Russia kama Tanzania, sema wenzetu ni MATAJIRI na wanajipendelea wao kwanza. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Russia kama Tanzania, sema wenzetu ni MATAJIRI na wanajipendelea wao kwanza.

Discussion in 'International Forum' started by Sikonge, Jan 13, 2011.

 1. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Baada ya Ukoministi kufa Russia, watu walianza kuchukua chao mapema kwa nguvu sana. Ziliuzwa silaha na kila kinachowezekana. Watu walichukua mikopo serikalini na kununua viwanda na migodi kwa bei chee. Mafia walianza kunyang'anyana mali hizo kwa kukulazimisha kuwa umeuza na ukikataa wanakuulia nduguzo na mwisho wanakumaliza wewe.

  Mafia hawa wengi ni wale walikuwa ndani ya KGB na kwao kuuwa haikuwa shida kabisa ni kama sisi wengine kunywa chai. Kwa maana hiyo, wengi sana waliuawa au kukimbia Russia na milele hawawezi kurudi huko kwani Adui zao wanawasubiri au Serkali inawasubiri. Ninaposema Serikali ina maana inaweza kuwa haohao adui zao kama PUTIN anatumia Serikali kuwarudi adui zake.

  Hawa jamaa kwa UJUMLa unaweza kusema ni wale wote walikuwa kwenye SYSTEM ndani ya Ukoministi. Watu walipouwa Ukoministi, jamaa walikaa pembeni huku wakiwa wameteka hela nyingi sana na wengi wao wakawa wamejiingiza kwenye BIASHARA kubwa sana.

  Kwa Tanzania tumekuwa tukiona viongozi wetu wakiiba na badala ya kuwafundisha watoto wao wawe wafanya biashara na kuwa na viwanda, makampuni yanayofanya kazi hadi nje, mashirika mazito nk, wamekazania kuwaingia watoto wao kwenye SIASA ili wabaki kwenye System bado kuendelea kuiba. Biashara pekee wanaoifanya ni kuwa na vikampuni Uchwara vya Uwakili na hapo wanaanza na wao kurudi Serikali ili wapate deal za kula.

  Kwa hali hii, wenzetu Warusi wametuacha mbali sana kwani tunaona akina Roman Abramovich wa Chelsea FC. Matajiri wa namna hiyo wenye makampuni ya Mafuta, almasi, alminium, magari, ndege, mafuta nk wako wengi sana sana kwa sasa Russia na hasa Moscow. Maduka mengi ya bei mbaya kwa sasa wamehama kutoka Monaco na kwenda Moscow. Hii imefanya mji huu kuwa aghali sana. Nina hamu nije nifike hapo walau kwa siku mbili na kuona matajiri hao.

  Mmoja ya watu waliokuwa kwenye SYSTEM na sasa kawaacha Familia yake wakiishi bila matatizo wala Mikwaruzo ni huyu mzee aitwaye Yevgeny Primakov aliyekuwa zamani Boss wa KGB na mwisho akawa mwanasiasa hadi kufikia kuwa PM wa Russia.
  [​IMG]

  Huyu Mzee, mke wake anaitwa General Tatiana Anodina. Huyu mama ndiye BOSS wa MAK Russia. MAK ni INTERSTATE AVIATION COMMITTEE (IAC) ya Russia. Hii ni kama TAA kwa Tanzania na huyu mama huwa anaruhusu au kuzuia shirika la ndege ku-Oparate Russia.

  Ila kichekesho ni kuwa la Shirika la PILI kubwa la ndege la RUSSIA, ni shirika lililoanzishwa na mtoto wa huyu mama aitwaye Aleksandra Pleszakov. Mama mwenyewe ana asilimia 4% Officially. Kwa sasa kijana amejiweka PEMBENI na kumuweka mkewe aitwaye Olga kuwa ndiyo BOSS wa Kampuni. Shirika hilo waweza ona mapipa yake hapa maana wametuacha mbali sana sisi na Ki-Air Tanzania chetu.
  Transaero Airlines - Wikipedia, the free encyclopedia.

  Hili shirika lilianzishwa wakati Warusi Wayahudi wameanza kuhamia Israel kwa wingi sana. Hata wale wa Ethiopia pia walibebwa kipindi hiki. Kulihitajika ndege nyingi na mashirika yalikuwa hayana uwezo wa kubeba watu wengi namna hiyo. Ndipo Primakov kwa kutumia Connection zake ndani ya KGB (kumbuka ni KGB walikuwa wakisimamia uhamaji wa Warusi/Wayahudi kwenda Israel), walianzisha hilo shirika haraka sana na hapohapo wakawa na Abiria wengi sana na kazi kibao za kufanya.

  Ufisadi wanaofanya kwa sasa sanasana ni KUKWEPA KODI. Sidhani kijana anahitaji tena kuingia serikalini au kwenda Kufisadi mali za TAIFA. Shirika linafanya safari hadi nchi za West Uropean na Canada, Mexico, Africa na Asia.

  Kwa hilo, naona wenzetu wametuzidi maana wanajua kujiweka mbali na siasa za baba zao au niseme baba zao wanawaweka mbali na Siasa. Wanabaki kuwa wafanyabiashara huku wakitoa ajira kwa watu wengi tu na shirika kuwa ni moja ya Kitega uchumi kikubwa sana kwa nchi.

  Nina tegemea na sisi siku moja Viongozi wetu wataanza kufikiria kuwa wanapofisadi, basi hizo hela waziwekeze hapahapa kwetu Tanzania na kuleta AJIRA kwa wananchi na siyo kuzipeleka nje na mwisho wa siku wanabaki kuwalazimisha na watoto wao au niseme kuwaruhusu watoto wao kuingia kwenye SIASA kwa nguvu huku wakijijengea maadui wengi sana kwani siku wakiondoka madarakani, watoto watakuwa na hali mbaya sana.
   
 2. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  tatizo la wanasiasa wetu ni wezi na tabia ya mwizi ni kuwa akiiba leo anatumia chote na kesho anarudi tena kuiba na mbaya zaidi mpaka mtoto mdogo atajua kwamba huyu kiongozi ni mwizi
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Hata Wazungu ni wezi sana. Nigerian nao wanakomba kishenzi. Ila wenzetu wanaiba na kuzifanyia kitu cha maana. Warusi utajiri wao mkubwa uko chini ya mikono yao na siyo kama sisi kila siku kiguu na njia eti kuwatafuta Dowans waje wawekeze kwenye umeme.

  Ningeliwaona wa maana kama wangejiuzia Air Tanzania na kuiendeleza kuwa shirika kubwa sana Africa. Wao wanakula hadi mbegu na hizo pesa wanahonga wanawake vigari vyekundu, too sad.
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,376
  Likes Received: 19,646
  Trophy Points: 280
  urusi kwenye swala la ajira wanajiangalia wao kwanza na hawacheki na nyani, hawa jamaa hawataki kabisa kufanya mistake na wananchi walio wengi wanaishi vizuri hasa wanaoishi mijini ndio maana hutakuja kusikia kuwa watu wameandamana kwa kukosa umeume kwa sababu wanapata kila kitu wanachotaka na % kubwa hawafuatilii siasa hasa vijana , hata siku ya uchaguzi wa rais wengi wao walikuwa hawajui hata jina la mpinzania wala chama cha upinzani . Hii ni kwa sababu viongozo wao Putin n Medvedev wapo makini sana hasa kwenye kuwasaidia wananchi wao hadi kwenye mambo ya emegency . Naweza kusema kuwa jamaa wanakubalika sana kwa wananchi kwa sababu wananchi wanapata huduma zote.
   
 5. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,081
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Mkuu Sikonge, nimefurahishwa sana na post hii.Niliwahi kusoma Russia kipindi fulani.Ni kweli hawa jamaa wametuzidi mbali lakini pia style yao ya utawala na nguvu ya mafia inalimit makampuni(hasa ya ulaya) kuingia Russia. Ni challenge kubwa kwa sasa manake kuna potential market na raia wako willing for a change ila mabadiliko hayo yatachukua muda kwa sababu ya gap la wenye nacho na wasionacho.Tz inaanza kuelekea huko na soon tutaanza kuongozwa na matakwa ya genge la wenye nguvu.(mafia) Au tumeshafika huko! sina uhakika...
   
 6. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,081
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Mkuu issue ya Russia haiko kama unavyofikiria... Putin siyo kwamba anakubalika saaana ila ni kwamba Russia nguvu ya dola, rushwa, na mafia ambao wana influence kubwa on political, economical and other areas wana nguvu sana. Hawa ni maofisa wa zamani wa KGB, Putin mmoja wao sasa all what you can see on media are simply tip of the iceberg.Wananchi walio wengi wanaishi vizuri Russia? Dude that is totally wrong, Warusi wengi wana maisha magumu labda kama unacompare third world countries lakini kwa standard ya developed countries, they are quite below.However kuna matajiri wengi na watu walio kwenye system lakini sio majority.Pia upinzani unaminywa sana Russia. I can go into details how Putin has put in jail the guy who is most powerful as he feared he is supporting oppositions.
   
 7. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  we lack quality to match this
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,376
  Likes Received: 19,646
  Trophy Points: 280
  mkuu mgalanjuka nakubaliana na wewe ila hapa nilikuwa nakompare na nchi kama Tanzania,na ni kweli there is no democracy in Russia na huwezi kuifananisha na democracy ya europe lakini ukija kwenye suala la huduma kwa wananchi hata kidogo you cant compare it with Tanzania ,kwa sababu Urusi in rasilimali nyingi sana na wanaweza kutumia rasilimali zao kisawasa.let say in Moscow huwa umeme haukatikagi hata siku moja mimi niliiishi urusi for 5 year na umeme haukuwahi kukatika hata mara moja ,na wakikata wanaambia 2 days before that umeme hautakuwepo kwa 2 hours, na mara nyingi warusi wanakuwa na bifu na nchi za eurpoe kutokana na rasilimali zao kama gesi, nchi za europe zinaitaka sana gesi ya urusi na urusi analijua hili na mara nyingi wanajitahidi san kumuingiza katika mikataba mibovu ili ajifunge ila urusi huwa anajitoa na kuifunga gesi yake mara kwa mara ..tukija kwa Tanzania hakuna kiongozi hata mmoja anayeweza kutetea rasilimali zetu Mwinyi alimuuzia mwarabu mbuga kwa miaka 99 na nadhani wanaojua hili ni wengi sana ,sasa hapa utu na upendo wa nchi yako unajionyesha kabisa haupo kwa sababu effect nzuri wananchi hawaioni .nafikiri viongozi wangekuwa wanaingia mikataba let say ya madini ambayo ina efffect nzuri ya moja kwa moja kwa wananchi nina uhakika wananchi wangekaa kimya na matatizo mengi tu yasingekuwepo lakini wanajiangalia wao tu kwanza
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Kuna Propaganda nyingi sana zinatembea kwa sasa.

  Ni kweli miaka ya 90 Russia kulikuwa msoto sana ila kwa sasa jamaa wengi wanaishi maisha mazuri. Ni vijijini na hasa mbali na Moscow ndiko bado watu wana hali mbaya kulinganisha na Moscow.

  Ukiangalia hata kwenye Googleearth, miji mingi sana inabadilika. Miji inajengwa, madaraja mapya, viwanja vya ndege vinatengenezwa, viwanja vya michezo vinatengenezwa na kila aina ya mabadiliko. Kwa sasa wanasema kwamba "Russia kuna mabenz mengi zaidi ya German."

  Russia siku hizi vijana hawashindani tena "wewe unaendesha gari gani maana hao wako wengi sana wenye magari makali ya bei mbaya..." Sasa hivi Russia wanatambiana "wewe una ndege gani au helcopiter gani."

  Nina mshikaji wangu mmoja Europe ambaye huwa anakuwa Russia kama 1/3 ya siku zake kwa mwaka huku akitembelea miji mingi sana Russia. Huwa nikimpata kwenye SKYPE huwa ananipa story nyingi sana ya jamaa hawa Warusi. Mwanzo alipoenda alikuwa na imani kuona umasikini wa ajabu. Kufika huko ameishiwa nguvu kukuta jinsi jamaa wanavyoishi na hasa Moscow. Pia huwa anaenda sana kishughuli katika nchi kama za UK, German, France, Kazakastan, USA, Hungury nk nk nk.......

  Kwa sasa anasema Moscow kuna kitongoji ambacho jamaa wamejiwekea kama KIMJI chao wenyewe. Huingii hapo kama huna VISA (barua maalumu au kibali ya kufika hapo na kwa sababu gani kama huishi hapo. kwa wananchi wa kawaida ni kweli kabisa kuwa huduma kama Maji, Umeme, nk kila siku zinazidi kuwa nzuri na ndiyo maana hawajali sana akina Putin wanafanya nini Russia au Chechnia/Georgia.

  Kumbuka kuwa kama umezungukwa na matajiri, na wewe ni rahisi kuwa tajiri. Dada yako ataolewa hapo. Mshikaji wako atakuwa tajiri. Wewe utaowa mtoto wa Shangazi wa tajiri nk nk na utajiri unaanza kusambaa. Nasikia sasa hivi kuna shule ya akina dada jinsi ya KU-PIMP (kutongoza) mabwana matajiri bila ya kuangalia UMRI.

  Angalia mfano wa huu moja ya mji wa Siberia unaoitwa Novosibirsk.

  Novosibisk. Siberia. Russia. - SkyscraperCity

  Mkuu Ivungu, huyu ndiyo Tania wako wa zamani? Mtoto wa Novosiberisk, angalia picha kwenye link.

  [​IMG]
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,376
  Likes Received: 19,646
  Trophy Points: 280
  well said !! kama ushawahi kuishi moscow na USA you will not see any different,coz Russia ya sasa sio kama ile ya ucommunism hata wanawake wao sasa hivi washakuwa wajanja huwezi kumbeba tu kijinga kama zamani
   
 11. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #11
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,081
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Kweli kwa kuliganisha Urussi na Tanzania kuna mengi yanatufunza lakini pia sidhani kama Russia is a good role model for us. Ni kweli wako mbali na as we know Russia was once a rival of US thats already tells they were or they are at other levels to be compared with tiny country like ours.Kama jinsi ulivyotoa mfano wa Umeme kutokatika Moscow, lakini warussi wengi wanalalamika jinsi uchumi wa Russia ulivyojikita Moscow na kuacha baadhi ya miji mingi ikiwa kama outsiders. Kama umekaa Russia 5 yrs you know what I mean, Moscow ndio kila kitu na tofauti yake na miji mingine ambayo ni zaidi ya 100, ni kubwa mno.St petersburg ndio second largest lakini bado imeachwa mbali kwa hiyo that unequal distribution tayari ni kiashirio kwamba kama sie Tz tungekuwa on the same path, only Dsm ndio wangeneemeka lakini kwingineko wangekuwa kama wako nchi nyingine.Jingine baya la Urussi ni rushwa iliyokithiri hiyo kweli Medvedev na Putin they got work to do.Russia kuna kubebana pia na bila connection huwezi kufanya lolote la hilo sio siri linaudhi sana.Lakini what I agree with you ni kwamba at least warussi wana uzalendo mkubwa tofauti sana na viongozi wa Tz ambao kwao hiki ki-nchi masikini kabisa wao wanakuwa vinara wa kukishindilia kaburini.Inatia uchungu sana kuwa masikini and on top of that kuiibia nchi yako kile kidogo sana kilichobakia. Kizazi kijacho kitarithi nini? Hata Moscow imejengwa zamani kizazi cha sasa wameikuta lakini kwetu naona jamaa hawana mpango na kizazi kijacho.
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,376
  Likes Received: 19,646
  Trophy Points: 280
  mkuu maswala ya rushwa hayo yapo hadi white house, kuna shangazi yake Obama alizamia US lakini baada ya Obama kupata urais ile kitu ikaisha kinyemela hii kitu naweza kuiita rushwa in other side,a rushwa as a rushwa unaweza kuipunguza tu na huwezi kuimaliza kamwe katika maisha ya binadamu kujuana kupo kila mahali na kweli Urusi swala la kujuana wanalitumia ipasavyo na kama ulikuwa hujui ni kwamba Rais Medvedev wa Urudi wa sasa alikuwa ni school met wa Putin na wote walisoma st peters kama sikosei na ukiangalia uongozi mzima umejaa marafiki,classmet na ndugu ,hapa sitabishana na wewe ila kitu mbacho mimi nakiangalia ni utendaji kazi wao na upendo kwa nchi yao na rasilimali zao,ndio kuna vitu vingi watakuwa wanajipendelea lakini asilimia kubwa hawa jamaa wanatetea taifa lao na rasilimali zao na hakuna mtu anayeweza kwenda kuiba gesi yao na mafuta yao na ajira zao,au kuwaingiza katika mikataba mibovu haya mambo yote yanawanufaisha wananchi ,sasa ukija kwetu Tanzania hii kitu ni (NAABAROTI)kwa kirusi hii inamaanihs ni virseversa ,sisi viongozi wetu hawajali kitu wanasaini tu makaratasi bila hata ya kuyasoma na wengi wao ni wagumu kuwajibika, na hapa ndio tatizo linapotekea ,wanatudharau sana na ukiwakamata pabaya wanaleta udini believe me hii ndio ngao yao kwa sababu wakishaleta udini lazima kunakuwa na mgawanyiko,sasa mpaka sasa hivi mimi sijajua solution ya hii kitu labda katiba ndio inaweza kusolve hili tatizo la kuwa na viongozi wasiojali na wasiopenda kuwajibika.nikupe mfano tu JK juzi juzi hata mwezi haujaisha kuna chuo kilimtunuku degree ya heshima sasa hivi hicho chuo kuna migomo ina maana yeye JK hawezi kuwasaidia hawa jamaa direct? au yeye hana taarifa? sasa hapa umakini wa kiongozi hauonekani.ingekuwa kweli hayupo madarakani kwa manufaa yake na angekuwa hana madharau hii kitu angeweza kutoa tamko na kuchukua warusi wanaita (balinaya reshenyia) maana yake maamuzi magumu bila kumuangalia nyani usoni na mgogoro ungeisha hapo hapo.ngoja nikupe mfano mwingine wa urusi..meya wa moscow amabaye alikuwa anaitwa Yury Luzhkov alikaa madarakani kwa muda usiopungua miaka 15 lakini badae akalewa madaraka na aalifanya vitu vingi tu kwa huo mda lakini wananchi walichoka na kuna baaadhi ya mambo yalikuwa hayaendi kama wananchi wanavyotaka,wananchi wakataka jamaa a resign lakini yeye akakataa baada ya kukataa ndani ya masaa yasiopungua 24 rais Medvedev alisaign barua ya kumsaafisha kwa lazima.baada ya hapo mgogoro ukaisha maandamano hayakufanyika tena na maisha yao yakaendelea kama kawaida,sasa haya mambo kwetu hayapo tunaendekeza ushemeji tuuu.believe me tunakakiwa tufanye kazi ya ziada kwa sababu wazungu tunawahusudu lakini hao hao wenyewe sio kwamba wana akili za darasani kutupita waliosoma nchi za mbele wanaweza kunithibitishia hili
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,376
  Likes Received: 19,646
  Trophy Points: 280
  [​IMG][​IMG]
  uwiiiiiiiiiiii !! SIKONGE ndugu yangu usinikumbushe siku police aliponikamata kwenye lift na kunipeleke kwenye chumba chake na kunikaribisha mzinga wa vodka,asubuhi akaniambia kuwa mimi ni choklate !!! haya mambo usiombe yakukute unaweza usirudi nyumbani TZ
  :car::focus:
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,376
  Likes Received: 19,646
  Trophy Points: 280
  sikonge ukitaka kwenda moscow unishtue nimwambie mamaa akuunganishe na kaka zake but if only you drink ndio unitafute kama hupigi moja baridi moja moto basi haina haja
  [​IMG]
  uwii naimiss hii kitu
   
 15. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #15
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,081
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Mkuu kweli rushwa ipo sehemu mbali mbali lakini kuna levels tofauti na Russia ni mojawapo wako kwenye level kubwa katika corruption.Sasa ukijustfy kwamba hii ipo tu hata white house hawa kina vijisenti nao wanaweza wakaegemea on that justication na at the end of the day tutarudi palepale. Hebu ya Warussi tuwaachie wao maana naona yetu yamevuka mpaka hasa hili swala ulilogusia la kukimbilia kujificha kwenye nguzo ya udini mtu akishaboronga.Kama watanzania wengi wangekuwa na uelewa mkubwa hili lisingekuwa tatizo ila nina wasiwasi kwamba kutokana na uelewa mdogo watu wamekuwa wepesi kusahau uhalisia wa hoja na kuhamia kwenye udini. hii haitakuwa na mwisho mzuri kwa sababu lengo zima la kuisogeza Nchi another step linamezwa na kutatua issue ndogo zinazochochewa na watu kwa mgongo wa udini.
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,376
  Likes Received: 19,646
  Trophy Points: 280
  well said mkuu Mgalanjuka,appreciate
  ila mimi nadhani suala ni elimu bora kwa vizazi vyetu jambo ambalo mimi hadi nikifikiria solution yake kwamba tutapataje elimu bora hapa nchini kwetu bado linaniumiza kichwa na tukisema tumuombe tu Mungu hii peke yake haitoshi ,na ukisema kuwa labda watu wakielimika basi wataachana na mambo ya udini sijui kama hii ni solution bado kwa sababu wanaoingiza mambo ya dini ni wameelimika vya kutosha
   
 17. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #17
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,081
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Mh hiyo kitu noma, lazima usitue na samaki au um-sniff mtu kichwani ukipiga shot! :)
   
 18. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #18
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,376
  Likes Received: 19,646
  Trophy Points: 280
  mkuu hii kitu inapigwa na kalbasa ,kalbasa ina ingredient nyingi ya nyama na inakupa nguvu
  [​IMG]
   
 19. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #19
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,081
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Duh Pazhalusta! Nimesikia ubao na kiu ghafla.
   
 20. Marunde

  Marunde JF-Expert Member

  #20
  Jan 14, 2011
  Joined: Jun 9, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 60
  wakuu mimi niko Moscow karibu yote waliosema wadau hapo juu ni sahihi bip up! guys wellcome to Moscow!.
   
Loading...