The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 617
- 1,790
Habari wanaJF,
Natumai mungali bukheri wa afya. Niende kwenye mada.
Ikiwa imesalia miezi kadhaa tu kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu nchini Burundi, nchi ambayo inakosolewa na jumuiya ya kimataifa kwa ukiukaji wa haki za binadamu na ukandamizaji dhidi ya upinzani, inaimarisha uhusiano wake na Urusi, suala ambalo wachambuzi wa mambo wanathubutu kufikiri kuwa huenda taifa hilo la Afrika Mashariki likategemea msaada wa kisiasa toka Urusi.
Juzi Jumanne akiwa katika ziara iliyolenga kuimarisha mahusiano baina ya Burundi na Urusi jijini Moscow, Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Ezekiel Nibigira alifanya mazungumzo na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov ambaye aliweka bayana kuunga mkono kutoingiliwa kwa Burundi katika masuala yake ya ndani.
"Tumethibitisha msimamo wetu usiobadilika kuhusu uhuru wa Burundi. Na tukasema kwamba kuingilia kwa mataifa ya kigeni katika maswala ya ndani ya Burundi haikubaliki ", alisema Lavrov.
Kwa hatua hii, Urusi imeonesha uungaji wake mkono wa bila kupepesa macho kwa viongozi wa Burundi, tofauti na nchi nyingine za Magharibi ambazo zimekuwa zikiishutumu vikali nchi hiyo kwa ukandamizaji wa haki na uhuru wa raia wake.
"Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Serikali na wananchi wa wa Urusi. Hapa ningependa kusisitiza misaada mbalimbalii Burundi inayopata kutoka Urusi. Misaada mbalimbali muhimu ya Urusi kwa Burundi inaonesha uhusiano wa ndani kabisa kati ya nchi hizi mbili” alisema Bw. Nibigira
Ikumbukwe kuwa tangu mwaka 2015 wakati mgogoro wa kisiasa ulipoanza nchini Burundi, baada ya Rais Nkurunzinza kutangaza kuwania muhula mwingine, vyombo huru vya habari nchini humo na mashirika yasiyo ya kiserikali vimefungiwa huku raia wakiripotiwa kutoroka nchi hiyo.
Je, uungaji mkono huu wa Urusi kwa Burundi unaweza kuleta matokeo gani?