Rushwa yavuruga Bunge, zamu inayokuja ni dhidi ya Bernard Membe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rushwa yavuruga Bunge, zamu inayokuja ni dhidi ya Bernard Membe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 2, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Raia Mwema | Toleo la 252 | 1 Aug 2012

  BAADA ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu wake Mkuu, Eliakim Maswi, kunusurika kung'olewa na mtandao wa mafisadi kupitia kwa wabunge wanaodaiwa kupewa rushwa kutimiza azma hiyo, taarifa zinaeleza zamu inayokuja ni dhidi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.


  Membe anatarajiwa kuwasilisha hotuba yake bungeni wiki ijayo, na inaelezwa kwamba msimamo wake dhidi ya watuhumiwa wa kashfa ya ununuzi wa rada umemfanya kusubiriwa kwa hamu na baadhi ya wabunge ambao nao wanaelekezewa tuhuma kupewa fedha na mafisadi ili kushinikiza kumng'oa waziri huyo au hata kumchafua wakati wa mjadala wa bajeti ya wizara yake.


  Maandalizi hayo dhidi ya Waziri Membe yanakuja katika wakati ambao, vyanzo kadhaa vya habari vya gazeti hili vinamnukuu Rais Jakaya Kikwete akipata kumweleza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwamba; "nimechoka kuapisha mawaziri wapya," akiwa na maana hataki kumpoteza waziri yeyote kwa sasa.


  Kikwete anakaririwa kutoa kauli hiyo baada ya joto la mafisadi kupitia wabunge kutaka kumng'oa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter na Katibu wake, Maswi ambao wanaaminika kudhibiti mirija ya unyonyaji ya mafisadi iliyopachikwa katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).


  Mpambano uzalendo vs ufisadi

  Katika harakati za kuokoa jahazi na kudhibiti nguvu ya mafisadi katika kuwang'oa viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, baadhi ya mawaziri, wabunge na timu nyingine maalumu zilizoshirikisha viongozi kutoka makao makuu ya CCM, zilishiriki huku baadhi ya wabunge wa kambi ya upinzani wakiunga mkono juhudi hizo katika imani ya kupigania maslahi ya Taifa.

  Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa stahili iliyokuwa ikitumiwa ni kupita kila walipokuwa wakipita ‘mawakala' wa ufisadi ambao nao walikuwa wakiwaona wabunge mmoja mmoja kwa kuzingatia orodha waliyojiandalia.


  Katika juhudi hizo, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, anadaiwa kulazimika kutumia usafiri wa bajaji nyakati za usiku kupita kwa baadhi ya wabunge ili kuwaeleza hali halisi ni kwa nini viongozi wapya wa Wizara ya Nishati na Madini wanapigwa vita.


  Mbali na Waziri Kabaka, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, ambaye ni Mbunge wa Shinyanga Mjini, naye alikuwa na kazi maalumu ya kupita kila alipokuwa akipita mbunge mmoja kutoka moja ya majimbo mkoani Arusha (CCM).


  Inadaiwa kuwa mbunge huyo alikuwa na kazi ya kusambaza fedha ili ‘kuwanunua' wabunge wafanye mashambulizi dhidi ya uongozi wa wizara, fedha ambazo alizipata kutoka kwa baadhi ya kampuni zilizowahi kufanya biashara na TANESCO kwa njia za kifisadi.


  "Kazi ilikuwa moja tu, wao wanapoondoka katika ‘kijiwe' fulani baada ya kugawa fedha sisi tulikuwa tunakwenda kueleza ukweli na kwa kulinda maslahi ya nchi badala ya maslahi ya genge la wafanyabiashara wanaotafuna nchi," alieleza mtoa habari wetu.


  Mbunge wa Mwibara, Alphaxard Kangi Lugola naye anadaiwa kutembea kilomita kadhaa bila usafiri wa chombo chochote, akitoka hoteli moja kwenda nyingine ili kuweka mambo sawa kwa kufichua ukweli kwa wale waliopewa rushwa.


  "Kazi ilikuwa moja tu ambayo ni rahisi. Ilikuwa ni kazi ya kusema ukweli, kwa maslahi ya nchi. Tulikuwa tunasema fedha za rushwa zimetoka kwa nani, kwa sababu gani na kwa maslahi ya nani na kwa malengo gani hasa dhidi ya nchi," alieleza mtoa habari wetu.


  Waziri Mkuu na Rais Kikwete

  Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa siku chache kabla ya joto la mafisadi kupanda na kuelekea kutaka kufanikiwa, Rais Kikwete anatajwa kumwita Waziri Mkuu na kumweleza kuwa amechoka kuapisha mawaziri wapya.

  Kauli hiyo ni kama ilikuwa agizo kwa Waziri Mkuu ambaye kichwani mwake alikuwa na kumbukumbu ya shinikizo la wabunge lililosababisha kusukwa upya kwa Baraza la Mawaziri.


  Baada ya hapo, Pinda aliitisha kikao cha wabunge wa CCM walioko katika Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini. Wengine waliokuwamo katika kikao hicho ni pamoja na Spika wa Bunge, Anne Makinda, Waziri Profesa Muhongo na Katibu Mkuu, Maswi.


  "Kikao kilidumu kwa saa sita hivi. Hali ilikuwa tete na Katibu Mkuu aliwaumbua baadhi ya wabunge. Aliwataja kwa majina wanaonufaika na TANESCO ambao ndio hao waliokuwa wakitetea viongozi waliosimamishwa kazi TANESCO warejeshwe.


  "Wabunge wawili wa Viti Maalumu walirushiana matusi pale. Mmoja alimwambia mwenzake anatetea ufisadi wa TANESCO kwa kuwa anafanya biashara na shirika hilo, naye alisimama kumjibu bora yeye anafanya biashara na TANESCO kuliko mwenzake huyo anayefanya biashara kwa kuuza mwili wake.


  "Maswi pia alimkumbusha mbunge mmoja namna alivyowahi kwenda kumwomba rushwa ya shilingi milioni 50 ili aende akawagawie wenzake. Alipomwambia hana kiasi hicho cha fedha alipunguza dau hilo hadi shilingi milioni 20. Ushahidi wa hilo umehifadhiwa na utawasilishwa sehemu husika," kinaeleza chanzo chetu cha habari.


  Malecela aitwa kuokoa jahazi

  Waziri Mkuu wa zamani, John Malecela, alilazimika kutumika pia. Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatajwa kumwomba amweleze hali halisi mbunge mmoja kutoka mkoani Arusha ili aache kuendelea kuwa wakala wa mtandao wa mafisadi waliokuwa wakinufaika na TANESCO.

  "Mzee Malecela alikaa na .... mbunge (jina linatajwa) akamweleza kila jambo lakini jamaa alikuwa kichwa ngumu. Mzee alimwambia unakwenda kujimaliza kisiasa siku si nyingi, yeye akaendelea na msimamo wake, kwa hiyo Mzee akamwacha na sasa hali yake kisiasa ni mbaya. Yeye ni sehemu ya wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa," kinaeleza chanzo chetu cha habari.


  Siri ya wabunge kuomba rushwa

  Siri za baadhi ya wabunge wa Bunge na hasa katika kuomba na kupokea rushwa nazo zimezidi kuanikwa na baadhi yao, wakilieleza Raia Mwema kwamba, wengi waliochukua mikopo ya hadi shilingi milioni 200 na kuanzisha biashara, biashara hizo zimekufa na mshahara wao ‘unatumikia' mikopo hiyo na kwa hiyo, hawana chanzo kingine cha mapato.

  Kutokana na hali hiyo, wabunge wamekuwa wakililia nyongeza ya mishahara na posho na kwa kupitia kamati zao wengine wanadai hufanya shinikizo la kupewa semina na baadhi ya mashirika na taasisi za umma.


  Baadhi ya wabunge waliozungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa gazetini wamesema mbali na wabunge kuwa katika hali hiyo ngumu, kuna udhaifu wa serikali kiasi cha kuacha wabunge kuingilia shughuli za kiutendaji za kiserikali.


  "Kutokana na serikali kama mhimili wa dola kuonekana kuzidiwa na Bunge na hivyo kuwa too submissive to the parliament (kujisalimisha kwa Bunge), Bunge limejikuta likitumia vibaya nafasi yake ya kuisimamia na kuishauri serikali kwa kujiingiza kwenye masuala madogo madogo ya utawala na utendaji wa siku hadi siku.


  "Wameacha kuisimamia serikali katika masuala ya kisera, sasa wanakuwa mawakala wa wafanyabiashara waliokosa zabuni au wafanyabiashara wanaofutiwa leseni," anaeleza mmoja wa wabunge kutoka Kanda ya Ziwa.


  Katika kuongeza nguvu hoja hiyo, mbunge mwingine anasema; "Wanaolalamika kuonewa au vyovyote wanapaswa kwenda mahakamani na si kwa wabunge, tena kwa kuwapa fedha.


  "Wafanyabiashara wengi wanaoathirika na uamuzi wa watendaji wa serikali, siku hizi hawaendi tena kortini kupinga uonevu wanaodhani wamefanyiwa, wanakimbilia bungeni kwa wabunge."


  Mbunge mwingine kutoka Nyanda za Juu Kusini anataja sababu nyingine za wabunge kudai rushwa ni mfumo wa uchaguzi wa wabunge ambao ni wa gharama kubwa na baada ya uchaguzi, wananchi waliosaidia kampeni za mbunge wamekuwa wakiwageuza wabunge kama vyanzo vya mapato yao.


  Anasema wabunge pia huchukua mkopo na kuanzisha biashara ili kujiongezea kipato lakini wengi kwa kukosa utaalamu wa biashara, biashara hizo zimekufa na wakati huo huo, mishahara yao ikikatwa kwa sehemu kubwa kufidia mkopo.


  ‘Kamati Maliasili ivunjwe'

  Baada ya wito wa kutaka kamati za Hesabu ya Mashirika ya Umma inayoongozwa na Kabwe Zitto, Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa inayoogozwa na Augustine Mrema na Serikali Kuu ya John Cheyo zivunjwe, kama ile ya Nishati na Madini kutokana na tuhuma mbalimbali za ufisadi, wito umetolewa sasa kwa Spika Makinda kuvunja kamati nyingine za Bunge.

  Kamati hizo ni pamoja na Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, Kamati ya Uchumi na Fedha na Kamati ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje.


  Kamati za Ulinzi na ile ya Uchumi na Fedha zinashinikizwa na baadhi ya wabunge zivunjwe kwa kuwa wenyeviti wa kamati hizo tayari uadilifu wao unatiliwa shaka mbele ya wananchi. Kamati hizo zinaongozwa na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na ile ya Uchumi inaongozwa na Andrew Chenge.


  Lowassa alijiuzulu baada ya shinikizo kutoka katika Bunge la Tisa akihusishwa na kashfa ya kampuni tata ya ufuaji umeme ya Richmond. Chenge anatazamwa kama kiongozi aliyefanikisha ununuzi wenye utata wa rada ambayo mchakato wake ulitikisa mapaka kwenye bunge la Uingereza.


  Lakini wakati hali ikiwa hivyo kwa Lowassa na Chenge, Kamati ya Ardhi inayoongozwa na Mbunge wa Kahama, James Lembeli, inadaiwa kutiwa mfukoni na genge la wafanyabiashara, ikidaiwa kwamba kwa nyakati tofauti genge hilo limewahi kuwalipa posho wajumbe wa kamati hiyo ili kujadili uamuzi wa serikali wa kuzuia vibali vya usafirishaji wanyama nje ya nchi.


  Kamati hiyo ya Lembeli ‘ilitiwa mfukoni' na wafanyabiashara hao katika kikao kilichofanyika Siku ya Jumapili (Novemba 6, 2011), siku ambayo si siku ya kazi za Bunge na inadaiwa wajumbe walilipwa na wafanyabiashara hao. Semina hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, bungeni mjini Dodoma.


  Kamati hiyo pia inadaiwa kuwahi kulipiwa ukumbi wa semina na posho kwa wajumbe wake na wafanyabiashara wa uwindaji wa kitalii, semina iliyofanyika katika Ukumbi wa Mtakatifu Gaspar, mjini Dodoma, Aprili, mwaka huu.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Kazi haswa... Sasa Ina Maana huyo Mbunge wa Arusha Mzee Malecela aliyeongea nae ni Ole-Sendeko???

  Kwahiyo CCM itamtema??? Ina Maana Siri zitatoka kibao... CCM oh CCM ... SAMAKI MMOJA AKIOZA....??
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  huyo mbunge anayeuza mwili wake ni nani?.........................., Halaf kumbe Pinda haheshimiwi na wabunge kabisa ndo mana wanafikia hatua ya kurushiana kashfa nzito na za aibu mbele yake!
   
 4. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Kumbe huyo mbunge anauza mwili sijui ana wauzia wabunge au wana dodoma.

  Itakuwa posho yake ana rudisha fadhila ya kupata ubunge, sasa ana bakiwa bila kitu kwa hiyo kipochi ni solution kwake.
   
 5. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Njedi bila kupepesa macho anaitwa Vick kamata....
   
 6. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,161
  Trophy Points: 280
  Mimi sioni ajabu kwa baadhi ya wabunge (may be walio wengi) kwa vile wabunge wetu ile tamaa ya kujilimbikizia posho na kujipandishia mishahara, watu wa aina hiyo wakipata rushwa watapokea tu1 Unaona kuwa hawa watu wana uroho/uchu wa mali bila kujali wanaowawakilisha wana maisha gani!
   
 7. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Hahaaa..huyu VK si ndio nasikia pale head office wanakula kama hawana akili nzuri....tutasikia mengi mwaka huu
   
 8. m

  mharakati JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ili kumjua angalia hizi hints

  -mbunge wa viti maalum
  -ndani ya kamati ya madini
  -ili auze mwili atakua ni mdogo kiumri na labda anavutia vutia (mwanamke hamtukani mwanamke mwenzake anajiuza kama anamuona ni mbaya kuliko yeye)
  -atakua ni mgeni bado hajapewa dili za kifisadi siyo mzoefu wa kutosha kama huyo mwenzake (anatiliwa wasi wasi na mafisadi kwa kiasi fulani anaweza kuwaanika)

  kama unajua wabunge utamjua huyu mtu
   
 9. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Mmoja kati ya wateja wa biashara yake ya mwili ni JK
   
 10. H

  Haki Yetu Senior Member

  #10
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu na huyo anayefanya biashara na TANESCO? ...............nadhan ni huyo aliyetajwa kuuza matairi mabovu kwa bei ya kupaa!
   
 11. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Ni ajabu sana kumshambulia Zitto iwapo tuliacha Lowasa na Chenge kushika kamati kubwa za Bunge
   
 12. m

  markj JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  mtoto mtamu sana huyu! Wakati niko dodoma nilikuwa naonja onja mara 1 1! Katamu jaman! All in all watanzania wenzangu tujiandae dhidi ya wabunge mana inaonesha wazi wabunge wote wanamaslahi yao na si wananchi! Na ni uhakika kuwa wote wanayajua yanayofanyika mabaya! Na wanatuficha ila wanajifanya kuibua yale madogo yasio na ishu sana, sasa makubwa yameanza kujitokeza! Dah! Bora dr.slaa angekuwa mbunge nadhani tungepiga hatuwa kubwa nda ya bunge mana hata hawa wengine tuliona wanatujali kumbe ndo walewale tu.
   
 13. Young Tanzanian

  Young Tanzanian JF-Expert Member

  #13
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,740
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Membe aache kutapatapa tunataka fedha za ghadafi huyu jamaa mbona analia ata ajaguswa apa kuna kitu na atatueleza yote na ya hawa mabaloz wanaotembeza matajir wa nigeria kwenye ofs za vyama...asijbu jf aende bungen malechela alishashndwa siasa
   
 14. Young Tanzanian

  Young Tanzanian JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,740
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Yeye anajua wizara yake imejaa madudu hana jipya mwambie tumemkatalia hata uwazr hafai
   
 15. Young Tanzanian

  Young Tanzanian JF-Expert Member

  #15
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,740
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Puma haisafshiki...apa wameonga wabunge wasafshe puma ilivyopewa tenda kwa shnkzo la mtoto wa kgogo wakat ilishashndwa hawahawa wanaojiita wazalendo wanaamn et huyo dogo atawasaidia kufikia malengo yao ya urais 2015 hii nchi ni ya watanzania si shamba la bb
   
 16. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #16
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu anaye uza matairi ni mwingine na anayetoa mzigo ni mwingine.:wacko:
   
 17. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,792
  Likes Received: 3,879
  Trophy Points: 280
  BAADA ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu wake Mkuu, Eliakim Maswi, kunusurika kung’olewa na mtandao wa mafisadi kupitia kwa wabunge wanaodaiwa kupewa rushwa kutimiza azma hiyo, taarifa zinaeleza zamu inayokuja ni dhidi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

  Membe anatarajiwa kuwasilisha hotuba yake bungeni wiki ijayo, na inaelezwa kwamba msimamo wake dhidi ya watuhumiwa wa kashfa ya ununuzi wa rada umemfanya kusubiriwa kwa hamu na baadhi ya wabunge ambao nao wanaelekezewa tuhuma kupewa fedha na mafisadi ili kushinikiza kumng’oa waziri huyo au hata kumchafua wakati wa mjadala wa bajeti ya wizara yake.

  Maandalizi hayo dhidi ya Waziri Membe yanakuja katika wakati ambao, vyanzo kadhaa vya habari vya gazeti hili vinamnukuu Rais Jakaya Kikwete akipata kumweleza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwamba; “nimechoka kuapisha mawaziri wapya,” akiwa na maana hataki kumpoteza waziri yeyote kwa sasa.

  Kikwete anakaririwa kutoa kauli hiyo baada ya joto la mafisadi kupitia wabunge kutaka kumng’oa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter na Katibu wake, Maswi ambao wanaaminika kudhibiti mirija ya unyonyaji ya mafisadi iliyopachikwa katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
   
 18. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama amechoka kuapisha mawaziri wapya basi awe anateua mawaziri wachapa kazi na wenye uwezo wa kuongoza wizara na sio kuweka maswahiba wake, matokeo yake ndo haya mawaziri wanavurunga
   
Loading...