Rushwa ndani ya mchakato wa kura za maoni Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Mangungu

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
2,680
2,000
Kwenu viongozi wa CCM Taifa!

Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yetu ya Ulinzi na Usalama,Mwenyekiti wa CHAMA Cha Mapinduzi na Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Mh Dkt Jonh Pombe Joseph Magufuli!!

Kwanza nakupa pole,na pili kabisa,napenda kusema mimi ni mwana CCM lia lia kabisa,ambaye nipo tayari kufa kwa sababu ya Chama Changu na Serikali yangu!

Mh Mwenyekiti,katika kura za maoni majimboni kumekua na utoaji wa rushwa wa wazi wazi kabisa! Kwa sasa naomba nizingumzie Jimbo la Hanang Mkoani Manyara!

Mh Mwenyekiti,Jimbo hili limeongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mh Fredrick Sumaye kwa miaka 20,baadae akamwachi Mama Mary Nagu ambaye nae yuko pale kwa miaka 25 sasa, na ndiyo mbunge Mstaafu wa Jimbo hilo!

Kwenye kura za maoni waliokua wanachuana ni Mary Nagu, George Bajuta na Samwel Hayuma! Mh Mwenyekiti huyu George Bajuta katoa rushwa sana kwa kula mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi, hadi kupelekea kushinda kura za maoni kwa za ubunge wa Jimbo la Hanang

Mh Mwenyekiti,nakuomba sana haki itendeke,na ukizingatia kwamba wewe ni mpinga rushwa kweli kweli, kwenye vikao vyenu vya CC vinavyoanza Jumanne, kila aliyetoa rushwa na ikathibitika hivyo,afutiwe matokeo nakupewa mtu mwingine..

Mh Rais hii itatia tawira kwamba ni kweli wewe unachukia Rushwa,na hii itapelekea sisi wanyonge,tusio kua na pesa tuamini ya kwamba kweli,Rushwa ni adui wa maendeleo.

Mh Rais,athali za rushwa nikupata kiongozi ambaye hapendeki kwa wananchi au Jimbo likachukuliwa na upinzani! Kumbuka ya mwaka 1995 ya Dkt Slaa na Jimbo la Karatu..

Mh Rais kwa maoni yangu haya,naomba suala la Rushwa liwe ndiyo ajenda kuu kwenye kamati kuu!

Mh Mwenyekiti nakutakia kazi njema
 
Wajumbe

Senior Member
Jul 26, 2020
136
500
Ushauri: CCM irudishe utaratibu wa wanachama wote kupiga kura, maana kwa mfumo huu majizi yanamudu kuyapa rushwa majumbe kwa kuwa idadi ni ndogo. Na katika maeneo mengi, wanaccm wasio wajumbe hawakubaliani na jinsi mchakato ulivyoendeshwa na pia hawawakubali wagombea wenye kura nyingi. Inavyoonekana hapa na hoja wa wivu wenzetu wamempa kura kwa kuwa walipewa pesa, hivyo mgombea ataungwa mkono na wanachama wachache sana
 
peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
1,786
2,000
CHADEMA imejitahidi kuteua wanawake wengi kugombea kwenye majimbo .Ni mfano wa kuigwa na Chama tawala.ila Nagu Sasa Ni muda wa kupumzika
 
Jose Mmassy

JF-Expert Member
Jul 30, 2020
1,765
2,000
Ushauri: CCM irudishe utaratibu wa wanachama wote kupiga kura, maana kwa mfumo huu majizi yanamudu kuyapa rushwa majumbe kwa kuwa idadi ni ndogo. Na katika maeneo mengi, wanaccm wasio wajumbe hawakubaliani na jinsi mchakato ulivyoendeshwa na pia hawawakubali wagombea wenye kura nyingi. Inavyoonekana hapa na hoja wa wivu wenzetu wamempa kura kwa kuwa walipewa pesa, hivyo mgombea ataungwa mkono na wanachama wachache sana

Umewaza Kama mimi
 
M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
12,515
2,000
Mh Mwenyekiti,nakuomba sana haki itendeke,na ukizingatia kwamba wewe ni mpinga rushwa kweli kweli, kwenye vikao vyenu vya CC vinavyoanza Jumanne, kila aliyetoa rushwa na ikathibitika hivyo,afutiwe matokeo nakupewa mtu mwingine..
kama mwana CCM mwenzako, nimekubaliana na yote uliyoyaandika isipokuwa hapo kwenye red... hapa comrade naona unaturushia pilipili machoni aisee!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom