Rushwa yakithiri mchakato wa kuwapata wawakirishi wa bunge la e.a | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rushwa yakithiri mchakato wa kuwapata wawakirishi wa bunge la e.a

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ELIESKIA, Apr 15, 2012.

 1. E

  ELIESKIA Senior Member

  #1
  Apr 15, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  tumezoea kuona ccm wakitoa rushwa za kofia,tshirt na pilau ili wawachague . nimesoma kwny blod ya mjengwa nikaluta post ya zitto akisikitika kwny FB kuwa rushwa imekidhiri kuwapata wabunge wa kuwakilisha bunge la afrika mashariki. kama wananch wanahongwa kofia wabunge wanahongwa nn
   
 2. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wabunge huenda watakuwa wanahongwa bia mzee lol
   
 3. A

  Antar bin Shaddad JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  si wote wanaotoa rushwa namfahamu mgombea Mrisho Gambo hatoi rushwa hata kidogo!
   
 4. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Huu ni wakati mwingine wa serikali kuonyesha kama kweli wanaweza kudhibiti rushwa. Tunaambiwa kuna mwanadada ambaye anamwaga fedha kama hana akili nzuri na kwa kweli ni kuanzia milioni moja kwenda juu. Cha ajabu hana biashara inayojulikana ya kumfanya awe na uwezo wa kuwa na kiasi hicho cha fedha. Katika moja ya nafasi kabla ya hii ya Afrika Mashariki, alitumia zaidi ya Sh milioni 300 lakini akabwagwa na mpinzani, sasa tena anatumia mamilioni, anazitoa wapi hizo fedha na anapozimwaga ni faida ama mtaji wa hiyo biashara yake? Anawaambia wabunge kwamba anafanya biashara ya Import and Export lakini haijulikani hasa anavyoifanya maana kabla ya 2010 alikua kiongozi tu wa CCM wa wilaya!!!! Jamani hapo Takukuru wanahitaji kweli kusaidiwa na SFO? FIU hivi mpaka mupate nyaraka? Tunakwenda wapi kama Taifa? Kwamba kila nafasi ya uongozi inapatikana kwa fedha? Vyombo vya dola visikate tamaa na yaliyotokea Arusha, vifanye kazi na kuweka katika kumbukumbu. Mbona Muheza Mbunge kashitakiwa mwaka huu kwa rushwa ya 2010? Vita hii isiishie kwa hao wanasiasa pekee ihusishe na vyanzo vyao vya mapato maana yaweza kuwa ni wahalifu wanataka kutupandikizia watu wao, je, tuko tayari?
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,408
  Likes Received: 81,442
  Trophy Points: 280

  Wanachukua Dollars, Pounds au Euro hela za madafu hawataki hata kuzisikia. Nimemuona Mbunge mtarajiwa mmoja kwenye picha mbali mbali jinsi anavyojikomba ili kupata kura za kuingia kwenye Bunge hilo kusema kweli inatia kinyaa na bado atatoa mshiko mnene kwa hao wapiga kura ili wampitishe....Kweli siasa ni mchezo mchafu.
   
 6. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Uhai wa chama cha CCM unategemea rushwa! Bila rushwa hakuna CCM!
   
 7. N

  Ngarenaro JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwani huu ubunge wa A/Mashariki ndio ule wa Masaburi?
   
 8. W

  Wakati Member

  #8
  Apr 16, 2012
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasemekana zoezi la kuwapata wawakilishi wetu katika bunge la Afrika mashariki limegubikwa na rushwa kwa kiwango kikubwa kiasi cha kuleta wasiwasi juu ya uthabiti wa ushiriki wetu kama nchi katika bunge hilo lijalo.

  Source: Zitto Kabwe twitter account
   
 9. W

  Wakati Member

  #9
  Apr 16, 2012
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasemekana zoezi la kuwapata wawakilishi wetu katika bunge la Afrika mashariki limegubikwa na rushwa kwa kiwango kikubwa kiasi cha kuleta wasiwasi juu ya uthabiti wa ushiriki wetu kama nchi katika bunge hilo lijalo.

  Source: https://twitter.com/#!/zittokabwe
   
 10. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kuwa tweeter ni mtandao wa kijamii, huyu bwanamdogo zitto nadhani utaifa hana, wala hafikirii kuwa nao. yeye ni member humu, kuvipakua vyamoto huku haoni umuhimu, akijabanwa popote anakuja kutuumiza vichwa, nikiunganisha dot naona kama walivyo hawaipendi jf kina mukama na jk, wamemuelekeza naye kwani ni rahisi kujichanganya akabwatuka waliyopanga sirini.
  Hata mimi naanza kuwa na mashaka na ZITTO KABWE
   
 11. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tusishabikie, hili ni tatizo ambalo linaathiri hata wasiokuwa na vyama. Tuchukue hatua sote.
   
 12. K

  Keil JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu Halisi,

  Unataka kuniambia serikali na vyombo vyake vya dola havijui kwamba kuna rushwa inatembea? Kwa mahali tulipofika kuhusu tatizo la rushwa ni kwamba ni ngumu kulishughulikia.Vijana wa PCCB wao wenyewe wako frustrated maana unamshika mtu huku una evidence lakini ukisogeza kwa wakubwa unaambiwa huyo hutakiwi kumshughulikia na kama ikitokea kushikwa kwake kumefanyika mbele ya wambea then ushahidi utakaopelekwa kwa DPP ili kuomba ridhaa ya kesi kwenda mahakamani unakuwa ni mwepesi na hivyo kumpa ground DPP kusema hapa hakuna kesi.

  Serikali yetu na Chama tawala ni waumini wakubwa wa rushwa. Hivi mmesahau kwamba waliwahi kupitisha sheria ya TAKIRIMA? Hata hizo parties, dinner na lunch ambazo wabunge wanapewa ni sehemu ya "vitakrima" kabla hawajashikisha mamilioni ya shilingi. Ukijiuliza hivi mtu anahonga milioni zote hizo, in return anategemea nini? Maana hata nikikusanya mshahara wa wa Mbunge wa EALA kwa miaka 5 haufiki hayo mamilioni ambayo mtu anayateketeza ili apate huo Ubunge.

  Je, tuchukue hatua gani? Maana ukiwaita TAKUKURU au Polisi, hawaji kuwashika watuhumiwa.
   
 13. K

  Keil JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  YES, ila mwaka huu hajagombea maana ana "ma-ulaji" mengine makubwa kule Tume ya Jiji.
   
 14. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mkuu maneno yako sahihi kabisa. Mfano wa hivi karibuni ni wa Arumeru ambako Takukuru walikamata watuhumiwa wa CCM lakini CCM wenyewe wakaudharau ushahidi uliokusanywa na waliohusishwa wakaibuka kuwa wateule na waliowapinga wakaenda kufanya nao kampeni 'bega kwa bega', unadhani vijana wasio na uvumilivu wanaweza tena kukamata watu wa CCM? wamekatishwa tamaa, japo tumeshuhudia Mbunge wa CCM akifikishwa mahakamani kwa makosa aliyoyafanya mwaka 2010 wakati wa uchaguzi.

  Kwa sisi sote kuna njia nyingi za kuwashinikiza watawala waone umuhimu wa kuchukua hatua. Kwanza kwa kukataa rushwa katika mioyo yetu, na pili kuikataa kwa vitendo kila mtu katika nafasi zetu, kuanzia wananchi wa kawaida vijijini na mijini (hawa wanaweza kwa njia nyingi na zaidi ni kura zao), na kwa tunaobahatika kuingia kwenye mitandao, tuendelee kupiga kelele kama hivi tufanyavyo na waandishi wetu nao wafuate hayo hapo juu (namba moja na mbili) na waandike kuwazindua watawala na wanasiasa bila kuchoka, kama ilivyokuwa kwenye EPA, pamoja na kuwa bado wapo watuhumiwa ambao hawajaguswa. TUSIKATE TAMAA.
   
 15. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #15
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu hao hao wabunge si walipatikana kwa kuhonga? Kwa hiyo wanajua kuhonga na pia kuhongwa. Wabunge wengi wamechoka Mkuu hongo yao ni hela ya kununulia mafuta ya kuweka kwenye gari basi!
   
 16. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #16
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  Promo @ work.
   
 17. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  kimbunga vipi una hang over ? sijakuona jana mtaani
   
 18. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,795
  Likes Received: 2,569
  Trophy Points: 280
  Kunani bunge la EA, hadi tunatembeza rushwa kiasi hiki tuchaguliwe?
   
 19. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #19
  Apr 16, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM Bila rushwa haiwezekani!
   
 20. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #20
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,524
  Likes Received: 1,312
  Trophy Points: 280
  inauma brother.....dawa ni kukataa kushiriki michakato inayoshirikisha rushwa.....mfano hapa kwenye huu ubunge tuna taarifa za rushwa kutawala..haswa kwa wawakilishi toka ccm.....sasa kwa vile wao ni wengi na watatoa wabunge wengi kwenda EAC parliament..kwanini vyama pinzani vishiriki kuwapitisha watu waliopatikana kwa rushwa???..kufanya hivyo ni kushiriki rushwa.....I'm sure wanaotoa rushwa wanajulikana......dawa nyingine pia ni kuwanyima kura...maana inasikitisha mijitu inayotaka kutuwakilisha kama nchi inapatikana kwa rushwa......ikienda huko si ndio kwenda kushiriki kuihujumu nchi!!..maana watanzania wanashiriki kwa kiasi kikubwa sana kuimaliza TZ......
   
Loading...