Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,402
Watuhumiwa hao, Wanne kutoka Mkoani Njombe na wanne kutoka mkoani Ruvuma Wanashikiliwa na Polisi Wilayani Namtumbo kwa kufanya ramli chonganishi na kutaka kumtoa kafara mtoto mdogo
Walikamatwa katika Mlima Mgwijima wakiwa na mtoto mdogo pamoja na vifaa mbalimbali vinavyodaiwa kutumika katika kafara wakiwemo Mbuzi mmoja mweusi, kuku wawili(mmoja mweusi na mwingine mweupe)
Inadaiwa Polisi baada ya kupata taarifa za kiintelijensia walifika katika mlima huo na kuwakamata Watuhumiwa hao ikiwa ni pamoja na Mganga wa Kienyeji, lakini baada ya mahojiano wamekana madai hayo
Awali, mmoja wa Watuhumiwa, Mwanamke ambaye yupo na mtoto huyo akiwa ametokea Njombe, mara tu baada ya kufika Kituo cha Polisi 'alipandisha mashetani' na kuanza kujigaragaza akisema wale wengine hawana makosa ila yeye
Baadaye alipotulia na kuhojiwa alikana madai hayo na kidai kuwa yeye ni mgonjwa, hivyo alioteshwa kutoka Njombe kwenda kwenye mlima huo ili kupona. Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo