapewe msosi daily na serikali iliyowafungia!!

na kwanza mtalockdown kwa muda gani wakati maambukizi yenu na maambukizi ya dunia nzima yanazidi kila kukicha? kama Corona sasa ina miezi mitano inazidi ikienda hadi December mnaweza? mna hela gani Rwanda?

usipotoshe wabongo, Rwanda acheni ulimbukeni kuiga wazungu contexts dictate solutions!! Rais wenu anafurahia lockdown ni nzuri kuwakomoa na kuwakomesha raia wasiompenda na ni nzuri kwa usalama wake na wa watutsi, Rais wa Uganda hakuna raia anamtaka lockdown ni kitu bora sana kwa kuwakomoa na kuwakomesha raia wabishi wafuasi ya Boby Wine , Kiiza Besigye na Cameleon!

usitufundishe namna ya kuishi nyumbani kwetu!!siku si nyingi mtatuomba msaada sisi ni donor to fellow Africans au hujui nchi tulizowapa msaada nikutajie?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom