Rutyfiya Abubakary 'Amber Ruty' na Said Bakary Mtopali wamerejea uraiani baada ya kupata dhamana

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
20,079
2,000
Mchungaji Daud Mashimo wamewadhamini msanii Amber Rutty na mpenzi wake Said Bakary, katika Mahakama ya Hakimu Makazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Wawili hao walikuwa wanashikiliwa kwa kusambaza kwa video yenye maudhui ya ngono.

======

Dar es Salaam. Hatimaye mshtakiwa Rutyfiya Abubakary 'Amber Ruty' na Said Bakary Mtopali wamerejea uraiani baada ya kupata dhamana leo Jumanne Novemba 27, 2018.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka manne likiwemo la kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Wawili hao walifikishwa kwa mara ya kwanza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba 2, 2018 kujibu mashtaka hayo, lakini walishindwa kupata watu wa kuwadhamini jambo lililowafanya waendelee kusota rumande kwa siku 25.

Washtakiwa hao jana Jumatatu walishindwa kutimiza masharti ya dhamana wakati kesi yao ilipokuja kwa ajili ya kutajwa lakini leo walipoletwa tena mahakamani hapo mambo yamekuwa mazuri.

Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile kuwa washtakiwa hao wameletwa kwa ajili ya kupatiwa dhamana kwa kuwa wadhamini wao wamekamilisha masharti ya dhamana.

Baada ya kueleza hayo, waliitwa wadhamini wa Amber ambao ni Salma Omary (46) mkazi wa Mabibo na Asha Seif (46) mkazi wa Mtoni Mtongani ambao wote ni mama zake wadogo na mshtakiwa huyo.

Mtopali yeye amedhaminiwa na Daud Mashimo (32), mchungaji wa Mitume na Maaskofu Tanzania wa Kanisa la Emmaus Bible Church Pentecostal lenye makao yake Mbezi Luis, jijini Dar es Salaam na Francis George (30) mkazi wa Mwananyamala kwa Kopa.

Wadhamini hao waliwasilisha vitambulisho vya Taifa mahakamani hapo na kusaini bondi ya Sh15 milioni.

Hakimu Rwezile ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 10, 2018 itakapotajwa tena.

Mbali na Amber Rutty na Mtopali mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo James Charles maarufu ‘James Delicious’ tayari yupo nje kwa dhamana.

Katika kosa la kwanza la kufanya mapenzi kinyume na maumbile ambalo linamkabili Amber Rutty, anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Oktoba 25, 2018 ambapo alimruhusu Mtopali kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.

Katika shtaka la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linalomkabili Mtopali anadaiwa kati ama baada ya Oktoba 25, 2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Rutty kinyume na maumbile.

Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, linalomkabili James Charles ama James Delicious inadaiwa kati ya Oktoba 25, 2018, Charles alisambaza video za ngono kupitia makundi ya WhatsApp.

Kosa la nne ambalo ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Rutty na Mtopali wakidaiwa kati Oktoba 25, 2018 walisambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp, jambo ambalo walilikana.

Chanzo: Mwananchi
1543322555824.png

1543322258524.png

1543322275863.png
 

kashesho

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
4,982
2,000
Duh kumbe bado walikuwa selo?watakuwa wamejifunza kama sio kukoma kabisa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom