Kenya 2022 Ruto amestaafisha siasa Familia 3, Kenyatta, Moi na Odinga Family

Kenya 2022 General Election

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,486
8,706
William Ruto, ushindi wake una mambo mengi sana na kubwa kuliko yote ni kuwastafisha siasa Moi Family Odinga Famiily na Kenyata Fammily.

Endapo Odinga angeshinda alitaka afufue tena BBI ili katiba ibadilishwe na watengeneze vyeo vipya na Uhuru alitaka kumtumia Odinga kufanya yale mambo ya Putin, kwamba kuna wakati Putin aliachia Urais akawa Waziri Mkuu na baadae tena karudi na hio ndo ilikuwa plan ya Uhuru Kenyatta, na Ruto hapo ndio alishituka na Ugomvi wao wote uko hapo kwenye hizo plan za Uhuru Kenyatta

Kwa Umri wa Odinga uwezekano ulikuwa ni kuongoza Miaka mitano tu kwa sababu ya Umri umemtupa sana mzee na hapo ndio Uhuru alitaka baada ya miaka Mitano arudi tena kuja kuwa Rais au kuwa Powerfull Prime minister.

Kwa Moi Family, baada ya Gideon Moi kushindwa kiti cha Useneta maana yake ndio mwisho wa Gidioni Moi na Moi family kwa sababu Gidion ndo kabeba fimbo ya Moi, kuna ndugu yake mwingine ila yule hana jina kabisa, Moi family imefikua mwisho.

Ruto atakumbukwa kwa Kuwastafisha Siasa Familia tatu zilizotawala siasa za Kenya Vizazi na Vizazi.

Hutarajii tena kumsikia Odinga kwenye active politics, the same na Uhuru Kenyatta.

Hapa Tanzania kuna Famiily zinaji-Group na sisi tunawachekea tu na kuwalamba miguu. Kikwete Family, Pinda Family, Mwinyi Family, Makamba Family na Lowassa Family.

Hawa wana ambition za mbali saba na kubwa sana wanataka kutumia majina ya Wazazi wao kufika mbali sana, Uhuru Kenyata alianzia mbali sana usimuone hivyo.

Tukiendelea kuchekea hizi familia moja wapo itatutawala muda si mrefu sana.

Mama anachofanya sasa nu kuwapa Exposure zaidi kuwajengea uwezo waje watawale sisi wajinga. Ridhiwan Kikwete ana target mbali sana, the same na Makamba, angalau Mwinyi kaisha kamata Zenji, Hussein Mwinyi amepewa semina kuanzia utawala wa Mkapa, Kikwete na Magufuli.

Hizi Familia si kwamba zina uniqueness, niambie Ridhiwan ana kipi special? Makamba ana kipi? Yule Mtoto wa Pinda ana kipi?
 
Mtoa mada ni mropokaji na mchochezi...kwanza matokeo ya uchaguzi bado,pili mtoa mada una roho ya kichawi kwani nani alimzuia baba yako kuwa na bidii ili nae awe rais? hao uliowataja hapo ni uchochezi
Duh una hasira

Ova
 
Mtoa mada ni mropokaji na mchochezi...kwanza matokeo ya uchaguzi bado,pili mtoa mada una roho ya kichawi kwani nani alimzuia baba yako kuwa na bidii ili nae awe rais? hao uliowataja hapo ni uchochezi
Kenya sio CCM na hata Chebukati yule Bosu wa tume alisha waambia Wajenya ingibe kwenye portal ya tume jumlisheni ila mwenye mamlaka ya kutangaza mshindi nu tume
 
Mada kama hizi ndio zinawaponza wakenya mpaka wananyukana. Sasa hapo Ruto asipotangazwa mshindi sio ndio wanaloanzisha la kimbari
 
Back
Top Bottom