Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 297
Kwa vile Chadema kimejitokeza kuwa chama kikuu cha upinzani (a Government-in-Waiting), na kimetokea kuaminiwa na watanzania wengi, kitumie kipindi hiki cha kabla ya uchaguzi wa 2015 kujijenga kimuundo zaidi ndani na nje ya chama. Nitazungumzia muundo wa nje ya chama kwa vile muundo wa ndani umekamilika.
Tunajua ruzuku ya chama itaongezeka, ni wito wangu kwa viongozi kwa vile watanzania wameanza kuwaamini(kwa kuwapa kura za kutosha ofcourse) badala ya sehemu kubwa ya ruzuku kutumika kwenye mambo ya administrations itumike kujenga miundombinu ya chama.
Chadema inaweza kuanza kwa kupata ofisi za kudumu za mikoa, inawezekana kabisa kutenga kiasi fulani cha ruzuku kila baada ya miezi miwili na kujenga au kukodi ofisi moja ya mkoa. Wakifanya hivi kwa muda wa miaka miwili wanaweza kuwa wamekamilisha mikoa yote ya Tanzania.
Chadema ni chama cha kudumu viongozi wake wawe na mitazamo (vision) ya muda mrefu hata kuanza kufikiria kujenga makao makuu ya kudumu, ofisi wanazotumia leo zinaweza kuwa ofisi ndogo za chama au ofisi za wilaya ya Kinondoni, mbona CUF waliweza kununua jengo la ghorofa moja/mbili kwa ruzuku ya muda mfupi. Inawezekana kinachotakiwa ni commitment.
Vilevile wajaribu kuzipatia ofisi za wilaya uwezo kama usafiri wa uhakika na mawasiliano kuwezesha smooth running kati ya makao makuu na wilayani waliko wapiga kura. Kama tumeamua kuijenga nchi kupitia Chadema inawezekana tuache tamaa.
Nawasilisha.
Luteni is a True Revolutionist