Ruzuku za vyama vya siasa Tanzania na global financial crisis | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ruzuku za vyama vya siasa Tanzania na global financial crisis

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Steve Dii, Feb 26, 2009.

 1. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  WanaJF, naomba maoni yenu na kueleweshwa vizuri kuhusiana na hili swala.

  --- Mgawanyo wa ruzuku kwa vyama vya siasa hapa nchini Tanzania ukoje?

  --- Vyanzo vya ruzuku hizi ni nini?

  --- Makadirio ya mapato kutoka vyanzo hivyo ni yapi?

  --- Je, kuna limitations zozote katika kupokea michango kwa ajili ya ruzuku za vyama (kutoka watu binafsi, miradi, mashirika, etc..)?

  --- Ni taasisi gani inashughulika na ufatiliaji wa michango katika vyama vyetu?

  --- Je, taratibu zipi na adhabu zipi zipo iwapo miongozo iliyopo inakiukwa katika upatikanaji wa ruzuku na matumizi yake?  Ninasoma mengi kuhusiana na wizi wa mabillioni nchini. Shutuma nyingi zinaelekezwa kwa chama tawala, CCM. Ya kwamba, kuna pesa nyingi kutoka vyombo mbalimbali vimepoteza mabillioni ya pesa kwa ajili ya jaribio la kufanikisha uchaguzi wa 2005. Wahusika wengi wametajwa. Kila ninavyozidi kusoma, utetezi wa shutuma hizi ni kama vile unakosekana, hivyo kupelekea shutuma hizi kuwa kweli pamoja na kwamba kuna kesi mbalimbali bado zinashughulikiwa mbele ya sheria.

  --- Ninachojiuliza mimi hivi sasa ni kwamba iwapo shutuma hizi zote ni kweli, funding ya uchaguzi itafanikiwa vipi kwa uchaguzi ujao kwa upande wa CCM?

  Kutapakaa kwa pesa kama ilivyokuwa kwa miaka 2 - 4 iliyopita kumepungua na kunazidi kupungua kwa kasi kubwa sana pahali pengi duniani kutokana na financial crisis iliyopo. Nchi wahisani (donor nations) zimekumbwa na recession, hapa kwetu yaonekana bado tunajirusha kama kawa...

  --- Swali: Vyama vyetu vimejihimu vipi na crisis hii kwenye upande wa ruzuku zake kiutendaji na kwenye uchaguzi ujao?

  Hivi karibuni kumeibuka ufunguaji wa matawi ya vyama nchi za ughaibuni, haswa yale ya chama tawala, CCM.

  --- Maswali: Funding ya uendeshaji wa matawi hayo vyanzo vyake ni vipi?

  --- Kama kuna michango mbalimbali ya pesa kwenye matawi hayo kutoka kwa wanachama au chanzo chochote kile, pesa hizo zinaratibiwa vipi kwa hapa nyumbani?

  --- Je, kuna limitation yoyote katika funding za matawi hayo na nani mratibu wa hili kwa serikali?

  --- Je, matawi ya vyama vya upinzani yanaruhusiwa?

  --- Je, nguvu ya wanachama hao (tawala na upinzani) ni ipi katika chaguzi zetu hapa nchini? (je wanaweza kupiga kura kuwakilisha uchaguzi fulani hivi hapa nchini wakiwa huko huko, au?)

  --- Iwapo linatokea tatizo kwenye matawi hayo ya ng'ambo, serikali yetu inashughulikiaje tatizo hilo? (Scenario ni kwamba - kunatokea mgongano kati ya wanachama wa vyama tofauti nje ya nchi)

  Ahsanteni, ni haya tu kwa sasa.

  SteveD.
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Si ajabu Mwakani tukaambiwa WaTanzania waishio nje wataruhusiwa kuiba kura.
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Fafanua zaidi tafadhali mkuu...
   
 4. K

  Kwaminchi Senior Member

  #4
  Feb 27, 2009
  Joined: Dec 30, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa maoni yangu, huu mpango mzima wa vyama vya siasa kupewa ruzuku, ni ujanja wa TANU/CCM kutafuna nchi. Ki-uwiano, hili zoezi la ruzuku linakinufaisha chama tawala. Wao ndio wanaopata fungu nono la ruzuku.

  Endapo ruzuku ikikomeshwa chama tawala ndicho kitakachoathirika kwa asilimia kubwa sana.

  Kwa desturi vyama vinatakiwa vijitegemee kutokana na wanachama wake. TANU ilijitegemea wakati wa ukoloni. Na ndivyo ilivyokuwa kwa UDP, ANC, UTP na vyama vingine wakati ule. Sioni sababu kwa nini ishindikane kwa wakati huu.

  Hizi ruzuku za vyama, hazina tofauti na hii tabia ya omba omba ya nchi. Inajenga tabia mbaya sana inayodekeza hata vyama vyetu vya michezo kungojea wafadhili.
   
 5. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ....?
   
 6. O

  Ogah JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  kwi kwi kwi.......too picky ma friend!.........NN anakutafuta......
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Feb 27, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  aaah bana....usimshtue sasa na wewe...kwanza simtafuti wala nini....

  vipi sasa dk. masau?
   
 8. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145

  https://www.jamiiforums.com/384920-post14.html
   
 9. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kuna thread mpya ya ruzuku CUF may be iunganishwe na hii!
   
 10. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mgawanyo wa ruzuku kwa vyama vya siasa kutoka serikalini umeelezwa katika sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, sheria no 5 na kurekebishwa mwaka 1996 na sheria no 11. Sheria hiyo inasema, ruzuku ya serikali itapewa kwa vyama vya siasa vyenye wabunge na madiwani kwa asilimi, na vyama vinavyotimiza masharti ya kuendesha chama kwa miongozo yake. Inamaanisha, wenye wabunge wengi ndio watapata nyingi.

  Serikali kwa mwaka 2008/2009 ilitoa bilioni 18 kwa ruzuku, 2007/2006 ilikuwa 16, na 2005/2006 billion 39… sikumbuki vizuri hesabu zake. Pia sifahamu kila chama kilipata kiasi gani.
   
 11. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  a)michango ya hiari, b) ada za wanachama c)Ruzuku ya Serikali d) hisa ama miradi mbalimbali ya chama - makapuni yakiwemo etc... soma vyanzo vya mapato katika Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, kifungu cha 13 (1)
   
 12. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli hamna kiwango! unaweza kukusanya popote kutoka kwa yeyote, ila kifungu cha 13 (2) kinataka vyama vya siasa vitoe taarifa za kina kuhusiana na michango yato kutoka kwa watu ambao sio raia, na mashirika ya nje kila mwaka.

  Hapo kunamwanya, maana, kimsingi vyama vya siasa havijatajwa kwenye sheria za fedha za umma ili mtibit mkuu was hesabu za serikali aviangalie. Kwahiyo, msajili wa vyama vya siasa kupitia sheria ya 1992, vyama vyote vya siasa vinapaswa kupeleka hesabu zake kwa msajili kila mwaka baadaya ya hesabu hizo kuhakikiwa na mwanamahesabu wa chama. Msajili akizipokea anapaswa kuzichapisha kwenye gazeti la serikali. Basi hapo ndipo songombinde inapochezwa.

  Mwanamahesabu ni wa chama, CAG hajishughulishi kuangalia hesabu za vyema, msajili hana uwezo wa kuhakiki mahesabu hayo! basi mchezo wa kuigiza tu unakuwa.

  adhabu zipo zilizoinishwa kwamba wanaweza kufungia chama, kufunga viongozi - lakini ufuatiliaji ni mdogo kwahiyo yamebaki kuwa maandishi tu
   
 13. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #13
  Mar 27, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  SteveD, nadhani katika kuweka maswali haya unaangalia vitu viwili muhimu;
  - Campaign finance reform
  - Impact of Global economic crisis on election funding

  Nadhani vyote viwili ni muhimu na ndo kiini cha mabadiliko ya kisiasa nchini , kwani imani yang uni kwamba wananchi wa Tanzania wameshachoka na CCM na wako tayari kubadilisha uongozi, kinachogomba ni funding. Na factors hizi mbili zitawabana sana CCM.

  Petu Hapa: asante kwa taarifa nzuri na iliyo kamili, lakini labda tu niulize hivi kuna initiative yoyote bungeni ya kufanya campaign finance reform?
   
 14. U

  Uswe JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  RUZUKU Hapana, Pinga Ruzuku kwa vyama vya siasa, Pinga Ruzuku! Wawe na sera nzuri, wananchi wataovutiwa na sera zao watawachangia, mfano, mie sipendezewi hata kidogo na tabia ya CCM kukumbatia mafisadi lakini sina namna ya kukataa kodi yangu isiende CCM kupitia ruzuku.
   
 15. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2013
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ndugu Msajili wa Vyama,
  Ndugu wananchi,
  Kwa heshima napendekeza ruzuku inayotolewa na serikali kwa vyama vya siasa ifutwe. Hizo fedha takribani bilioni 1 na milioni 200 kila mwezi, tuzitumie kuajiri madaktari na walimu. Naam, tuwe na walimu wa kutosha, wafundishe vijana wetu wasifeli mitihani hadi tukalazimika kuwarekebishia matokeo kiaina. Vyama vitafute namna ya kugharimia shughuli zao.
  Natanguliza shukrani kwa watakaoniunga mkono katika hili.
   
 16. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #16
  May 4, 2013
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hujui kazi kubwa inayofanya ruzuku katika kujenga demokrasia ndogo unayoiona katika nchi hii. Katika nchi ambayo utamaduni wa kuchangia vyama vya siasa Haupo,.ruzuku haikwepeki
   
 17. M

  Molemo JF-Expert Member

  #17
  May 4, 2013
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Haya mazuri yaliyoletwa na Chadema ni ruzuku imefanya kazi.
   
 18. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2013
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Huo utamaduni wa kuchangia unaweza kujengwa, na sio kwamba haupo kabisa.
  Aidha, katika nchi ambayo kuna utegemezi bado katika bajeti ya serikali, na hatujaweza kuwa na wataalam wa kutosha katika kada nilizozitaja, uotaji wa ruzuku lingekuwa jambo la mwisho kufikiriwa.
   
 19. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2013
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  na hayo ya ajabu yanayoletwa na CCM ni ruzuku ya m.800 imefanya kazi?
   
Loading...