Rushwa TANROADS: Magufuli atangaza vita

Majoja

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
612
186
Na Richard Makore
NIPASHE ya 6 Sept 2011

Waziri wa Ujenzi ,Dk John Magufuli amesema kitengo cha Manunuzi(Procurement) Makao Makuu ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kinanuka kwa rushwa na kutangaza kukivunja kwa maelexo kuwa kimeendelea kitia hasara serikali.
Dk Magufuli alitangaza hatua hiyo jana jijini Dar es salaam wakati mkutano wa wakandarasi (na wahandisi) uliofunguliwa na Rais Jakaya Kikwete.
Alisema watumishi wa kitengo hicho wanaongeza gharama katika miradi ya ujenzi na kuongeza kwamba hivi sasa kilometa moja ya barabara inajengwa kwa Sh bilioni 1.8 huku barabara ikiwa chini ya kiwango.

Well done Magufuli, sasa tukupe hint:
Mradi wa nyongeza Bodoma Manyoni-kilometa 16 kwa Tshs bilioni 32-Mkandarasi Estim(Bilioni 2 kwa kilometa)
Mradi wa Msata-Bagamoyo-kilometa 64, Tsh bilioni 105-Mkandarasi Estim(Bilioni 1.6 kwa kilometa)
Kuna makandarasi Tanroads ni sitting room.

Mifano mingi tu,na ni urithi wa Mrema wa TANROADS, Mfugale na Magufuli mnakazi kwelikweli kusafisha uozo.
 
Mpaka nimefika hapa nimeweza kumsikia mtu m1 tu Tanzania nzima ndo alitamka kutokumkubali mh.Pombe...nilimshangaa sana mpaka udenda ukanitoka,loh!!
 
Yah jana kaongea kwa kujiamini sana na akasema kitengo cha proquamenti ndani ya tanroads kifumuliwe haraka sana!
 
Yah jana kaongea kwa kujiamini sana na akasema kitengo cha proquamenti ndani ya tanroads kifumuliwe haraka sana!

chama dume, chama chenye watu, kina hazina ya vichwa, muwe wapole mapaka mtapenda
 
well done magufuli. pamoja na mapungufu yako lakini you are the best (i do not know if is among the worse, but you are good). Huyo kiazi hapo juu yako sioni hata anachokifanya.
 
Action speaks louder than words. Magufuli fanya kweli isiishie kwenye mikutano tu. Tunataka tuone kama tulivyoona kwa Mramba na wenzake!
 
Nadhani Mh. Rais anatakiwa kumpa ushiriakiano wa hali ya juu sana Dr Pombe Magufuli. Kwanini? Kwanza ndiye Waziri pekee naye muona anaweza kumwambia Rais ukweli bila kumficha tena mbele ya kadamnasi; Pili, mambo aliyotakiwa Mkuu kuyaongea, Dr Pombe anaye ongea kwa niaba yake; Tatu, ni waziri pekee ambaye anamfundisha hata Rais jinsi ya kufanya kazi. Ukifuatilia hotuba yake pale anaposema " Nakuomba Rais mambo mengine madogo madogo yakija kwako, uyasikilize na uyaweke pembeni usiyafanyie kazi, tuachie sisi tushughurike nayo. Hapo hakuna ubishi kwamba Mkulu anapewa somo kuwa ashughulike na mambo makubwa na mazito ya kitaifa, haya ya wavamizi wa barabara na mabango ya matangazo na vituo vya mafuta si size yake, ni madogo sana. Hongera magufuri, kwa kweli Rais inapaswa afahamu, huyu Dr anaibeba sana Serikali ya CCM.
 
Kwa jinsi alivyoshangiliwa , watuwamemkubali sana tu.
 
Action speaks louder than words. Magufuli fanya kweli isiishie kwenye mikutano tu. Tunataka tuone kama tulivyoona kwa Mramba na wenzake!
Magufuli has the sincirety and passion to work positively.
Lakini Taasisi kama TANROADS zilikuwa safi sana kabla ya Mrema, itachukua miaka kuisafisha, maana rushwa pale ilikuwa ndo pake.
 
Back
Top Bottom