Rushwa nje nje uchaguzi Wazazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rushwa nje nje uchaguzi Wazazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jodeny, Oct 30, 2012.

 1. Jodeny

  Jodeny JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 202
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi mambo yameanza kuwa moto uchaguzi wa wazazi Dom na waya zilizopatikana zinasema mgombea nafasi ya mwenyekiti taifa, Abdalla Bulembo amekurupushwa na maofisa wa TAKUKURU akijiandaa kumwaga fedha. Jamaa muda mrefu walikuwa wakifuatilia nyendo zake kutokana na kumwaga fedha.

  Nyuzi zinapasha kuwa anafadhiwa na Mtandao wa mafisadi wanaowania urais mwaka 2015.

  Update: Soma post hii - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/347009-rushwa-nje-nje-uchaguzi-wazazi.html#post4935227
   
 2. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  mkuu kwani we hujui kuwa hiyo sasa ndo style ya kupata uongozi kupitia chama tawala? walianza kinamama wakaja watoto na sasa wanamalizia madingi.usipoteze muda wako kuwafuatilia hao kwani hiyo kitu sasa hivi ni ruksa ndani ya chama.
   
 3. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Wamemaliza mnada wa vijana sasa ni gulio la wazee
   
 4. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,402
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kama fisadi atapitisha kugombea urais kupitia CCM huo utakua ndio mwanzo wa mabadiliko ya kisiasa nchi hii!
   
 5. p

  politiki JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  jamani hata hawa wazee nao wamo ni aibu kubwa, sasa ndani ya ccm ni nani atakayemuonya mwezake yaani rushwa na
  CCM ni kama watoto mapacha. jk kila siku anatangaza vita dhidi ya wala rushwa inaelekea kabla ya kuja kwenda nje ya serikali inabidi aanze ndani ya chama chake kwanza kabla hajaja huku nje kuimba wimbo wa kupambana na wala rushwa.

  hii ni ndio legacy ya uongozi wa jk ndani ya ccm chama cha wala rushwa.

  kingine ni huyu mdudu anaitwa Takukuru yaani wananchi wanalia nchi nzima kuhusu rushwa ndani ya chaguzi lakini mpaka hii leo imeshindwa hata kumfikisha mtu mmoja mahakamani na kufankiwa kujenga hoja na mhusika kufungwa.
   
 6. m

  msemakwelii JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 217
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nini cha kukushangaza mtu wangu, juzi kati Jk katangaza kuwa huo ndio utaratibu wa kupata uongozi Chama Cha Mapenzi, Wanaume wanatoa Pesa Wanawake Ng_n_ Kamataaaaaa hao , Kwetu ni kusema No Uchaguzi 2015
   
 7. Jodeny

  Jodeny JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 202
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
   
 8. Jodeny

  Jodeny JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 202
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Takukuru kamata huyooo ...kakimbia darasa la QT
   
 9. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  sasa wamemkurupusha au wamemkamata?
   
 10. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #10
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  kwa upumbavu wetu sisi wapigakura wa Tanzania na kwa unafiki wetu, fisadi atapitishwa na CCM kwa pesa zake, CCM watamnadi na kumsafisha kila doa, na tulivyo mbumbumbu sisi tutamshangilia na kumpa kura za kishindo kama tulivyofanya 2005.

  baada ya hapo ndipo 2015-2020 tutafuatia kulia na kusaga meno kama tunavyolia leo
   
 11. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,402
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hata mimi nimekuwa na mashaka na wapiga kura! lakini ivi kweli mtu kama EL anaweza kupitishwa kweli mimi naona
  ni upepo tu huu!!
   
 12. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,402
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Wamkamate wapi, watasema hawana ushahidi sana2 wamemtonya aondoke hali siyo!!!!
   
 13. bhikola

  bhikola JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 457
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  huyo wamemwonea tu, atakuwa siyo mwenzao ndiyo maana.
  mbona badwel sijui gudwel bado anakula posho zetu? mbona wale vijana waliogawa shekeli mbele ya jk hawakusemwa, mdona da sofi lion aliachwa akatamba mpaka na mipasho juu
  wamuache na yeye apunguze alizotuibia
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,611
  Trophy Points: 280
  Rushwa nje nje uchaguzi Wazazi

  Mwandishi Wetu, Dodoma
  Mwananchi

  WAKATI uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ukifanyika leo, suala la rushwa, makundi na wajumbe kutaka kuzipiga yalitawala jana.

  Uchaguzi huo wa wazazi ndiyo wa funga dimba la mfululizo wa chaguzi za chama hicho tawala kuanzia ngazi za shina tangu Aprili.
  Tuhuma hizo za rushwa zimejitokeza licha ya juzi wagombea mbalimbali kukaririwa wakiyakana makundi ambayo yamekuwa yakitajwa kuwa na ajenda maalumu ya kusaka urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kupitia chama hicho.


  Kampeni na rushwa

  Mmoja wa wajumbe kutoka mkoani Iringa alimwambia mwandishi wetu kuwa tayari baadhi ya wajumbe wanaoonekana kuwa na msimamo mkali wamekuwa wakipewa Sh100,000 kila mmoja wakati wajumbe wengine wamekuwa wakihongwa kati ya Sh40,000 na 70,000.

  “Nikimwona Rais Jakaya Kikwete nitamwambia. Hali hii siyo nzuri na haiwezi kuvumiliwa. Kama alivyosema juzijuzi hapa nilimsikia, lazima achukue hatua, la sivyo chama chetu kitakufa,” alisema mjumbe huyo ambaye aliomba asitajwe jina.

  Katika hatua nyingine, makundi ya baadhi ya wajumbe waliokuwa wameketi katika moja ya baa maarufu mjini Dodoma, juzi usiku walitimka mbio baada ya kuona gari likiegeshwa pembezoni mwa baa hiyo.
  Wajumbe hao waliokuwa kwenye harakati za kupanga mikakati ya kuzunguka katika nyumba za kulala wageni kwa ajili ya ‘kuonana’ na wajumbe, walitimka wakidhani kuwa gari hilo lilikuwa na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

  Wagombea wanaowania uenyekiti, John Barongo na Abdallah Bulembo juzi, kwa nyakati tofauti walikanusha kuwa na maslahi na makundi yanayodaiwa kushiriki katika vitendo vya kutoa rushwa katika uchaguzi huo unaofanyika leo. Mgombea mwingine wa nafasi hiyo, Martha Mlata alikataa kuzungumzia uchaguzi huo.

  Uchaguzi huo, unahitimisha uchaguzi wa jumuiya tatu za chama hicho, baada ya ule wa UWT na UVCCM ambazo zilizua malalamiko kutokana na kutawaliwa na madai ya rushwa.
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifunga mkutano wa UWT na baadaye alipofungua ule wa UVCCM, alikemea vitendo hivyo na kueleza athari za rushwa katika chaguzi za chama.

  Mchuano wa wabunge
  Kama ilivyokuwa katika uchaguzi wa UWT, mchuano mwingine mkali unaonekana katika kinyang’anyiro cha ujumbe wa Nec, huku kukiwa na idadi kubwa ya wabunge wanaowania nafasi hiyo.
  Majina 16 yamepitishwa kuwania viti vitatu vya Nec kwa upande wa Tanzania Bara, wakati kwa upande wa Tanzania Visiwani majina yaliyopitishwa ni saba kugombea nafasi mbili.

  Miongoni mwa wanaowania nafasi tatu Bara ni Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu, Stella Manyanya na Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu.

  Pia wamo wabunge ambao majimbo yao yapo kwenye mabano Said Bwanamdogo (Chalinze), Vita Kawawa (Namtumbo), Murtaza Mangungu (Kilwa Kaskazini) na Mbunge wa zamani wa Viti Maalumu, Esther Nyawazwa.

  Wengine katika kundi hilo ni Norad Kigola, Priscilla Mbwaga, Dk Salim Chikago, Jeremia Wambura, Bernard Murunya, Thobias Mwilapwa, Paulo Kirigini na Clementina Mollel.

  Kutoka Zanzibar, wanaowania nafasi mbili za Nec ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Perera Ame Silima, Abdulla Khamis Feruz, Ali Suleiman Othman, Fatuma Abeid Haji, Panya Ali Abdalla, Twaha Ally Muhajir na Hassan Rajab Khatib.

  Pia mkutano wa leo unatarajiwa kumchagua Makamu Mwenyekiti, nafasi inayowaniwa na Hassan Rajab Khatib, Ali Issa Ali na Dogo Iddi Mabrouk.
  Utawachagua pia wajumbe wa Baraza Kuu la Wazazi na wawakilishi wa jumuiya hiyo katika mabaraza ya UVCCM na UWT.

  Vijembe vya kampeni
  Kampeni zimekuwa zikipamba moto kadri muda wa uchaguzi unavyokaribia na mbinu mbalimbali zimekuwa zikitumika ili kujihakikishia ushindi.
  Magari mengi yamepambwa picha nyingi za wagombea, wapambe wanapita sehemu mbalimbali kuomba kura na kuta za uzio wa ofisi za CCM zimechafuka kwa picha za wagombea.

  Ushindani mkubwa unaonekana kuwa baina ya Barongo na Bulembo ambao jana walikuwa kivutio kikubwa walipokutana katika ofisi za CCM Makao Makuu, Dodoma ambako walikumbatiana kisha kuanza kurushiana vijembe.
  Bulembo alisema: “Nilipomkuta anachukua fomu, nilimwuliza mwalimu wangu huyu (Barongo) kwamba nilidhani kwamba sasa unaniachia nikutue mzigo, kumbe bado tena na wewe unagombea?”

  Barongo alimjibu akisema: “Hilo haliwezekani kabisa, ujue ninyi bado watoto hamjakomaa bado mnahitaji kuongozwa, kwa hiyo wewe tulia kwanza muda mwafaka ukifika nitakukabidhi.”
  Jana asubuhi, Bulembo alifika katika Viwanja vya Bunge kuomba kura kwa baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa mkutano mkuu wa jumuiya hiyo.
  Muda mfupi kabla ya wabunge kuingia ukumbini, Bulembo alikuwa nje ya lango kuu la kuingilia kwenye ukumbi wa Bunge na kila mbunge aliyejitokeza alimsalimia kisha kuomba kura kwa wale ambao ni wajumbe hao.

  Mlata jana kwa muda mrefu hakuonekana katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM na taarifa zinasema huenda alikuwa akihudhuria kikao cha Baraza Kuu la Jumuiya hiyo kilichofanyika jana katika Chuo cha Mipango.
  Licha ya kutokuwapo kwake, kulikuwa na vijana wachache waliokuwa wamevalia mabango makubwa yenye picha yake, vifuani na kwenye migongo yao wakimpigia kampeni.

  Wafuasi nusura wazichape

  Wakati Bulembo na Barongo wakirushiana vijembe kwa furaha, watu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wao nusura wachapane makonde walipokuwa wakiimba nyimbo za hamasa CCM Makao Makuu.
  Wafuasi hao jana walikuwa wakizunguka wakiwa na mabango yenye kuwanadi wagombea hao katika ofisi hizo kati ya saa sita na saa nane mchana huku wakiimba nyimbo za hamasa.

  Hali hiyo ilisababisha kutosikilizana katika eneo hilo, hivyo kuwalazimu maofisa wa CCM kuviamuru kuondoka na kuelekea katika mbele ya jengo la vikao vya NEC maarufu kama White House. Viliitikia wito na kwenda huko ambako viliendelea kuimba nyimbo za hamasa.

  Wakati vikiwa katika eneo hilo, wafuasi hao walianza kurushiana maneno makali kwa huku kila upande ukidai kufanyiwa rafu na upande mwingine, hali iliyozua tafrani iliyodumu kwa zaidi ya dakika 20.
  Hata hivyo baadhi ya makada wa pande hizo mbili, walitumia busara na kuwatuliza na kila kikundi kuelekea upande tofauti na kuhitimisha shamrashara hizo.

   
 15. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  yaani rushwa imehalalishwa ccm, na watu wana price tag, na pumgufu unaongea.
   
 16. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #16
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ccm rushwa sio dhambi na ni haki ya mgombea na mpiga kura kwa kifupi jk na wenzake ndio walihalarisha leo hii ni full shangwe unategemea takukuru itatokomeza rushwa kama ccm wanapokea rushwa nje nje?
   
 17. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #17
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Amwambie nani, Kikwete huyu wa EPA na Suti, huyu huyu aliyempa Hu Jintao kusini yetu.

  Akishamwambia itakuwaje, sana sana ataishia kumwambia sasa na wazazi mkichaguana kwa rushwa si nchi imekwisha, halafu ataishia hapo hapo.

  Na magamba wengi wanafiki, wanaolalamika ni wale ambao wamepata mgao pungufu au mgao umewapitia pembeni.
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,611
  Trophy Points: 280
  Sana sana DHAIFU ataishia kulalamika tu na kubwabwaja bila hatua zozote za kupambana na rushwa iliyokithiri ndani ya magamba na Serikali. Dr Slaa hakukosea kabisa aliposema, "Kumchagua Kikwete katika uchaguzi wa 2010 ni janga kubwa la Taifa."

  Janga hilo tunaliona kila kukicha.


   
 19. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nchi imeoza hii, Hakuna pa kukimbilia. Itabidi tuka mkodi Putin aje kutufundisha jinsi ya kupambana TZ-Oligarchy
   
 20. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #20
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,745
  Likes Received: 17,824
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo Kamanda, kama rushwa zingekuwa zinatungisha mimba, hawa wazee wangekuwa na mimba kubwa sasa baada ya chaguzi
   
Loading...