Russia yasimamisha kwa muda uwekaji mitambo ya makombora barani Ulaya

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Russia yasimamisha kwa muda uwekaji mitambo ya makombora barani Ulaya

Dec 14, 2021 12:26 UTC

[https://media]

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema nchi hiyo imeamua kusimamisha kwa muda mpango wa kuweka mitambo yake ya makombora katika bara la Ulaya.

Sergei Ryabkov amesisitiza kuwa, ikiwa Marekani haitaweka mitambo yake mipya ya makombora barani Ulaya, Russia nayo itaendelea na hatua yake ya upande mmoja ya kusitisha kuweka mitambo ya makombora katika bara hilo.

Ryabkov ameongeza kuwa, muhula wa kisheria wa kuweka mitambo ya makombora ya Russia katika bara la Ulaya umeshatangazwa na Rais wa nchi hiyo Vladimir Putin; na hivi sasa Moscow inangojea jibu la nchi wanachama wa Shirika la kijeshi la NATO.

[https://media]Sergei Ryabkov

Kabla ya hapo, Putin alishaonya kuhusu kuwepo kijeshi nchi wanachama wa NATO nchini Ukraine na hatari itakayosababishwa na hatua hiyo kwa usalama wa taifa wa Russia.

Katika miaka ya karibuni, Marekani na NATO zimekuwa zikitumia kisingizio kwamba Moscow ni tisho kwa Magharibi ili kupanua kuwepo kwao kijeshi karibu na ardhi ya Russia na kwenye maeneo yanayopakana na nchi hiyo.

Uhusiano wa Magharibi na Russia umekuwa wa vuka nikuvute, hata hivyo ulianza kuharibika zaidi mwaka 2014 kufuatia kujiri matukio manne makuu ya kujipenyeza kijeshi shirika la Nato na hasa Marekani karibu na ardhi ya Russia na mashariki ya UIlaya, mgogoro wa Ukraine, kadhia ya Bahari ya Baltiki na hali ya mambo nchini Syria.../
 
Back
Top Bottom