RUSHWA KATIKA UCHAGUZI 2010: CCM yawakamua wafanyabiashara Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RUSHWA KATIKA UCHAGUZI 2010: CCM yawakamua wafanyabiashara Arusha

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Sophist, May 22, 2010.

 1. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,083
  Likes Received: 1,729
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Kila mfanyabiashara atakiwa kutoa Sh. milioni 10

  [​IMG]Lowassa aongoza kamati ya kutembeza ?bakuli?


  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea "kuwakamua fedha" wafanyabiashara na wanachama wake mkoani Arusha kwa kuwachangisha mamilioni ya shilingi ili kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
  Kwa mkoa wa Arusha, uchangishaji huo ni wa pili baada ya Jumuiya ya Wanawake (UWT), wiki mbili zilizopita, nayo kuwachangisha wanachama wake, wakiwemo madiwani na wabunge wa viti maalumu, mamilioni ya fedha ambayo yalizua malalamiko makubwa kutoka kwa wanachama wa jumuiya hiyo.
  Na sasa malalamiko kama hayo yanatolewa na Jumuiya ya Wafanyabishara wa Arusha wakidai kuwa chama hicho, kwa kutumia kamati teule ya watu wanne iliyoundwa, kinawalazimisha kuchangia kiasi kikubwa cha fedha bila ya kuzingatia uwezo wa wafanyabiashara hao kiuchumi.
  Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa wa Arusha zilieleza kuwa ili kufanikisha ukusanyaji wa fedha kutoka kwa wafanyabiashara hao, chama hicho kimeunda kamati inayoongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa.

  Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdori Shirima, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Nangole na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Elishilia Kaaya.
  Vyanzo vya ndani kutoka CCM vilieleza kuwa wajumbe wa kamati ya Lowassa wamedhamiria "kuvunja rekodi ya kutembeza bakuli" kwa kukusanya kiasi cha Shilingi bilioni moja ili kufanikisha uchaguzi huo kuanzia ngazi ya chama hadi uchaguzi mkuu wa kitaifa.
  Duru za habari zinaeleza kuwa kamati hiyo ilikutana na baadhi ya wafanyabiashara hao Alhamisi iliyopita ambapo iliwataka kuchangia fedha ili kufanikisha kampeni za CCM katika kipindi cha uchaguzi wa mwaka huu.
  Wafanyabiashara hao, hata hivyo, wanalalamikia mbinu zinazotumiwa na chama hicho ya kuwaita mmoja mmoja kukutana na kamati hiyo ambayo imekuwa "kama inawalazimisha" kuchangia fedha badala ya kila mmoja kutoa fedha kulingana na uwezo wake.
  Mmoja wa wafanyabishara hao aliyezungumza na Raia Mwema kwa sharti la kutotajwa jina lake alieleza kuwa, awali uongozi wa chama hicho mkoa wa Arusha, kupitia kwa katibu wake, Mary Chatanda, uliwaandikia barua ya wito wa kuhudhuria kikao na kukutana na kamati hiyo.
  Barua hiyo, ambayo Raia Mwema ilifanikiwa kupata nakala yake, kichwa chake cha habari kilisomeka: "Kuhudhuria kikao maalumu siku ya Alhamisi ya tarehe 13 Mei mwaka 2010, saa 10 za jioni katika ofisi za CCM mkoa".
  "Katika kikao hicho utakutana na kamati teule inayoongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Edward Lowassa, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isidori Shirima, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Nangole na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Elishilia Kaaya", ilisomeka sehemu ya barua hiyo.
  Barua hiyo pia imeandikwa hivi: "Kutokana na uhusiano mzuri chama kina imani kubwa na wewe kwamba utaitikia wito huu na tunategemea kwamba wewe mwenyewe utahudhuria kama muda uliopangwa na kamati hiyo".
  Mfanyabiashara huyo alisema kuwa, hata hivyo alipofika katika ofisi hizo za CCM na kukutana na wajumbe hao, alielezwa kuwa anatakiwa achangie chama tofauti na barua ya mwaliko ilivyoeleza kuwa wanatakiwa kuhudhuria kikao maalumu.
  "Hali niliyoikuta ilikuwa tofauti kabisa. Wajumbe wa kamati walianza kunishawishi nitoe fedha za kuchangia chama tofauti kabisa na barua ya mwaliko ilivyoeleza", alisema mfanyabiashara huyo.
  "Kwa kweli nilichanganyikiwa kiasi kwa sababu sikuwa nimejiandaa kuchangia….lakini pia sikufurahishwa na mbinu hii ya kuwaita wafanyabiashara mmoja mmoja na kuwataka watoe fedha", alisema.
  Naye mfanyabiashara mwingine alieleza kuwa kamati hiyo imekuwa ikiwataka watoe kiasi kukubwa cha fedha bila kuzingatia kuwa wao kama wafanyabiashara wana majukumu mengine yanayowakabili kimaisha.
  Akitoa mfano, mfanyabiashara huyo alieleza kuwa, kwa mfano, kamati inawashawishi wachangie fedha zisizopungua Sh. milioni 10 hadi 20 kwa mtu; kiasi ambacho ni kikubwa sana kulingana na hali ya biashara ilivyo katika kipindi hiki.
  "Fedha walizokuwa wanashawishi tuzitoe ni nyingi kwa mtu mmoja, lakini pia mbinu inayotumika ya kuwaita wafanyabiashara mmoja mmoja inatia shaka; tofauti na tulivyozoea ambapo michango ya aina hiyo huchangwa kwa hiari na kwa uwazi mkubwa kama walivyofanya CCM Mkoa wa Kilimanjaro wiki iliyopita", alisema.
  Katika harambee hiyo ya kuchangia CCM Kilimanjaro, iliyofanyika jijini Dar es Salaam na iliyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, jumla ya Shilingi milioni 200 zilipatikana; huku milioni 100 zikiwa ni fedha taslimu.
  Mfanyabiashara huyo alisema, hata hivyo, kuwa fedha zinazochangishwa ni nyingi mno na hazina maana sana hasa katika kipindi hiki ambacho tayari Bunge limepitisha sheria mpya ya kuthibiti fedha katika chaguzi mbalimbali hapa nchini ukianzia uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
  "Kwa ujumla kamati hii imewatia hofu baadhi ya wafanyabiashara kutoka na kuonekana kama inawashinikiza kutoa fedha nyingi wakati tayari CCM ngazi ya Taifa imeshachangiwa mabilioni ya shilingi na walishatangaza kuwa fedha hizo zitasambazwa nchi nzima….sasa hii michango ya mkoani ni ya nini?", alihoji.
  Hakuna mjumbe wa kamati hiyo aliyepatikana, mwanzoni mwa wiki, kuelezea suala hilo la uchangishaji fedha ambalo limezua malalamiko ya chini kwa chini kutoka kwa wafanyabiashara wengi wakubwa wa Arusha.
  Karibu wafanyabiashara wote wakubwa waliozungumza na Raia Mwema waligoma majina yao kuandikwa gazetini kwa kuhofia ‘kushughulikiwa' na Serikali ya CCM.
  Akizungumzia malalamiko ya wafanyabiashara hao, Katibu wa CCM, Mary Chatanda aliyapuuza na kuyaita kuwa hayana msingi kwa kuwa hakuna aliyelazimishwa kuchangia fedha chama hicho.
  Katibu huyo, ambaye alionyesha wazi kuchukizwa kuulizwa maswali yanayohusiana na michango hiyo, alisema wafanyabiashara wote walioitwa ni wanachama na wapenzi wa CCM na hakukuwa na uvunjaji wowote wa kanuni na taratibu za kukusanya fedha za kusadia chama chao. "Hakuna kanuni wala utaratibu uliovunjwa……rasimu ya sheria mpya ya uchaguzi inaeleza wazi kuwa kila mwananchi anayo haki ya kuchangia chama anachokipenda kwa kufuata taratibu zilizowekwa", alisema huku akionyesha nakala ya rasimu hiyo ya sheria mpya ya chaguzi.
  Katibu alilalamika:'Nawashangaa sana waandishi wa Arusha….hivi kila mara lazima muandike habari mbaya tu za CCM? Hakuna habari nyingine? Mbona mazuri tunayofanya hamuandiki?", alihoji katibu huyo huku akifoka.
  Chatanda alieleza kuwa kimsingi wanachofanya ni kuwaita wafanyabishara hao na kuweka mambo sawa kabla ya kufanyika kwa harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuchangia chama hicho mkoani Arusha ambapo wanatarajia kumwalika Rais Kikwete.
  "Kama una shughuli nyumbani kwako si lazima kwanza uwaalike watu uwaeleze kuwa unataka kumwoza mwanao…..sasa hapa ndicho tunachokifanya. Kabla ya kuandaa harambee tumeona ni vyema tuwaite wafanyabiashara na wanachama wetu kwanza kabla ya shughuli yenyewe", alisema.
  Kuhusu kiasi cha fedha walichopanga kukusanya, katibu huyo alijibu kwa mkato kuwa hawezi kukitaja kwa kuwa hawajibiki kwa waandishi wa habari.
  "Siwezi kutaja kiasi kwa sababu siwajibiki kwako, na wala siwezi kukuambia ni lini tunafanya harambee yetu….hayo ni mambo ya chama chetu ambako ninawajibika kwa viongozi wangu", alisema Chatanda.
  Kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko kutoka kwa watu wa kada mbalimbali juu ya matumizi ya kupita kiasi ya fedha yanayofanywa na chama hicho kikongwe katika kampeni na chaguzi mbalimbali nchini.
  Licha ya kutungwa kwa sheria ya kuthibiti matumizi ya fedha katika uchaguzi, lakini hali bado ni tofauti kwa CCM.
  source: Raia Mwema May 19-24, 2010
   
 2. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hawa so-called wafanyabiashara wa arusha wengi wao ni majambazi na wavunja sheria wakubwa.. Kwanza CCM sijui inashirikiana nao ili iweje, Chama kimepoteza maadili. Inachukiza sana
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Usipotoa rushwa wanakuuwa ....huyu ni Meya wa jiji la mwanza akiwa kwa pilato

  [​IMG]
   
Loading...