Tetesi: Rushwa kumlinda mjumbe wa baraza kuu UVCCM taifa

Wangooto

Member
Feb 1, 2013
20
5
Zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya kufanyika kikao cha Baraza Kuu la Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa. Ambapo imeelezwa kuwa kikao hicho kinatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 4/5/2019.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana wa CCM-Taifa kutoka Mkoa Fulani ambaye ameomba Jina lake lihifadhiwe ameeleza kuwa Pamoja na ajenda za kikao hicho kuwa nyingi lakini moja ya ajenda muhimu kwa baraza hilo ni Jumuiya hiyo kulinda hadhi yake na kujisafisha.

“Tunakwenda katika baraza kuu tunajua moja ya agenda ni kubariki maamuzi makini ya Baraza la Vijana Mkoa wa Rukwa ambalo liliketi mnamo tarehe 12/04/2019 pamoja na ajenda nyingine kwa pamoja wajumbe wa baraza hili waliazimia kuwavua nyazifa zote viongozi wawili ambao ni Ndg. Nyansio Gregory (Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa anayetokea mkoa wa Rukwa) na Ndg Buto Lubusi (Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Mkoa wa Rukwa), sababu ya makosa ya kimaadili na kijamii. Vijana hao wawili wamekuwa ni Vinara wa matendo ya Utapeli, kujifanya usalama wa Taifa, Kujipatia starehe za ngono kwakutumia Vyeo vyao kuanzisha makundi ndani ya Chama na Jumuiya kabla ya Uchaguzi kitu ambacho ni kinyume kabisa na kanuni ya Maadili ya CCM, Kuchukua pesa katika taasisi mbalimbali za Serikali kiulaghai kinyume na utaratibu” alimeeleza Mjumbe huyo ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe.

Alipouzwa mjumbe mwingine ambaye naye jina lake limehifadhiwa amesema kuwa “Si huyo tu Jumuiya hii ya Vijana katika Mkoa wetu imekumbwa na zahama sana kwani hata Mwenyekiti Ndg. Ramadhan Shabani ndio alitakiwa kuwa wakwanza kuwajibishwa kwani amekuwa akinufaika na matendo yao na ameshindwa kuiongoza Jumuiya sababu ya kutoshaurika. Lakini kwa wajumbe hao wawili zipo taarifa za uhakika kabisa kuwa wanakingiwa kifua na Kiongozi Mkubwa wa Chama hapa Mkoani na tayari wamejipanga kutoa rushwa ili kushawishi wajumbe wa baraza kuu kutoka mikoa fulani kupinga mapendekezo ya Baraza la Mkoa wa Rukwa katika Baraza kuu. Hata hivyo katika kulifanyikisha saula hili wanashirikiana pia na kiongozi Mkubwa tu wa Jumuiya pale Taifa ambaye na yeye anasadikiwa kupokea bahasha kutoka kwa kiongozi huyo Mkubwa wa Chama hapa mkoani.”
Aliongeza kwa hamaki sana… “Sisi tunashindwa kuelewa kwanini kiongozi huyu awatete matapeli na anamaslahi gani na hawa vijana ambao wameaminiwa lakini wameshindwa kuunganisha vijana na badala yake kuwavuruga na kuwaibia?”

Baadhi ya Vijana wameendelea kuunga mkono maamuzi ya Baraza la VIjana wa CCM Mkoa wa Rukwa na kudai kuwa hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao.
“Kuto wawajibisha Viongozi hao matapeli ni kuikosea heshima Jumuiya ya Jumuiya ya Vijana kwa ujumla na italeta mashaka ya kuamini kama kweli hili ni Jukwaa sahihi kwa Chama kuandaa viongozi wa Chama na Serikali” alinukuliwa mmoja wa makada vijana amliyefahamika kwa jina moja la Siza
 
Subiri wakina melikiory hussein and Co warudi dar wapumzike ziara ya magufuli, comments zitafika 1000 zote kukashifu upinzani na wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom