Ruvuma: Christopha Njako, Tajiri wa mahindi akamatwa kwa utakatishaji fedha

Mara ya kwanza alikuwa anawalipa wakulima vizuri tu na hivyo serikali haikuwa na shida nae na akapewa ulinzi.
Baadae kidogo akaanza kuwakopa wakulima, wakulima hawakulipwa na wakaandamana. Hivyo serikali ikaingilia kati kuwanusuru wakulima
Mwisho ndio ikagundulika anatakatisha pesa
Style ya biashara yake ilikuwa lazima siku atakwama tu

Ova
 
Utakatishaji ni kitendo cha kuchukua fedha isiyo ya halali (wizi, utapeli, n.k) kwenda kuizungusha katika miradi iliyo ya halali...apo unakuwa unaisafisha ile hela ya haramu ionekane ni ya halali...

Ukiangalia hapo huyo jamaa amewatapeli wakulima na kisha ile hela akaenda kuipeleka katika miradi yake kama hotel nk hivo ameitakasa hela ya haramu kuonekana ya halali.

Sent from my iPhone 12 Pro using JamiiForums mobile app
Jamaa amewatapelije hao wakulima? mbona nilisikia bado anawalipa.

Hata kama aliacha...huo muda aliokuwepo akifanya hiyo biashara atakuwa ameshakula hasara kiasi gani??imesharudi?
 
Kazingua Kivip?kwani kuna watu wamelizwa?
Aliwaingiza kwenye aka wamaliza hakuna pesa ya bure
images(7).png
 
Picha ya mtuhumiwa tafadhalo. Maana huyu jamaa ni kama niliwahi muona mahali miama michache huko nyumba. Nikishathibitisha picha yake naweza mfahamu.
 
Ufafanuzi pliz,, anatakatishaje hizo fedha ?
Pesa za utapeli unapoenda kununulia mashamba, magari, na kujenga nyumba ndio kuzitakatisha maana unaziingiza katika mfumo wa mali ambazo unaweza ukaziuza na ukaingiziwa malipo benki na zikapokelewa kwenye akaunti yako kama pesa safi na halali za mauzo halali ya kiwanja, nyumba au gari lako. Na hapo unakua umetakasa pesa chafu. Umeelewa au nirudie?
 
Kuchelewa kuishtukia Ile picha ilikuwa ni matumizi mabaya kabisa ya ubongo, na ndio tatizo letu kubwa blacks!

Jamaa ananunua mahindi kwa shilingi 72000 taslim anauza kwa sh 42000 pesa ya Tanzania, Kuna biashara hapo? Kuna tofauti gani na deci amabyo watu walikuwa wakipanda mbegu za pesa wakitegemea zitaota pesa mtoto na kukuwa ?

Wengi nahisi watakuwa wamelizwa maana hawakujiuliza logic ya Ile biashara
Mitelemko ganda la ndizi kunapunguza kufikiri kwa kina kifupi ilikuwa ni michezo ya kitoto kwa watu wazima nao wakakubali kucheza.
 
Huyu mwamba ni noma, zaidi ya wakulima 1200 wametapeliwa, jumla ya kiasi cha 1.3bil . Msemo wa jiwe tz ni tajiri
 
Kwa hiyo ukipata hasara hiyo ni biiashara.

Ndio maana biashara ina pande ya faida na hasara.

Biashara ni kuuza na kununua.

Biashara inafaida na hasara.
Kupata hasara ni ajali na kamwe si lengo. Hasara haipaswi kuwa sehemu ya biashara.
 
Pesa za utapeli unapoenda kununulia mashamba, magari, na kujenga nyumba ndio kuzitakatisha maana unaziingiza katika mfumo wa mali ambazo unaweza ukaziuza na ukaingiziwa malipo benki na zikapokelewa kwenye akaunti yako kama pesa safi na halali za mauzo halali ya kiwanja, nyumba au gari lako. Na hapo unakua umetakasa pesa chafu. Umeelewa au nirudie?
umeeleweka mkuu!,, asante kwa ufafanuzi
 
Back
Top Bottom