Russian Ambassador to Turkey Andrei Karlov shot dead in Ankara

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,842


Wizara ya Mambo ya Nje imethibitisha kuwa Balozi wa Urusi, Andrey Karlov amefariki dunia baada ya kushambuliwa kwa risasi mjini Ankara, Turkey.


Hatari sana, ngoja tumsikie Rais wa Russia, Vladimir Putin atatoa tamko gani. Tayari wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi kupitia msemaji wake Maria Zakharova imesema tukio hili ni la kigaidi na pia Marekani kupitia msemaji wake John Kirby na mataifa mengine kadhaa tayari wamelaani tukio hilo la leo.

Mtu aliyemshambulia balozi , alikuwa amevaa suti na tai akiwa na muonekano wa ''kama bodyguard'' huku akipaza sauti kwa lugha ya ki-Russia na pia maneno " Aleppo-Syria ", '' Allahu Akbar'' ! alipigwa risasi na polisi mita michache toka eneo la tukio. Katika shambulio hilo wakati wa maonesho ya picha, watu wengine watatu walijeruhiwa na muuaji wa Balozi Andrey Karlov. Pia mshambulizi huyo kwa lengo maalum alivyatulia risasi picha kadhaa na kuziharibu, hii inasemekana ktk kuonyesha ujumbe Fulani dhini ya picha hizo.

Maonesho ya picha aliyohudhuria balozi Andrey Karlov yalikuwa na lengo la kuimarisha ushirikiano wa nchi mbili za Russia na Turkey. Maudhui ya maonesho hayo yalikuwa kusaidia ''kufahamiana'' zaidi kati ya Russia na Turkey kutokana na mlolongo wa matukio yaliyotia doa ushirikiano ikiwemo tukio la kutunguliwa kwa ndege ya Urusi na majeshi ya Uturuki November mwaka 2015.

Kwa mujibu wa RT (Russian Television) News habari ambazo hazijathibitishwa, Muuaji ametambuliwa kuwa ni ofisa wa Polisi wa Uturuki aliyezaliwa mwaka 1994 na kuhitimu elimu kiwango cha diploma na kujiunga na idara ya Polisi mwaka 2014 na baadaye kutimuliwa kazi mwaka 2016 baada ya mapinduzi ya Turkey kumuangusha Rais Recep Tayyip Erdoğan kufeli mapema mwezi Julai mwaka huu (2016).

Eneo lilipotokea tukio la kigaidi jijini Ankara, Uturuki ni karibu na majengo ya ubalozi ya mataifa ya Marekani, Uingereza n.k ambapo huwa kuna ulinzi mkali kutokana na majengo mengi nyeti.

Balozi Andrey Karlov mbobezi wa kidiplomasia kwa miaka 40, ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Moscow State Institute of International Economic Relations na Chuo cha Kidiplomasia cha the Diplomatic Academy of the Russian Foreign Ministry aliwahi pia kuwa balozi wa Urusi huko North Korea 2001-2006.

Tayari jumuiya ya wana-Diplomasia Urusi wamesema kuwa tukio hili la leo la mauaji ya Balozi Andrey Karlov ,yaweza kuwa limechochewa sana kihisia na matamko ya miezi mingi iliyopita ya wanasiasa wa nchi za magharibi ktk vyombo vya media na propaganda social media : blogs, twitter, facebook, YouTube juu ya hatua za Urusi huko Aleppo, Syria dhini ya wapiganaji wa Free-Syria na uungwaji mkono wa kijeshi wa Urusi kwa utawala wa Rais Bashar al Assad wa Syria.

Habari za punde kidogo, Rais Vladmir Putin ametoa tamko na kuwa kamati ya uchunguzi tayari imetumwa Turkey kuungana na vyombo vya Turkey katika uchunguzi wa tukio hili. Pia Putin amethibitisha kuzungumza kwa simu na Rais wa Turkey, Recep Tayyip Erdoğan kuhusu tukio hilo na kukubaliana kufanya kazi pamoja kusaidia kufahamu waliopanga mpango huo wa mauaji ya leo.

Rais Putin amempa sifa kemkem marehemu Balozi Andrey Karlov kwa kazi kubwa wakati wa uhai wake ikiwamo kushughulikia tukio nyeti la utunguaji wa ndege ya Urusi uliotekelezwa na majeshi ya Uturuki. Rais Putin amesema weledi wa balozi huyo ulisaidia tukio hilo la kutunguliwa ndege kumalizika salama kidiplomasia. Putin amesema tukio la leo la mauaji ya Balozi Andrey Karlov, halitafanya Urusi kupunguza wajibu wake kuisaidia serikali ya Syria katika vita vyake na makundi mbalimbali nchini Syria.

=======================

A gunman has shot dead Russia's ambassador to Turkey, Andrei Karlov, apparently in protest at Russia's involvement in the Syrian conflict.

Several other people were reportedly also injured in the attack, a day after protests in Turkey over Russia's military intervention in Syria.

The killer, said to be an off-duty Turkish policeman, opened fire at point blank range as Mr Karlov made a speech.
Police later "neutralised" the attacker, Turkish media say.

Mr Karlov was rushed to hospital, reports said, but his death was later confirmed by the Russian foreign ministry.

"Terrorism will not pass! We will fight it resolutely," said ministry spokeswoman Maria Zakharova.

"The memory of this outstanding Russian diplomat, a man who did so much to counter terrorism... will remain in our hearts forever," she said.

US state department spokesman John Kirby said US officials were aware of reports about the attack on the ambassador.

"We condemn this act of violence, whatever its source," he said. "Our thoughts and prayers are with him and his family."

While there were protests in recent days about the situation in Aleppo, on a political level the Turkish and Russian governments have been co-operating in the ceasefire operation, the BBC's Turkey correspondent, Mark Lowen, reports.

Eight shots
According to Russian TV, the ambassador had been attending an exhibition called "Russia as seen by Turks".

Video of the event shows Mr Karlov making a speech when gunshots ring out. Eight bullets are said to have been fired.


Source: Russian ambassador to Turkey shot in Ankara
 
Pole yake... Turkey & Russia wako kwenye tensions sana, tangia wadungue ndege ya Jeshi la Russia, sasa hii ni kali zaidi..

Ambassador apigwa shaba.. duuh..!!
 
Pole yake... Turkey & Russia wako kwenye tensions sana, tangia wadungue ndege ya Jeshi la Russia, sasa hii ni kali zaidi..

Ambassador apigwa shaba.. duuh..!!
Hawapo kwenye tension tayari uturuki washalipa fidia na hivi karibuni tu Putin na rais wa uturuki waliimarisha urafiki,waziri mkuu wa Turkey alikuwa Moscow juzi tu

Inasemwa wakati wa mapinduzi Putin alimpelekea makomandoo Erdogan wamsaidie ,na baada ya kusaidiwa Erdogan akaenda urusi

Itakuwa tukio la kigaidi tu
 
Hawapo kwenye tension tayari uturuki washalipa fidia na hivi karibuni tu Putin na rais wa uturuki waliimarisha urafiki,waziri mkuu wa Turkey alikuwa Moscow juzi tu

Inasemwa wakati wa mapinduzi Putin alimpelekea makomandoo Erdogan wamsaidie ,na baada ya kusaidiwa Erdogan akaenda urusi

Itakuwa tukio la kigaidi tu
Hilo la makomandoo nililipata na matusi nudie aliedukua mawasiliano ya visas maalim vya satellite vilivyokua vikitumika siku ya mapinduzi. Inasemekana kua wanamapinduzi walipishana na helicopter ya makomandoo wa Putin ambayo haikuonekana hata kwenye radar akatereshwa hadi ikulu ankara. Jamaa waliotumwa kwenda kumteka katika ule mji wa pwani wakashtuka wanamuona yuko live anahutubia taifa toka ikulu na kuhimiza wananchi kuingia barabarani kupinga wanamapinduzi
 
ngoja tuskie mwanamume Putin atasemaje. to shoot the ambassador nafkiri ndo uchokozi wa mwisho
Hili tukio limefanywa na magaidi.
Ambassador alikuwa kwenye public event ndipo shooter alipoanza kumimina marisasi ,secret service walikuwa wazembe

Japo atalaumiwa kwa security ila siyo kuzuka kwa vita
 
Russian ambassador to Turkey shot in Ankara

Kuna hali ya hatari nchini Uturuki baada ya balozi wa Urusi nchini Uturuki kupigwa risasi na anaelekea kufa.

Uenda Uturuki ikaingia kwenye mgogoro mkubwa na Urusi na kusababisha vita kati ya nchi hizo.
Sasa ndio watachapwa kama watoto subirini,walishadondosha ndege ya vita ya urusi na rubani kufa wengine waliruka walisamehewa sasa da nnavyojua Russia yetu macho ngoma ya Allepo inahamia uturuki
 
Back
Top Bottom