Yes maana hujui hata majeshi siku hizi yanakuwa outsourced kwa makampuni binafsi.Mimi Sina exposure?
Hujui kwamba kitu kama bandari kuendeshwa na private sector Serikali haitakuwa na information yoyote as if itaenda kulala na kuacha mambo yajiendee.
Ndugu zangu, eleweni kwamba hivyi vyombo vyote vinavyo endeshwa na serikali, kama vingeendeshwa na private sector vina uwezo wa kuzalisha zaidi ya mara mbili ya vinavyo zalisha sasa. Serikali ina urasimu na ni ngumu kuendesha kitu chochote kile kibiashara.
Ndo maana wenzetu walio endelea waliyaona haya mapema wakaamua private sector ndo iwe engine ya uchumi.
Najua wanasiasa wengi hawapendi hizi shughuli ziendeshwe na private sector kwa sababu ya masilahi yao. Watakuwa wajumbe wa board, watakuwa wajumbe wa kamati, watatembelea hayo mashirika na kujipatia mpunga. Private sector ikichukua hawatapata hizo nafasi.