Rushwa katika uchaguzi CCM wajinasa wenyewe waziwazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rushwa katika uchaguzi CCM wajinasa wenyewe waziwazi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MTWA, Jul 23, 2010.

 1. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Jamani kazi iliyobaki rahisi na tamu ni Ubunge tu!!
  Wakati Mwenyekiti wa chama Tawala CCM alipokimbiza muswada wa sheria ya gharama za uchaguzi, leo CCM inazidi kujiingiza yenyewe kwenye tanuri lake. wengine tulitaraji kuwa ni tanuri la upinzani, endelea:

  SHERIA mpya ya Gharama za Uchaguzi, imeanza kuwabana wagombea wa CCM baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwakamata na kuwahoji watu sita wanaowania kuteuliwa na chama hicho kugombea ubunge katika uchauguzi mkuu utakofanyika Oktoba, mwaka huu.


  WanaCCM hao walikamatwa jana maeneo tofauti nchini wakati wanaanza kampeni za kuomba ridhaa ya kuteuliwa kukiwakilisha chama hicho kwenye uchaguzi mkuu ujao.

  Wagombea watatu wa ubunge na mmoja wa udiwani walihojiwa jana na bado wanaendelea kuchunguzwa na Takukuru mkoani Iringa baada ya kudaiwa kukiuka sheria ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010


  Mkoani Mwanza, Takukuru imemkamata Dotto Makambi akidaiwa kuchinja ngÂ’ombe kwa ajili ya kuwagawia nyama wapiga kura na pikipiki tano wilayani Sengerema, zilizohisiwa kuwa ni sehemu ya kampeni.

  Mkoani Kilimanjaro uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa kampeni hizo zinaambatana na ushawishi wa fedha huku baadhi ya wagombea waimekuwa wakiziendesha usiku hata kwenye nyumba za kulala wageni baa.

  Kutoka Dodoma uvumi ulienea jana asubuhi kuwa wapambe wa mgombea ubunge jimbo la Dodoma Mjini Adam Kimbisa wamekamatwa na kuhojiwa na taasisi hiyo ambayo hata hivyo baadaye jioni ilikanusha madai hayo.

  juzi Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa aliliambia gazeti hili kuwa wagombea waliovunja sheria ya gharama za uchaguzi wataanza kuchukuliwa hatua.

  Jijini Dar es Salaam utaratibu mpya wa wagombea hao kutembea pamoja na kunadi sera zao ulionekana kuwakera baadhi yao huku wagombea wa majimbo ya Segerea na Ukonga yaliyopo katika Manispaa ya Ilala wakiilalamikia kamati ya siasa ya wilaya hiyo kuwa imefanya maamuzi yanayopinga muongozo wa Nec.

  Chanzo: Mwananchi newspaper 23rd 07. 2010
   
Loading...