johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,853
- 141,785
Tatizo la rushwa katika idara za kodi siyo jipya na lina historia ndefu na msingi wake ni wafanyabiashara kutotaka kulipa kodi halali.
Lakini pia kuna watoza ushuru ambao sio waaminifu na waliojawa na tamaa ambao hulazimisha kupewa rushwa.
Wakati awamu ya pili inaingia madarakani Sweden ilitoa msaada wa kujenga chuo cha kodi pale mikocheni kikiitwa Institute of Tax Administration ( ITA).
Chuo hiki kilikuwa ni maalumu kwa ajili ya wafanyakazi kufundishwa maadili ya kazi pamoja na mbinu mpya za ukusanyaji pale inapolazimu, lakini zaidi ni kuwafanya watoza ushuru wawe wabobezi katika utendaji wao.
Wakati ule taaluma ya kodi ilikuwa ikifundishwa pale IFM lakini ubobezi ulipatikana ITA.
Kwa sasa ITA imebadilishwa na kuwa chuo cha kibiashara na kwahiyo watumishi wa TRA wanakosa sehemu sahihi ya kuimarisha mbongo zao na kufanya rejea ya uadilifu na utendaji wao mara kwa mara.
Kutoza ushuru ni zaidi ya kukusanya kodi, kuna falsafa yake hata kwenye maisha ya kawaida ya mfanyakazi. Ndio maana maana makamishna karibia wote walioteuliwa nje ya mfumo au malezi ya kikodi walifeli. Kwa mfano Sanare aliyetoka ATC wakati ule, Kitilya aliyetoka TBL, Bashe aliyetoka Barclays bank na hata hawa akina Maswi, Mpango na Kadata wa awamu ya 5.
Kutoza ushuru ni tofauti na kuwa bank teller au afisa mikopo, tax collection inahitaji kubalance matumizi ya nguvu na akili ili vitumike kwa pamoja. Wakati TRA inaanzishwa July 1996 mtoza ushuru mmoja alikataa kuvaa koti na tai akidai kiutamaduni mtoza ushuru anapaswa kuvaa kaunda suti, hao ndio watoza ushuru!
Watoza ushuru wana lugha yao kama ambavyo wafanyabiashara wana lugha na hicho ndio kilichofundishwa pale ITA enzi zile.
Binafsi nimeshangaa kusikia takribani makampuni 17,446 yamepeleka financial statements wakideclare profit ndogo kule TRA at the same period profit kubwa kwenye banks zao wanakopewa mikopo.
Nimejiuliza hivi hiki chuo cha kodi cha sasa huwa kinafanya tafiti kweli au wanasubiri hadi ofisi ya Rais iingilie kati?
Itaendelea............
Naunga mkono pendekezo la waziri wa fedha la kuunda tume.
Maendeleo hayana vyama!