Rushwa: Tamu na Chungu Yake

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
732
Rafiki yangu mmoja hakusita kutamka wazi kuwa anaomba rushwa iendelee. Nikamuuliza kulikoni? Naye akasema "Wewe unafikiri kama polisi-trafiki watafuata sheria zote, ni magari mangapi yatatembea barabarani?" Bila shaka kuna unafuu alioupata katika kutoa rushwa.

Ni kweli kuwa kuna watu wanapata unafuu wanapotoa rushwa. Lakini ni kweli pia kuwa kuna watu wengi zaidi wanaumia kwa sababu ya hao wachache wanaotoa rushwa. Tukichukua mfano wa rafiki yangu, ni wangapi wanakufa kwa ajali za barabarani kwa sababu ya polisi-trafiki wanaopokea rushwa?

Lakini tujiulize upande mwingine, ni kweli kuwa wote wanaopokea rushwa ni kwa sababu ya tamaa ya kuwa matajiri? Si ni hakika kuwa kuna wengine wanapokea rushwa ili watoto wao wapate chakula cha siku hiyo tu? Naomba nisimamie ninavyoamini kwamba, kwa kiasi kikubwa, mfumo mbovu wa maslahi kwa watendaji wa serikali na umma unasababisha rushwa.

Rushwa ina tamu zake. Mwenye kutoa akipata huduma haraka au kupata haki ambayo hakustahili hufurahi; hiyo ni tamu kwake. Anayekosa huduma au kunyimwa haki yake huchukia; naye huyo ni chungu yake.

Naleta kwenu tujadili, utamu na uchungu wa rushwa. Vile vile tupendekeze kwa viongozi wetu namna ya kupunguza rushwa serikalini na mashirika ya umma.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom