Rushwa ndani ya CCM

Teamanaconda

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
602
564
Kuna vitendo vya rushwa vinavyoendelea ndani ya CCM hasa kwenye uteuzi wa wagombea wa serikali za mitaa inasikitisha sana, kuna huu mtaa ninapoishi mimi unaitwa Mtaa wa Muungano kata ya Goba wilaya ya Ubungo. Kuna mwenyekiti ambaye anamaliza muda wake ambaye ni wa CCM na wananchi wanampenda sana. Sasa mara ya kwanza kwenye kura za maoni jina lake kutoka CCM wilayani lilipita ila kufika CCM kata ya Goba wakamkata na wanachama wa CCM wa huu mtaa wakagoma kupiga kura ikabidi uchaguzi urudiwe na majina hakuna kwenda kata watu wakachagua hapa hapa mtaani.

Sasa katika uchaguzi wa marudio huyu jamaa ambaye jina lake lilikatwa akashinda kwa kura nyingi tu kuliko huyu mpinzani wake ambaye anahonga sana pesa huko kata, jana huyu aliyeshinda kwa kura nyingi CCM kata ya Goba wamemuita na kumwambia jina lake wamelikata kisa alivyoshinda kwanini wananchi walishangilia sana, hivyo huyu bwana ambay anatoa rushwa ndiyo jina lake limepita agombee, na huyu bwana aliepitishwa jina lake kimazabe jana amekodi muziki na amefanya sherehe kubwa sana hapa mtaani ya kushangilia ushindi.

Baada ya kufanyika uchunguzi imegundulika kuwa huyu bwana aliekatwa kilichomponza hajapeleka hela kule kata kuhonga kwa wajumbe ili wampitishe, hivyo basi wananchi wa huku jana wamekaa wameamua mgombea yoyote wa chama upinzani atakaye simama wanampigia kura wote, kuliko kumchagua mtu ambaye anatumia pesa kwa ajili ya kupata cheo cha uenyekiti wa mtaa maana wanajiuliza huyu mtu hii pesa atairudishaje?

Rais anahangaika kweli kudhibiti rushwa serikalini lakini kumbe rushwa inaanzia ndani ya chama chake cha Mapinduzi.
 
Noted mkuu! Hebu piga 113 au SMS ya lalamiko lako kwenda *113# Ok, natumaini utapata majibu mazuri zaidi toka TAKUKURU ulipo wapo.
 
Back
Top Bottom