Ruzuku kwa vyama vya siasa iondolewe Tanzania!

tuendelee kujadili

CCM inapata zaidi ya 800 milioni kila mwezi, CDM zaidi ya 200 milioni kila mwezi, CUF zaidi ya 117 milioni kila mwezi

haya mabilioni yanayoungua kila mwezi yanatakiwa yakanunue dawa, yajenge barabara, yakanunue vifaa hospitalini

VYAMA VYA SIASA VISIPEWE RUZUKU!
 
RUZUKU Hapana, Pinga Ruzuku kwa vyama vya siasa, Pinga Ruzuku! Wawe na sera nzuri, wananchi wataovutiwa na sera zao watawachangia, sipendezewi hata kidogo na tabia ya CCM kukumbatia mafisadi lakini sina namna ya kukataa kodi yangu isiende CCM kupitia ruzuku, hawa Jamaa wanachukua zaidi mil 800 kwa mwezi!!!
 
amesema vyama vya upinzani tu; CCM iendelee kuenjoy ruzuku yake ya bilioni 2 na ushee kwa mwezi. So, kina Zitto naona kwa mpango huu mmekwisha! LOL

Ni hatari sana kwa mwandishi wa habari kupindisha maneno; Mwanakijiji unajua kalamu ni hatari kuliko AK47? Hebu rudia kuisoma tena habari nzima na onyesha wapi Waberoya CCM iendelee kupewa ruzuku. Ama huu ni mwanzo wa Chadema kujiingiza kwenye siasa za ulaghai? Kumbuka wewe ni kiongozi halafu ni mwandishi.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
how i wish tungeacha kujadili mtu/watu

Kila mwezi CCM wanakunja zaidi ya 800M, CHADEMA zaidi ya 200M na CUF zaidi ya 117M, haya ni makosa, hizi pesa zinatakiwa zikanunue madawa na vifaa hospitalini, zinatakiwa zikalipe walimu, zinatakiwa zikalipe madaktari, zinatakiwa zikajenge vyoo shule za msingi, hapa tumeplan vibaya!!
 
Sijawahi kubadilika kuhusu hii hoja, kama vyama vina wanachama basi wanachama wake ndio wakitunze chama na viongozi wao na si kodi zetu!!

zaidi ya billioni moja kwenda kwa wanasiasa na kulisha matumbo yao si haki!! is unfair

tuna priorities nyingi mno na kibaya sisi ni maskini tunaongoza kidunia!!

Please unga mkono hili: RUZUKU KWA VYAMA VYA SIASA ZIKOMESHWE!
 
zaidi ya billioni moja kwenda kwa wanasiasa na kulisha matumbo yao si haki!! is unfair = well said, naomba mods mu-sticky huu uzi, don't let this movement die, RUZUKU KWA VYAMA VYA SIASA HAPANA!
 
Wanajamvi,

Nimetafakari sana matumizi mabaya yanayofanywa na serikali yetu kuvilipa vyama vya siasa kama Ruzuku.

walimu waliomba waboreshewe mishahara wakaambulia vitisho.

Madaktari wakagoma wakafukuzwa kazi,wakatekwa wakafanyiwa UNYAMA na kutupwa MAGWEPANDE, Magazeti yakaandika yakafungiwa kifungo cha maisha na Wahariri kumwagiwa TINDIKALI na KUNG'OLEWA MACHO.

CCM ...........TSH.800,000,000/-@MONTH

CDM.......TSH.200,000,000/-@MONTH

CUF................

NCCR-M............

UDP.............

TLP............

Shule nyingi hazina madawati,zingine mpaka ubao hazina na zingine hazina majengo kabisa.Eneo la shule lipo ila majengo ni ya NYASI.

Hosptalini na vituo vyo afya vya serikali hakuna dawa wala magari ya wagonjwa.

Sasa katika mazingira kama hayo kuna haja kweli vyama vyetu vya siasa kupewa fedha hizo zote wakati shuleni na hosipitalini pako hoi kiasi hicho?

Huu ni UZALENDO kweli?

Hebu serikali imwogope Mungu iwajali watu wake.Ivifutie vyama vyote RUZUKU na ielekeze fedha hizo kwenye huduma za jamii.

Sehemu zingine wakina mama wanatumia masaa zaidi ya sita wanatafuta MAJI wakati serikali inataka kutumia mabilioni kasafirisha gesi ghafi kutoka Mtwara hadi Bwagamoyo.

Kuna mambo mengi sana yanakwenda ndivyo sivyo kwa leo niishie hapo.Tafakari
 
Jiulize na wee pia
1. Je kuna umhimu wa rais kwenda nje ya nchi kuomba wawekazaji na misaada wakti nauli na posho za msafara mzima inazidi million 300. alaf msaada anaopewa kutoka uko ni vitabu ukipiga sana dhamani yake ni labda zaidi million 100!!!! ( unapoteza 300 direct unarudishiwa 100 indirect alaf unakenua meno kabisa)

2. Kwa swali lako je ni mhimu wewe kulipwa msharaha!!!
 
Wana JF Wenzangu!

Nimefuatilia sakata hili lililoanzishwa na Mh. Zitto juu ya ukaguzi wa Mahesabu ya Matumizi ya Fedha za Ruzuku kwa vyama vya siasa huku vikitajwa sana CHADEMA na CCM. Naomba mwenye ufahamu wa kutosha aweze kunipa ufafanuzi juu ya fedha hizi na vitu muhimu ninavyohitaji kujua ni kama ifuatavyo

1.Nafahamu fika fedha za Ruzuku(Umma) zinazotolewa na Serikali huwa lazima ziwe zimeandaliwa Mpango juu ya matumizi yake(yaani ziwe planned) na ndivyo inavyofanyika katika Halmashauri zote nchini.
Swali langu linakuja je hizi fedha za Ruzuku wanazopewa vyama vya siasa zina mpango wowote ulioandaliwa juu ya matumizi ya fedha hizo?

2.Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa fedha za Serikali(CAG) ufanya ukaguzi katika Taasisi kwa kuangalia kama fedha zimetumika kulingana na mpango unavyoonyesha na lengo ni kujua kama zimetumika sawa sawa au tofauti na lengo husika.
Swali langu ni kuwa kama hakuna mpango unaoonyesha fedha hizo zitumikeje Mkaguzi utumia vigezo gani kuhakikisha hizo fedha zimetumika kama inavyopaswa?

Nayauliza haya kwa kuwa inawezekana kabisa lawama tukazirudisha kwa Serikali kwani inawezekana kabisa hakuna plan yeyote au muongozo unaoonyesha hizi fedha zitumike vipi ndio maana utakuta zinafanya mambo tofauti kabisa na kinachobakia ni wanachama kupiga kelele huku kukiwa hakuna sehemu yeyoye itakayoweza kumbana mtumiaji kwani atakachokifanya ni kutunza kumbukumbu tu.

Mwenye muongozo au ufahamu wa kutosha juu ya hoja yangu naomba nisaidiwe.

Asanteni.
 
Saga la Ruzuku kwa vyama vya siasa nchini mwetu litakwisha salama kwa upande mmoja na kuangamiza upande mmoja kati ya chama dola na wapinzani.Hili ni suala very technical,hata chama tawala enzi hizo nchini Ujerumani kilikumbwa na saga la matumizi mabaya ya Ruzuku na hatimaye kilifutwa kwenye ramani ya vyama vya siasa ujerumani.Je,ccm kitafuata mkondo au wapinzani?Ni jambo kubwa na busara kwa ccm kujiandaa kisaikolojia maana bomu kubwa laja,si kuropoka tu
 
Nakuunga mkono mkuu, CCM haitasalimika hata kidogo, ukijumlisha na katiba ndo basi tena.
 
Mnapa homa bure subirini kule kinondoni kuna mtaalamu wa pesa tuliletewa jina lake juzi hapa jukwaani jibu litapatikana tu tusihofu
 
Saga la Ruzuku kwa vyama vya siasa nchini mwetu litakwisha salama kwa upande mmoja na kuangamiza upande mmoja kati ya chama dola na wapinzani.Hili ni suala very technical,hata chama tawala enzi hizo nchini Ujerumani kilikumbwa na saga la matumizi mabaya ya Ruzuku na hatimaye kilifutwa kwenye ramani ya vyama vya siasa ujerumani.Je,ccm kitafuata mkondo au wapinzani?Ni jambo kubwa na busara kwa ccm kujiandaa kisaikolojia maana bomu kubwa laja,si kuropoka tu

Nakuunga mkono mkuu, CCM haitasalimika hata kidogo, ukijumlisha na katiba ndo basi tena.

Kama sheria zitasimamiwa ipasavyo tutaimba buriani ccm,(msajili?)

Nafikiri kuna kitu muhimu nahitaji kujua kama nilivyouliza lakini sijajibiwa, je tuliochangia hatujui jibu la swali langu?
 
Kutokana na matumizi mabaya ya kodi za wananchi napendekeza ruzuku kwa vyama vya siasa zifutwe.

Malengo yaliyowekwa awali kwa kutoa ruzuku kwa vyama vya siasa ikiwa ni pamoja na kuboresha na kukuza demkorasia nchini kwa kuvipa vyama vya siasa uwezo zaidi kuwafikia wanachi, vyama vya siasa vikiwa kama viunganishi vya serikali na wananchi matumizi mabaya ya ruzuku kwa mambo binafsi na usiri mwingi wa matumizi yake hasa katika vyama vichanga vinapelekea kutokea kwa madai kama haya ya kufuta ruzuku kwa vyama vya siasa.

Vyama vya siasa vikianza kujitegemea kwa kutafuta vyanzo vya mapato kujiendesha vitakua na dhana ya dhati kutoa huduma ya demokrasia ya kweli kwa wananchi badala kubweteka na kutegemea ruzuku zitokanazo na kodi za wananchi.
 
Wakumbushe ccm vile viwanja vya uma pamoja na majengo yoote waliyopora tanu wakajimilikisha wayarudishe serikalini hizo nazo hujma kwa vile yalijengwa wakati kulikuwa na chama kimoja
 
Wakumbushe ccm vile viwanja vya uma pamoja na majengo yoote waliyopora tanu wakajimilikisha wayarudishe serikalini hizo nazo hujma kwa vile yalijengwa wakati kulikuwa na chama kimoja

Topic: MBOWE: Chadema hatutaki Ruzuku kwani ni utumwa kwa vyama vya siasa nchini

Habari wa JF! Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni mhe. Kamanda Freeman Mbowe ameweka bayana msimamo mpya wa chama chake Chadema kwamba hawatatumia ruzuku ya serkali ktk kuendesha na kujenga chama kuanzia na uchaguzi wa arumeru, Mbowe amesema kwamba ruzuku ni utumwa wa vyama vya siasa nchini kwahiyo amesema kwa kuwa CDM ni chama cha watu basi kitajengwa na watu kwa kuchangiwa michango na watu pasipo kutegemea ruzuku ya serikali" source star tv na watu wote walokuwepo arumeru leo na mimi mwenyewe"​
 
Back
Top Bottom