Ruvuma: Kiongozi wa Mbio za Mwenge amuweka Mahabusu Meneja wa TARURA Madaba

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,658
22,255
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru ametumia mamlaka yake ya kikatiba! Meneja wa TARURA huko Madaba awekwe mahabusu!
Karibuni wataalamu wa katiba na sheria.
Chanzo: Taarifa ya Habari Radio One Jumapili 22 09 2019 13:05hrs.

=====

Meneja awekwa mahabusu kwa kudanganya viongozi wa mbio za Mwenge

askari.jpg

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru mwaka 2019 Bw.Mzee Mkongea Ally amemuweka mahabu meneja wa wakala wa bara bara za vijijni na mjini wa halmashauri ya wilaya ya Madaba Bw. Razaro Kitomari baada ya kudanganya kuhusu mradi barabara huku akikataa kuweka jiwe la msingi kwenye mradi huo na mradi wa jengo la ofisi ya halmashauri ya Madaba kutokana na kutokidhi vigezo.

Mradi mwingine uliokataliwa kuwekewa jiwe la msingi na Mwenge wa uhuru ni mradi wa jengo la ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Madaba kutokana na kushindwa kukidhi vigezo ambapo vielelezo vya mradi huo amekabidhiwa afisa wa taasisi ya kupambana na rushwa TAKUKURU kwa ufuatiliaji zaidi.

Hata hivyo Mwenge wa uhuru umezindua mradi wa maji katika kijiji cha Lilondo na mradi wa darasa katika shule ya msingi Kibrang’oma.
 
katiba haina mtaalamu wa kusema anajua kila kitu. utaalamu kwenye katiba unakuja mahali ulipo na eneo hilo linagusa katiba.

Inawezekana ni kweli ana hayo mamlaka.
 
Lakini kama umewahi kuhudhuria mbio za mwenye yule kiongozi huwa anamuwakilisha rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania hivyo nadhani sina uhakika ana uwezo wa kumuweka yeyote ndani japo sijui ni kwa muda gani.
 
Kwa kosa gani sasa
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru ametumia mamlaka yake ya kikatiba! Meneja wa TARURA huko Madaba awekwe mahabusu!
Karibuni wataalamu wa katiba na sheria.
Chanzo: Taarifa ya Habari Radio One Jumapili 22 09 2019 13:05hrs.
 
Kiongozi wa kukimbiza mwenge ana mamlaka hayo kweli? Aisee, hapa kazi tu! Kajamaa kanajipa madaraka makubwa mno!
 
Kumbe hiki cheo kina jurisdiction kubwa kiasi hichi? Mmmhhh na mshahara wake unasomaje?

Au huyo kiongozi wa mwenge ana cheo kingine? Mfano Dc hivi...kwahiyo hapo ni anatumia mamlaka ya uDC na siyo ya mbio za mwenge.
 
Kiongozi wa mwenge ana uwezo wa kuamuru hata DC awekwe ndani.

Haijaandikwa popote kama vile katiba ya uingereza
Kumbe hiki cheo kina jurisdiction kubwa kiasi hichi? Mmmhhh na mshahara wake unasomaje?

Au huyo kiongozi wa mwenge ana cheo kingine? Mfano Dc hivi...kwahiyo hapo ni anatumia mamlaka ya uDC na siyo ya mbio za mwenge.
 
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru ametumia mamlaka yake ya kikatiba! Meneja wa TARURA huko Madaba awekwe mahabusu!
Karibuni wataalamu wa katiba na sheria.
Chanzo: Taarifa ya Habari Radio One Jumapili 22 09 2019 13:05hrs.

=====

Meneja awekwa mahabusu kwa kudanganya viongozi wa mbio za Mwenge

askari.jpg

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru mwaka 2019 Bw.Mzee Mkongea Ally amemuweka mahabu meneja wa wakala wa bara bara za vijijni na mjini wa halmashauri ya wilaya ya Madaba Bw. Razaro Kitomari baada ya kudanganya kuhusu mradi barabara huku akikataa kuweka jiwe la msingi kwenye mradi huo na mradi wa jengo la ofisi ya halmashauri ya Madaba kutokana na kutokidhi vigezo.

Mradi mwingine uliokataliwa kuwekewa jiwe la msingi na Mwenge wa uhuru ni mradi wa jengo la ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Madaba kutokana na kushindwa kukidhi vigezo ambapo vielelezo vya mradi huo amekabidhiwa afisa wa taasisi ya kupambana na rushwa TAKUKURU kwa ufuatiliaji zaidi.
Hata hivyo Mwenge wa uhuru umezindua mradi wa maji katika kijiji cha Lilondo na mradi wa darasa katika shule ya msingi Kibrang’oma.

Kama kafuata utaratibu, na alichokiaribu kinahusiana na mali ya uma, nampongeza.

Kuna watu walikuwa hawachukui mishahara yao,, kwa vile rushwa na misuse of public fund zilikuwa zinawatosha.
 
katiba haina mtaalamu wa kusema anajua kila kitu. utaalamu kwenye katiba unakuja mahali ulipo na eneo hilo linagusa katiba.
Inawezekana ni kweli ana hayo mamlaka.
Huyu si mwajiriwa wa serikali ni mwanaccm aliyechaguliwa kukimbiza mwenge akiufikisha mwisho kibarua kinaishia hapo, ni vipi anaweza kuamuru mtumishi wa serikali afungwe?
 
Back
Top Bottom