Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,646
- 35,981
Habari waungwana!
Kwa mujibu wa katiba yetu Tanzania ni nchi ya kijamaa. Ukisoma sura ya kwanza utaliona hili.
Ila misingi ya ujamaa ni kuwa mbali na rushwa, ufisadi na wizi wa mali za umma jambo ambalo tuko kinyume nalo.
Wizi upo
Ufisadi upo
Rushwa ipo na
Unyonyaji upo.
Unyonyaji ndio baba wa ufisadi, rushwa na wizi wa mali za umma.
Hebu fikiria mtumishi wa umma mmoja ndani ya taasisi moja analipwa milioni 5 huku mwingine analipwa laki 3. Je,huo sio unyonyaji?
Je, anayelipwa milioni 5 hataona kuwa ana haki zote za kuendelea kumnyonya huyu anayelipwa laki 3 kwa kujilimbikizia mali zaidi kwa njia zisizo halali?
Je, huyu anayelipwa laki tatu hatachukua rushwa kwa mwananchi ili file lake likae mbele ahudumiwe haraka?. Ni nini kitampa hofu huyu mtumishi asichukue rushwa?
Kwa nchi ya kijamaa ni halali kiongozi kutembea na msururu wa magari 50 yenye thamani ya juu huku ndani ya nchi hiyohiyo watoto wanakaa chini ya sakafu iliyotoboka baadhi ya shule?
Dar es Salaam nimepita shule kadhaa nimebaini kuwa kuna madarasa ya primary, darasa moja linachukua wanafunzi zaidi ya Mia kwa wakati mmoja. The same time mbunge wa hilo jimbo analipwa zaidi ya milioni kumi. Huo sio ukabaila na unyonyaji?
Kama watunga sheria wabunge pamoja na mawaziri wao wanakubali unyonyaji je, ufisadi, rushwa na wizi utaisha?
Dawa ya kukomesha rushwa, ufisadi na wizi Serikalini na taasisi binafsi ni kuuondoa rasmi mfumo wa kikabaila na kibwenyenye na sio kuunda taasisi za kupambana na hayo matatizo.