Rushwa: Wakuu wa ununuzi wa bidhaa serikalini Kenya wapewa likizo ya lazima

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Serikali ya Kenya imewaagiza wakuu wote wa vitengo vya ununuzi wa bidhaa na huduma katika wizara na mashirika ya umma kwenda likizo ya lazima ya mwezi mmoja huku juhudi za kukabiliana na ufujaji wa mali ya umma zikionekana kushika kasi.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Wizara ya Usalama na Mambo ya Ndani Mwenda Njoka inasema maafisa hao wanafaa kukabidhi majukumu kwa manaibu wao kwa sasa.

Bw Njoka amesema ametuma taarifa hiyo kwa niaba ya msemaji wa serikali Bw Eric Kiraithe.

Maafisa hao pia hawataruhusiwa kusafiri nje ya nchi bila idhini ya Mkuu wa Utumishi wa Umma Joseph Kinyua.

"Ingawa shughuli hii inalenga kubainisha iwapo watumishi hawa wanafaa kuendelea kushikilia afisi hizo za umma, na kuendelea kuaminika katika idara ya utumishi wa umma, shughuli hii itafanyika kwa njia ya haki na bila kupendelea upande wowote, kwa umakini na kwa kuheshimu haki za kikatiba za wahusika," taarifa hiyo iliyopakiwa katika ukurasa wa Twitter wa kitengo cha mawasiliano cha rais inasema.

ke1.png

"Rais amejitolea kuunda idara ya utumishi wa umma ambayo inakidhi mahitaji na kuakisi matamanio ya Wakenya bila maafisa hao kutumia nafasi hiyo vibaya kujitajirisha au kujifaa."

Wakuu hao wa ununuzi wa bidhaa na huduma wanafaa kutoshikilia majukumu huku shughuli ya kuwapiga msasa ikitarajiwa kuanza.

Maafisa hao wanatakiwa kuwasilisha taarifa kuhusu mali wanayomiliki, madeni waliyo nayo na taarifa kuhusu kazi walizozifanya awali.

Maelezo hayo yanafaa kuwasilishwa kwa afisi ya Mkuu wa Utumishi wa Umma katika jumba la Harambee, Nairobi kufikia Ijumaa.

Bw Njoka hata hivyo amesema wataendelea kupokea mishahara yao kama kawaida katika kipindi hicho.

Hatua hiyo ndiyo ya karibuni zaidi kuchukuliwa na Rais Kenyatta baada yake kuahidi kukabiliana vikali na ufisadi serikalini wakati wa sikukuu ya Madaraka.

ke2.jpg

Bw Kenyatta, wakati wa maadhimisho hayo mjini Meru, aliagiza wakuu wote wa ununuzi wa bidhaa na huduma katika serikali, wachunguzwe upya kufikia mwisho wa mwezi huu.

Watatakiwa pia kupimwa kwa kifaa ambacho ni cha kubaini iwapo mtu anasema ukweli au anahadaa.

Watakaobainika wanasema uongo baada ya kutumiwa kwa kifaa hicho watafutwa kazi.

Chanzo: BBC Swahili
 
Wako wanaojua kupambana na ufisadi, sio akina sie tulioweka pombe kwenye chupa ya soda tukidhani haitalewesha
 
Taharuki iliyotanda nchini haswa serikalini itazaa matunda, yaani hela ya umma itakua na ukakasi, kila mtu atakua haitaki.
Mbele kwa mbele lazima pazaliwe kiumbe tulee.
 
Wako wanaojua kupambana na ufisadi, sio akina sie tulioweka pombe kwenye chupa ya soda tukidhani haitalewesha
Hehehe
Nimecheka noma, vipi zile shtukiza za kuambatana na media kwenye maofisi ya watu.
 
Bora wewe umesema ukweli, miaka yote mitano alikuwa wapi kabla ya kuanza maigizo haya.
Wameagalia kushoto na kulia wakona hapa, Tanzania itatuacha pabaya. Ngoja na sisi tujitutumue kidogo.

Its funny, walarushwa wakubwa ndio hao wanaongoza vita ya ufisadi, sasa sijuwi na wao watajichunguza. Acha tuangalie hii movie, labda starring anaweza kuuwawa.
 
Hamna cha Tanzania hapo. Mwaka wa 2015 Wakati wa Kikwete, Uhuru alifanya jambo kama hilo tu. https://www.nation.co.ke/news/polit...-Secretaries/1064-2669222-13v1faez/index.html

Vita dhidi ya ufisadi hauhitaji ukurupukaji wa Magufuli au Uhuru. Mambo ya kuamka siku moja kisha unatoa maagizo. Magufuli angekuwa Rais mzuri ikiwa angelijua kufanya kaza na watu. Tatizo lake ni kuwa yeye ni one-man-guitar. Shida ya Uhuru naye ni kuwa hana nidhamu. La pili, anapenda kupendwa na watu. Hupenda sifa za kipumbavu sana. Baada ya miezi mitatu atakua yuaendelea tu na sakata zake. Sasa wizi katika wizara hufanywa na watu wengi sana hadi kule chini kwenye district accountant. Vyote anavyofanya vitapingwa na mahakama.
 
Kwa miaka hii miwili iliyopita, Kenya imezama chini zaidi kwenye rushwa kubwa na ndogo katika ngazi zote za kiutawala kulingamisha na Tanzania. Na ndio maana, nikasema Kenya kama nchi, imeangalia kushoto na kulia ikaona kama tukiacha mambo yaendelee hivi, tutawapa watu sababu ya kupeleka biashara zao nchi zingine ikiwemo Tanzania. Sio siku nyingi wazungu walikuwa wanakuja Tanzania asubuhi, wanaingia wizara ya madini au kilimo au yoyote ile, wanachukuwa kubali jioni wanapanda ndege wanaenda kuchukiwa mikopo kwa vibali vya Tanzania. Leo vitu kama hivyo ni ndoto.

Ukitaka kulinganisha Magufuli na Uhuru, japo unasema Magufuli he is one guitar man lakini his one guitar man who can tell you in front of your face wewe mwizi, with no fear what so ever. But having said that, ukisema eti ni mtu mmoja ndio anapabana na rushwa nadhani hata wewe huwezi kuamini kama mtu mmoja anaweza kufanya kazi zote hizo. Kuanzia intelligence gathering, intelligence analysis, execute, mpaka prosecution.

Kitu ambacho sijaelewa ni idea ya serikali ya Jubilee kupambana na rushwa kwa kutumia lie detector. Yani Kenya hamna information ya who own hata kama anaficha kwa majina fake mpaka mkawapie kwenye lie detector? Mtu akija na cheti cha daktari akasema I have heart condition, ushahidi wote uliopatikana kwa lie detector hautatumika mahakamani.
 
Hii ni PR tu. Hakuna kitakachofanyika hapa

Bro wewe kwa mtazamo wako ungeshauri nini kifanyike, maana hadi hapo kwangu mimi naona hizi hatua ni chanya na hazijawahi kutokea Afrika yote. Kwanza kabisa na ujuavyo mifumo na uhuru wa mihimili Kenya, rais hawezi akakurupuka na kuwafuta watu kwa mpigo au kuwafunga, lazima hatua za kisheria zihusike.

Watu wote hawa wametiwa ndani, leo hii wametimia 43 na wamenyimwa dhamana kwa kigezo kwamba wao ni threat to national security, kesi zao zimechunguzwa kwa ushirikiano wa NIS, na bado kuna wengine ambao wapo njiani kwenda jela, mahakama imegoma kuwaskliza na imeahidi kutenda haki, kama alivyosema yule jaji mkuu kwamba 'mood of the country must be considered'.

Wakuu wote wa manunuzi wamewekwa pembeni kutathminiwa upya, watachunguzwa wote kila wanachomiliki, maisha yao na jamii zao, watapitia mifumo ya kisayansi ya kugundua na kuumbua kama mtu anazungumza uwongo, kitu ambacho hakijawahi kutokea Afrika yote.
Sasa hapo labda na wewe ungeshauri humu kipi unahisi kinakosewa na hatua zipi zingekua bora, maana hawa wote wanaokamatwa wametajwa kwa nji moja au nyingine, hauwezi ukamkamata mtu ambaye hajatajwa au kuhusishwa, hiyo itakua haujamtendea haki.

Ni vizuri tukaunga mkono jitihada pale zinaonyesha kufua dafu, na tusiige ukurupukaji wa majirani zetu Tanzania, juzi 1.5tr zimekwapuliwa huko, hawataki zijadiliwe bungeni ambapo ndio muhimili wenye uwezo huo, kila wakiulizwa wanasema wanapigana na ufisadi, mara wamebuni mahakama ya mafisadi, leo hii sijui hiyo mahakama inafanya kazi gani maana hamna matunda. Awamu hii yao ya tano muhula wake wa kwanza umesalia mwaka mmoja warudi kwenye uchaguzi sijui watatumia nini kujinadi kwa watu maana hamna jipya ila matamko na visasi.
 
Asante kwa kuniuliza kuhusu mtazamo wangu: Kwa ufupi, Uhuru ambaye nilimpigia kura, ni mtu ambaye hawezi kupigana na ufisadi. Kile anachotaka ni mijisifa tu - Hakuna lingine. Kuna tofauti gani kati ya anayofanya sasa hivi na kile alichokifanya hapo 2015? Zote zake ni sifa tu. Na ukishagundua hili, utakereka sana na sarakasi zake hizi za kipumbavu.

Sera ya laptop kwa watoto ni sera ya sifa. Baada ya kuambiwa hapo mbelini kuwa hii ni sera mbovu, aliendelea nayo kwa kuwa ingempa sifa ya "AFRIKA." Sasa iko wapi sera hiyo?

Sera ya Open boarders ni sera ya Sifa

Mambo ya handshake ni mambo ya sifa

Kukurupuka na kuwatumia Tanzania Rambirambi wakati wa ajali ya watoto wa shule ni sera ya sifa tu. Wakati Wafuasi wa Jubilee walizama kule Ziwa Nakuru, mbona hakutuma rambirambi zake? Wakati wa mkasa wa Patel Dam, mbona alinyamaza hadi wananchi walipokasirika

Baada ya wizi wa wakati wa Waiguru, ni nini alichokifanya ili kuweza kusimamisha wizi katika NYS? Alikuwa wapi hizi siku zote?

Tatizo ni kuwa mahakama inafanya mambo na Herd Instinct. Hamna ushahidi kuwa wakitoka nje watahujumu uchunguzi. Hamna ushahidi ya kuwa watatoroka wala ni hatari kwa usalama wa watu. Ikiwa watakwenda kwenye High Court kuomba rufaa, basi watapewa.

Kumbuka kuwa mood of the country ni kulynch mtu. Ushahidi unaotokana na lie detectors haukubaliki kule marekani ambampo chombo hicho hutumika.

Watu arobaini na wanne waliiba 400 Million. Kwani zile 8.5 Billion ziko wapi? Huoni huu ni mchezo tu? CBK ilikuwa wapi?

Kile kinachohitajika ni kwanza uhuru awache tamaa ya kupendwa na kupewa mijisifa.

La pili, katika kupigana na ufisadi, ni sharti mambo kadhaa yafanywe:

1.) Mahakama iwe "revisited"
2.) Nguvu za EACC zipunguzwe hadi bare minimum na majukumu hayo yapewe CID. Kuwe na kitengo cha Economic Crimes Division
3.) Kuwe na Mapinduzi kwenye Utumishi wa Polisi.
4.) Kuwe na mapinduzi kwenye Auditor General Office
5.) Kuwe na mageuzi kwenye KRA
6.) Kuwe na Internal Audits Kila mwezi kwenye kila Wizara, Kitengo Cha Mahakama, Kitengo Cha Bunge, na Devolved Units Zote
7.) Serikali iwe proactive kutafuta kesi za ufisadi na isiwe ikingojap mabilioni zikishaibwa ndio kuleta drama na hype.

Wacha niulize, kuna kesi ngapi za ufisadi ambazo hivi sasa ziko kotini? Mbona haziendi kwa wepesi kama kesi hii?

Cha maana ni kuwa: ikiwa wakenya tutakuwa tukisherehekea hype kama hizi, tutazidi kutafunwa kama wajinga. Wizi unaendelea kila pahali katika serikali hii. Tunayoyaona tu ni kutufanya tusiwe na mapinduzi. Kama vile ukila nyama unamtupia mbwa mifupa.
 
Kuna jinsi naona hatujaelewana, binafsi sizungumzii ya hapo awali, ni wazi na bayana rais Uhuru hajaonyesha ubavu wa kupambana na mafisadi, ndio mojawapo wa kitu kilichonitamausha kwenye serikali yake hii. Japo pia sisi kama Wakenya hatujaonyesha nia ya kushinda vita dhidi ya ufisadi, kila mmoja wetu kwa njia moja au nyingine amezembea, unakuta mtu kama Waiguru aliyetemwa kwa ufisadi anachaguliwa kuwa rais wa kaunti, yaani tuna hulka ya kuwaenzi wanaotajwa kwenye tuhuma za ufisadi.
Unakuta watu wanateuliwa kupitia mchujo mkali lakini wanaishia kuwa mafisadi. Ni bora pia kama nchi tuwe tayari, sio kuelekeza tu vidole vya lawama.

Lakini nilikua nazungumzia kuhusu matukio ya hivi karibuni, nini kifanyike tofauti na kinachoendelea, kwamba hao waliokamatwa ulitegemea hatua zipi zifuatwe tofauti na zinazofuatwa.
 
Back
Top Bottom