Rushwa na Tanesco

Astrum27

Senior Member
Nov 28, 2016
143
215
WanaJF habari za asubuhi

Baada ya Serikali awamu ya tano kutoa offer ya umeme wanayodai ni sg 27,000/- maeneo mbalimbali, hawa wanaotumwa kuja unganisha huwa wanataka uwape na pesa pia, wanadai si rushwa ila ni wajibu wa kazi yao hasa Maeneo ya Arusha kabla ya kuunganishiwa umeme wamehalalisha kabisa nyongeza ya pesa (mimi naita Rushwa).

Naomba hoja hii ikiwezekana iwafikie Tanesco waweze toa mfumo wa kuripoti rushwa. Au kama wameamua halalisha malipo zaidi basi tunataka ilipwe benki nchi isikose mapato.

Ahsante
 
Tafuta ngazi sisi tuna haraka, tutakuacha kwenye giza! Hivi kwenye gari hawana ngazi? Au wanaandaa mazingira ya kitu kidogo?
 
WanaJF habari za asubuhi

Baada ya Serikali awamu ya tano kutoa offer ya umeme wanayodai ni sg 27,000/- maeneo mbalimbali, hawa wanaotumwa kuja unganisha huwa wanataka uwape na pesa pia, wanadai si rushwa ila ni wajibu wa kazi yao hasa Maeneo ya Arusha kabla ya kuunganishiwa umeme wamehalalisha kabisa nyongeza ya pesa (mimi naita Rushwa).

Naomba hoja hii ikiwezekana iwafikie Tanesco waweze toa mfumo wa kuripoti rushwa. Au kama wameamua halalisha malipo zaidi basi tunataka ilipwe benki nchi isikose mapato.

Ahsante
Ofisi za umma zinawanyonya wananchi kwa rushwa.
 
Usidhani kuwa hao Tanesco-Viongozi hawajui. Ukidhani hivyo, ni sawa na kuamini kuwa Aijipii alikemea rushwa kweli.

Ipo, inajulikana na wa kuanzia chini mpaka juu juu kabisa nje ya shirika.
 
WanaJF habari za asubuhi

Baada ya Serikali awamu ya tano kutoa offer ya umeme wanayodai ni sg 27,000/- maeneo mbalimbali, hawa wanaotumwa kuja unganisha huwa wanataka uwape na pesa pia, wanadai si rushwa ila ni wajibu wa kazi yao hasa Maeneo ya Arusha kabla ya kuunganishiwa umeme wamehalalisha kabisa nyongeza ya pesa (mimi naita Rushwa).

Naomba hoja hii ikiwezekana iwafikie Tanesco waweze toa mfumo wa kuripoti rushwa. Au kama wameamua halalisha malipo zaidi basi tunataka ilipwe benki nchi isikose mapato.

Ahsante
Tafadhali tupatie ushirikiano kwa kutoa taarifa kamili kwetu au TAKUKURU kwa hatua zaidi
 
Mie nimetegeshea kuna jirani zangu tumelipia pamoja tunasubiri kuletewa umeme siku akiletewa tu jirani nawafuata wakinizungua naondoka kimya kimya naenda TAKUKURU maana ushahidi ninao
 
Mie nimetegeshea kuna jirani zangu tumelipia pamoja tunasubiri kuletewa umeme siku akiletewa tu jirani nawafuata wakinizungua naondoka kimya kimya naenda TAKUKURU maana ushahidi ninao
Hauapaswi kushiriki kwenye mambo yasiyoruhusiwa kisheria tafadhali toa taarifa sasa kwetu au TAKUKURU kwa hatua zaidi
 
Tanesco tank bovu na viunga vyake Mungu anawaona na atawalipa !

Asema Mtumishi wa Bwana!

Mmewaacha wananchi gizani kwa muda mrefu sana Yani kuna taarifa nimepata watu wanasikitika sana kwa mnachowafanyia!

Tanesco tank bovu Mungu anawaona na atawalipa !

Asema Mtumishi wa Bwana!

Mmewaacha wananchi gizani kwa muda mrefu sana Yani kuna taarifa nimepata watu wanasikitika sana kwa mnachowafanyia!

Sijui kwanini hawatoi taarifa kwa mamlaka za juu kuhusu kero mnazowapa wananchi kwa kuwapa Giza muda wote!

TANESCO
 
Tanesco ni janga!! Ukifatilia utendaji wa Tanesco, ndio utajua kwa nini?! nchi yetu tunapiga hatua kwa mwendo wa kobe linapokuja suala la maendeleo!
Ni jambo la kusikitisha,!! Unapewa control number unaenda kulipia pesa nyingi tu! kwa ajili ya kuwekewa umeme, shirika wanakueleza kuwa watakuja kukuwekea umeme ndani ya siku sitini za kazi,hizo siku walizokuaidi zinaisha!! bila kuja kumuunganishia mteja umeme!!! Hawatoi taarifa yeyote kwa mteja kumfahamisha kama kuna tatizo lolote, mteja anakaa zaidi ya miezi mitano, bila kuunganishiwa umeme, na hakuna taarifa yeyote na pesa wameshachukua!!!
Shirika linajiendesha kijima sana, ukimsikiliza waziri anavyoongea kwenye vyombo vya habari unabaki unasikitika tu, majigambo mengi, takwimu nyingi ila kwenye ground ni zero kabisa,kama hapa dsm kumuunganishia mteja umeme mnashindwa uko vijijini si ndio aibu tupu?!! Imagine upo mjini miezi mitano huna umeme na umeshalipia, ni mateso. Ukifatilia wanaishia kuchukua number zako za simu na mtaa uliopo basi!hakuna feedback yeyote, hizo pesa mnazotoza watu wakati uwezo wa kusambaza umeme hawana!! Kwanini wasiweke utaratibu kuwa wakiwa tiyali kumuunganishia mtu umeme ndio alipie, kuliko kuchukua pesa ya mtu wanakaa nazo zaidi ya miezi mitano!! Mtu akiamua kuziweka kwenye mzunguko wake wa biashara zingemsaidia, kuliko huu unyang'anyi wanaoendelea kuutumia kupokea pesa za watu ilhali uwezo wa kuunganisha umeme hawana!! Shirika linajiendesha kijima sana, sijui kama lina afsa anaeshughulika na biashara, hio miezi mitano kwa hesabu za kawaida kama wangekuwa wamemuunganisha mtu uyu umeme kwa haraka, iyo miezi mitano angekuwa ametumia umeme kiasi kikubwa ameingizia shirika pesa na pia angekuwa amelipia tozo mbalimbali za serikali kupitia umeme ambao angekuwa ananunua kila mara!!
Shirika linatia aibu sana!! Hii inaonyesha ni jinsi gani watu waliopewa dhamana kuongoza shirika, wamelala usingizi wa pono!! Hakuna uwajibikaji, ukitaka huduma kwa haraka lazima utoe rushwa, ndio wakufanyie kwa haraka!! Ili ni tatizo usipotoa rushwa utasota kwenye giza mpaka ujute!! Ifike mahali mashirika kama haya wapewe wazungu, ili watufundishe namna ya kufanya kazi kwa weredi bila longo longo za sisi watanzania.
 
Tafadhali tupatie ushirikiano kwa kutoa taarifa kamili kwetu au TAKUKURU kwa hatua zaidi
Nyie tanesco mnakwamisha juhud za mh magufuli malalamiko.ya mdau ni kwali mnataka ushaidi gani wakati Mimi mwenye ni mhanga mnasumbua sana mara hamna usafiri au njoo na gari tutakupa fundi kweli ndo utaratibu huo iko siku rungu la awamu hii litakua juu yenu
 
Hauapaswi kushiriki kwenye mambo yasiyoruhusiwa kisheria tafadhali toa taarifa sasa kwetu au TAKUKURU kwa hatua zaidi
Dawa yanu tunaamini inachemka hamtoshi nyie ila yote ni kwa sababu hamna washindani wabiashara
 
Hauapaswi kushiriki kwenye mambo yasiyoruhusiwa kisheria tafadhali toa taarifa sasa kwetu au TAKUKURU kwa hatua zaidi
Tanesco mnazingua sijui shida yenu ni nini!? Nimepeleka form ya kuombanl umeme mwezi wa tatu sasa hakuna kila kitu.
 
Bila kutoa mlungula kwa wafanyakazi wa tanesco mambo hayaendi
Lasivyo utasubiri mpaka utakomaaaa
Wekeni vilainishi wazeee
Huo ndiyo ukweli...

TANESCO

Ova
 
Back
Top Bottom