Rushwa ya ngono sasa ni uhujumu Uchumi, ukikamatwa hakuna faini, ni kifungo miaka 20

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Habari wakuu,
IMG-20191121-WA0012.jpg

Leo TAKUKURU imefanya Kikao na Wadau wa habari kuhusu kampeni ya kupambana na rushwa ya ngono ijulikanayo kama Vunja Ukimya Kataa Rushwa ya Ngono.

Akiongea katika kikao hicho, Mwasheria wa TAKUKURU, Imani Nitume amesema kwamba kifungu Cha 7 cha PCCA kimeainisha majukumu ya TAKUKURU na Moja ya majukumu hayo ni kushirikiana na wadau katika mapambano dhidi ya rushwa.

Kwa kutekeleza jukumu hilo, TAKUKURU imeingia makubaliano na Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania-WFT katika kushughulikia kero ya RUSHWA YA NGONO nchini kwa kuanzisha Mradi wa Vunja Ukimya Kataa Rushwa ya Ngono.

Yamekuwepo malalamiko katika jamii dhidi ya rushwa ya ngono na tumeshuhudia baadhi ya vyombo vya habari vikitangaza uwepo wa tatizo hili kwenye jamii. Kwa kuliona hilo TAKUKURU kupitia Mradi wa Vunja Ukimya imeamua kuelimisha na kuhamasisha jamii kutolifumbia macho tatizo hilo kwa kujitokeza na kutoa taarifa za wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Sheria ya Kuzuia na Kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 imetamka kosa hili chini ya kifungu cha 25 ambapo kwa tafsiri isiyo rasmi kifungu hiki kinasema: “Mtu yeyote ambaye kwa kutumia nafasi yake au mamlaka yake katika kutekeleza majukumu yake anadai au analazimisha upendeleo wa kingono au upendeleo mwingine wowote kama kigezo cha kutoa ajira, kupandisha cheo, kutoa haki au upendeleo wowote unaotambulika kisheria atakuwa ametenda kosa.”

Kwa kutambua umuhimu wa mchango wa mwanamke katika mapambano dhidi ya rushwa, MACHI 8, 2019 TAKUKURU ilitoa TAMKO kuwa inaunga mkono juhudi zinazoendelea duniani kote za kuhakikisha kuwa wanawake wanalindwa na kwamba inapinga unyanyasaji na udhalilishaji wa aina yoyote ile unaofanywa dhidi ya wanawake ikiwemo kulazimishwa kutoa RUSHWA YA NGONO.Kuanzisha Dawati Maalum litakaloshughulikia RUSHWA YA NGONO katika ofisi zake zote.

Kupitia miscellaneous amendment act no 3 ya mwaka 2016 sheria ya uhujumu uchumi ilifanyiwa mabadiliko na kutambua makosa yote yaliyopo ndani ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa isipokuwa kosa chini ya kifungu cha 15 ni makosa ya uhujumu uchumi. Hivyo rushwa ya ngono kwa sasa ni kosa la uhujumu uchumi na adhabu yake sio faini tena ila ni kifungo cha miaka mpaka 20.

Ameiasa jamii kutoa Ushirikiano kwa takukuru ili kutokomeza rushwa ya ngono.

Unaweza kutoa taarifa katika Ofisi ya TAKUKURU iliyo karibu au kwa kupiga namba 113 au kwa kupakua Application ya TAKUKURU APP itakayokuweza kutoa taarifa za Rushwa bure kwa kutuma sauti, picha au Video.

 
Takukuru imesema tuhuma za rushwa ya ngono ni sawa na tuhuma za kuhujumu uchumi hivyo mtuhumiwa wa rushwa ya ngono ni muhujumu uchumi.

Source: Mtanzania
 
Hata kutokunywa chai asubuhi ni uhujumu uchumi

Hata kuingia chooni Mara 2 kwa siku ni uhujumu uchumi

Kila kitu sasa ni uhujumu uchumi kwa ccm

Nyenye...nyenyenye..nyenyenye ni uhujumu uchumi...!

Kumbafu wewe.
 
Hebu wanauchumi watufafanulie kivipi..? Mi nijuavyo watakuwa wamehujumu uchumi Kama wakifanyia vichakani,wasipolipa hata Senti ya kununua ndom wakafanya bure kabisa no gesti Wala mshikaki😎😎
 
Back
Top Bottom