Ruvuma, Tunduru: Daraja la Muhuwesi lajaa maji. Barabaraba yafungwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
TAHADHARI KWA MAGARI YANAYOSAFIRI KUJA AU KUTOKA TUNDURU KUPITIA DARAJA LA MUHUWESI.

Pamoja na simu nyingi ambazo mmepiga wenzetu wa vyombo vya habari na nyingine nimezijibu kwa kifupi mna na wanisamehe wale ambao nimeshindwa kuwapa ushirikiano, leo ilikuwa siku ngumu kikazi, vikao na mambo mengi mno.

Pamoja na hayo nitumie fursa hii rasmi kuwataka wananchi wote wanaosafiri kwa magari binafsi au ya abiria au ya mizigo ambao aidha wanatoka Masasi na Nanyumbu kuja Tunduru au wanaotoka Songea, Namtumbo na Tunduru kuelekea Masasi - kwamba wasimame kabla ya kuifikia kata ya Muhuwesi na hasa mto Mhuwesi wenyewe

Kwa uchambuzi wa hadi muda huu wa saa 3.30 usiku maji ni mengi na yamefunika kabisa daraja na kwa hiyo imetupasa kufunga barabara husika na vyombo mbalimbali vya ulinzi + taasisi zinazohusika na barabara ikiwemo TANROAD viko SITE kuangalia hali ya mambo.

Maji yakishapungua wahandisi wa TARURA na mamlaka zingine za kiusalama zitatoa ushauri ambao tunategemea utapelekea barabara iendelee kupitika.

Kwa wanaotokea Dar, Mtwara na Lindi mnashauriwa kulala Nakapanya, zipo nyumba za kulala wageni.

Kwa wanaotokea Mkoa wa Ruvuma kwenda mikoa ya jirani kupitia Tunduru wanashauriwa kulala Tunduru Mjini.

Poleni kwa usumbufu uliojitokeza ambao uko nje ya uwezo wetu.

Julius S. Mtatiro,
DC Tunduru,
14 Feb 2022.
IMG-20220214-WA0015.jpg
IMG-20220214-WA0016.jpg


======

UPDATES

=======

HALI YA DARAJA LA MUHUWESI SAA 2.00 ASUBUHI YA LEO TAREHE 15 FEB 2022

Baada ya maji kushuka na kuanza kupita chini ya daraja na wahandishi kukagua juu na chini ya daraja na kufanya uchambuzi wa uharibifu uliotokea, kitaalamu na kwa kuzingatia hali halisi ya watu waliokwama pande zote mbili tumeamua kuruhusu magari yapite daraja la Muhuwesi lakini kwa uraratibu maalum wa kupita gari moja na kupita katikati ya daraja tu.

Tumefanikiwa kuvusha magari yote yaliyokuwa yamekwama pande zote mbili za daraja na hata yaliyofika asubuhi ya leo.

Kazi inayoendelea kwa sasa ni kuwasubiri wahandisi wa wizara wafike kuungana na wa mkoa na wilaya ili kwa pamoja waamue aina ya marekebisho makubwa yanayohitajika.

Abiria au mwananchi asiyehitaji usumbufu anashauriwa kupanga na kuamua safari yake vizuri kabla ya kufikia hatua ya kupita upande wetu huu na anayejaribu kuja huku akifika upande wa daraja asijaribu kuvuka bila maelekezo.

Tusisahau kuwa mvua zinaendelea kunyesha mikoa ya Kaskazini na Mashariki mwa Tunduru na kwa hiyo huenda hali hii ya maji kufurika ikajirudia.

Poleni sana na ni muda wa walau kusaka usingizi.

"Muhuwesi Bridge Updates as of 0815 hrs (saa 1.15 asubuhi).

From @julius_mtatiro
DC Tunduru,
Jnne, 15 Feb 2022.
 
Hatari sana hii barabara nimepita mara kadhaa wakati wa mvua sijawahi kuona hali hii
 
Back
Top Bottom