Ruvuma: Mwalimu wa shule ya sekondari afariki kwa kunywa gongo bila kula

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
MWALIMU wa Shule ya Sekondari ya Matemanga wilayani Tunduru, Hekima Gregory, maarufu kwa jina la Mvomela (49), amefariki dunia baada ya kunywa pombe ya kienyeji aina ya gongo.

Wakati mwalimu huyo alipoteza maisha, watu watatu wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na lita 3.5 za pombe hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Marwa, alisema jana kuwa tukio la kwanza lilitokea Juni 5, mwaka huu, majira ya saa 3:00 asubuhi.

Alisema taarifa juu ya tukio hilo, ilitolewa kwenye kituo cha polisi cha Matemanga kutoka kwa Mratibu Elimu Kata ya Matemanga, Rashidi Nasoro.

Marwa alisema katika taarifa hiyo Nasoro alieleza kuwa mwalimu Gregory alikutwa akiwa anakunywa pombe aina ya gongo na inadaiwa kuwa alikuwa hajapata chakula.

Alieleza zaidi kuwa baada ya kumkuta mwalimu huyo akiwa chakari, hatua ya kwanza ilichukuliwa kwa kumpeleka katika hospitali ya misheni ya Kiuma ambako alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu.

Kwa mujibu wa Kamanda Marwa, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo ukisubiri kuchukuliwa na ndugu zake.

Alisisitiza kuwa katika historia yake inadaiwa kuwa inaonyesha ilikuwa kawaida yake kunywa pombe hiyo kwa kuzidisha bila kupata chakula cha kutosha licha ya kuonywa mara kwa mara na viongozi wake.
 
Mwalimu amefia kazini akithibitisha usemi kuwa 'POMBE SIO CHAI'

RIP mwalimu na pole kwa wafiwa
 
unaweza kuta hy gongo amenunua kwa buku akati chakula pia kinauzwa buku.
 
Hii gongo alipewa ofa au alinunua mwenyewe? Tatizo la walezi wanazungusha round tu, mwambie akununulie msosi usikia matusi yake,
 
Naona iwe kosa la jinai kumnunulia mtu pombekali bila kitimoto,
 
Vyuma vimekaza pesa ya kula hakuna na kinywaji anakitaka akaamua kinywaji kwanza sasa imekula kwake. Kupanga ni kuchagua.

Back
Top Bottom