Russia bado si salama kwa wanafunzi wa kiafrika

Andrew Kellei

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
348
123
Wadau bado lile wimbi la mauji ya wanafunzi wa kiafrika hasa wenye ngozi nyeusi wanaosoma Urusi linaendelea.Baada ya kuripotiwa mauaji ya mwanafunzi kutoka Zambia na baadaye Nigeria,sasa hivi yamaripotiwa mauaji ya mwanafunzi wa kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliyekua anasoma mwaka wa tano katika Chuo Kikuu Cha Ufundi (DGTU)cha mjini Rostov na Danu.Mwanafunzi huyo anayejulikana kwa jina la Tressor Monga amekutwa amekufa katika mji mdogo uliokaribu na Rostov unaoitwa Bataiski.
Kwa mnaoelewa kirusi mnaweza kufuatilia hii site hapa chini.
В Батайске погиб студент из Конго В Батайске погиб студент из Конго
www.donnews.ru
 
warusi bado hawapendi wageni,nilshawai ona kwenye tv mrusi aliingia bar na msichana wa kiafrika,akafukuzwa huyo msichana,
ikabidi jamaa amfuate dem wake watafute bar nyingine
 
Kama mmeshajua kuwa hampendwi kwanini mjipelepeleke kwenye nchi yao!.
 
Ubaguzi ulaya bado upo sana...

Mkuu ubaguzi si Ulaya tu, hata hapo TZ tunabaguana kiaina, ila tatizo la Urusi ni nchi ambayo utawala wa sheria uko chini sana hasa kwenye kujali utu wa mtu, sawa na nchi za kiarabu au kwetu. Uhai wa mtu hauna dhamani sana. most of western countries hata kama individuals wana ubaguzi kuua ni ngumu sana maana serikali zinafuatilia.
Kuweni macho mnao kaa Urusi maana warusi wengi wamechoka maisha wanadhani tatizo ni nyie.
 
aisee .... very very sad.
Chonde Chonde mlio kwenye nchi za kigeni. Tulieni Mmalize masomo mrudi salama.
Kesi nyingi za vifo zinatokana na wivu wa mapenzi na dhuluma za fedha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom