Rushwa ipo kila sehemu sio CCM pekee nyie vipi bana - Msekwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rushwa ipo kila sehemu sio CCM pekee nyie vipi bana - Msekwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Aug 11, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,250
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280
  Duh
  kweli mtoto wa mwizi ni mwizi kumradhi ccm,ilakwa stetimenti ya makamu wenu mbele ya taarifa ya habari kwamba mnashangaa nini kuona ccm kuna watoa rushwa ati rushwa ipo kila sehemu

  nakuja kwenu watanzania mzee wetu huyu ameeleza wazi na cha kusikitisha akaanza kutaja sehemu moja baada ya nyingine mahospitalini ukitaka huduma upati bila rushwa akaja mahakamani ushindi kesi bila rushwa akaja wizara ya ardhi uanataka kibali tena cha ardhi ya ko kujenga upati bila rushwa akauliza kila sehemu kumejaa rushwa nakushangaa watu mnaifwatilia ccm oooh wala rushwa....ndugu zanguni ni pius msekwa huyu sasa mwenye macho na asikie kama upuuzi wote aliooutaja ulikuwa chini ya uongozi wa ccm kwanini ukawapigie ccm leo hii
  embu pigia chedema jamani huyu mzee angejua cost ya maneno yake jana asingethubutu kutoka kwenye tv...anyway ndio washazoea tutafanyaje...

  Wana jf na wote wenye mapenzi mema kuliko kuipigia ccm na kama aujsikii kupigia wapinzani bora ulale siku ya uchaguzi usikubali kuwapa mbu waitbu malaria hata siku moja
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,250
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280
  Hivi ccm
  amwamini mtu awezi kufanya kitu bila kutenda dhambi....kwa kweli inasikitisha sana huyu mh kutaja sehemu zote kumbe yawezekana wanafanya kutokana na exp ya chama chao haya yetu macho ipo siku watanzania watasema basi yatosha
   
 3. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ni Aibu kubwa kwa mtu aliyekua spika wa bunge Mzee Msekwa kusema hivyo. Nakumbuka ni wakati wake rushwa ilirembwa kwa kuitwa Takrima wakisaudiana na Mzee wa Vijisenti
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hivi huyu Msekwa amesahau kama CCM ndio imekuwa madarakani tangu kupatikana kwa uhuru!
  Hajua mahakama, wizara ikiwemo ya ardhi na hospitali za taifa zipo chini ya Serikali ya CCM!
  Huyu mzee atakuwa na Maralia tena zaidi ya Sugu.
   
 5. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kadri unvyozidi kuwa mtu mzima zaidi basi na uwezo wa kufikiri huwa unapngua....ukisha kuwa mzee sana huwa unakua kama mwehu... sasa huyu msekwa ndo anapoelekea... yeye anadhani hayo yote yametokana na Serikali ipi??? Si hii hii ya CCM???
   
 6. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  CCM wana matatizo makubwa sana na wanahitaji kupumzika pembeni wajifunze kwanza jinsi ya kuendesha nchi.....hakuna kiongozi makini anaweza akatokea CCM tena, kama makamu mwenyekiti na katibu mkuu ambao ndio watendaji wakuu kimsingi kwa sbb Rais anakuwa busy muda mwingi....wameipamba rushwa hadharani kabisa...na chombo chao TBC1 kikatuonyesha bila kusitasita ili watu wote tuone na kuamini wanachokiamini.......
  Serikali ni ya CCM mpaka baada ya Uchaguzi hapo october 31st,na wao ndio watunga sera na serikali inatekeleza ilani iliundwa na hawa watu wa sisiEMU halafu nao eti wanashangaa na hawashangai na kututhibitishia kuwa kila sehemu kuna rushwa hapa nchini.....wanafananya nini kurekebisha haya?au ndo wanasema tuendelee hivihivi hatuna cha kufanya????mi siami...ndo maana kura yangu itasaidia kuwaweka pembeni hapo october.....
  inaumiza maini kuona hawana mbinu hata za kukosanya kodi,wamekomaa na wafanyakazi kuwanyonya tu mishahara yao.....hapa dar sasa hivi watu wanamiliki mareal estate ya uhakika halafu hawalipi kodi kabisa....mtu ana nyumba mpaka 10 na zaidi..kila nyumba inalipiwa rent zaidi ya 300K/month totaling more than 3000K halafu halipi kodi ya mapato...wanaona mfanyakazi tu mwenye kipato cha 200K wamtwange kodi akafie mbali...
  ....................................inauma sanaaaa.................
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  sometimes ni kukosa tools of analysis kichwani.
  1- Kwa mwenyekiti wa chama tawala kutamka hivyo lazima ujue ni tamko la chama. Huweki kulitenganisha na kuwa maoni ya mtu binafsi kutokana na nafasi/cheo chake kichama.

  2-alipaswa kujua kuwa wakuu wote wa medical/Hospitals, Mahakama, Polisi, taasisi na idara za kutoa huduma hapa nchini ni makada wa CCM maana wameteuliwa na mwenyekiti wa ccm ambaye ni rais wa nchi si kwa uamuzi wake pekeyake pia na wa ccm. Hivyo uteuzi huendana na uswahiba na influence ndani ya chama. Huwezi kumteua mla rushwa ikiwa wewe si mla rushwa.

  3 - Na hivyo yeye msekwa kwa position yake anahusika kwa ama kumshauri raisi kuteua wala rushwa na au kuwabakiza walarushwa ktk taasisi alizozisema kuwa zimejaa rushwa.

  CCM INAHITAJI KWENDA LIKIZO YA KUONGOZA NCHI AU IKUBALI KUOVERHAUL ATTITUDE YAKE-jambo ambalo kamwe hawawezi kufanya.
   
 8. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mkuu unajua ukizidi kufanya uhuni basi ujue siku moja utakuja kufanya mbele za watu halafu uwaache vinywa wazi.
  Na hili ndilo linalokuja sasa.
  Ameanika uozo wake wote, na isingekuwa Tanzania Basi CCM wangekuwa wameshajitoa madarakani kabisa. Inasikitisha kuona mtu anadiriki kusema anayafahamu yote hayo na wala hana wasiwasi.
  Anyway CHADEMA najua ndo chama pekee cha upinzani hizo ni quotes za kuchukua
  maana kasema ukweli, na ndo mambo ambayo tumechoka nayo kwa kutupeleka kubaya.
  Ukicheki Nchi kwa sasa imemezwa na rushwa na ndo hivi sasa ni nje nje. Huyu ni kiongozi wa juu na ameshindwa kupata point za kuficha. Of course ule ndo utetezi wake.
  Tuamkeni sasa hawa wanatakiwa kupumzika kwa mda angalau hata miaka mitano tu.
  Lakini,
  TUMWOMBEENI SANA SANA DR. SLAA maana kaingia katika kipindi kigumu sana ambacho CCM imefulia wazi wazi kabisa.
  SLAA AENDE MBELE AOKOE HII HALI!!
   
 9. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Msekwa asilaumiwe kuwa amesema aliyosema kwa sababu ya uzee wala asilaumiwe kuwa hana akili amesema hali halisi ilivyo. Hakuyasema kwa unafiki. Bali alichosahau ni kwamba hali ya rushwa imetengenezwa, kulelewa na kuendelezwa na Chama anachokiongoza. Kauli yake ni faida kwa vyama vingine kwa vile amethibitisha kukithiri kwa rushwa iliyoletwa na chama kilichoko madarakani. Makamba pia ametoa kauli ya kuisaidia Chadema alipotoa kauli yenye kuthibitisha kuwa Dr. Slaa ni tishio kwa Kikwete na CCM. Wataendelea kudhihirisha ubaya wa chama chao.
   
 10. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Hilo niukweli mtupu,
  Mzee naye anachanganyikiwa
   
 11. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ukiona mtu anahalalisha ujambazi basi nae ni jambazi pia. Iko wapi ile kauli mbiu ya baba wa taifa mwalimu nyerere ya kusema rushwa ni adui wa haki??? Au mzee hakumbuki hili?
   
 12. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,250
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280

  Wee tena anaongea huku anacheka jamani huyu mzee hata iana hana kabisa anyway pengine ccm wameumbwa bila haya
   
 13. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Ujue CCM sasa hivi wasikia kizunguzungu, kilka mahali nchini wanaCCM wanaandamana kudai wgombea wao waliowapigia kura lakini wakataliwa! Walijidanganya kufanya utezi wa kidemokrasia zaidi kumbe walisahau kwamba demokrasia kwao ilishatoweka ila rushwa ilishakuwa ndio jadi. Jana kwenye taarifa za habari TV mbalimbali walionyesha wanaCCM kibao wanaandamana wameinua kadi za kijani....wanaimba....tunataaaka, mgombea wetu! Nilijisikia vizuriiii.....Maana sala yangu huwa hivi zimwi lizimike siku moja.
  Matukio kama hayo akili ilioanza ku-expire kama ya Mzee Msekwa lazima kizunguzungu cha kufa mtu.
   
 14. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #14
  Aug 11, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Jenerali kwenye rai ya jenerali leo kanena namnukuu " msekwa ameajiri wahuni wa kutosha, asifanye uhuni"
  kwa mara ya kwanza kabisa rai ya jenerali ina maneno makali na ya kukaripia heko jenerali!
   
 15. Mwanamosi

  Mwanamosi Member

  #15
  Aug 11, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukisoma between the lines utagundua kuwa kimantiki ana kila sababu kusema hivyo kwani mtoa rushwa ni mtu na si chama..kutoa rushwa ni kitendo ambacho lazima mtoaji na mpokeaji wawepo, kwahiyo mtoaji na mpokeaji wanaweza kuwepo popote pale ndani au nje ya CCM..mahakamani,hospitali au popote pale nadhani mifano mingi ipo..barabarani ndio trafiki usiseme. so wote hao ukiwachukua mmoja mmoja wapo wa CCm na wapo wa Vyama vingine kwa hiyo kusema watoa rushwa wapo kila mahali ni sahihi. nadhani halihitaji mjadala mkubwa kuliweka wazi jambo hilo.

  Rushwa inajulikana ni adui wa maendeleo kila mahali ila kiukweli sidhani kama kuna mtu atakiri hadharani kuwa ametoa rushwa au kupokea kwani mara nyingi tumekuwa tukijikuta kwenye mazingira magumu na kujikuta tukitoa chochote ama kwa kujua au bila kujua kuwa tunatoa au kupokea rushwa ili tu mambo yetu yafanikiwe. na tatizo hili si kwenye kutoa/kupokea fedha tu..rushwa ina aina nyingi zikiwemo rushwa ya ngono na nyingine nyingi tu ambazo hatujui kama ni rushwa kwa kuwa hatuzisikii sana kwa hiyo rushwa ipo kila mahali kutegemeana na mazingira husika.

  hoja ya msingi ni ukubwa wa tatizo ambao mzee msekwa alijaribu kuuzungumzia na hili nadhani hata Takukuru na Hosea alikiri kuwa ni kubwa mno na wanaendelea kupambana. inawezekana kuwa tunataka kuigeuza kauli yake kuwa ya kisiasa zaidi dhidi ya kusudio lake halisi ambalo ni kueleza ukubwa wa tatizo na kuweka bayana kuwa sio CCM tu bali hata kwenye sehemu alizotaja kiuchache kuna tatizo hilo. kwa sababu hiyo nadhani iko haja ya kutazama tatizo kwa kutazama mhusika ambapo hapo ndipo sasa tutawakuta wanaCCM,wapinzani,askari,wanahabari,wanafunzi,walimu,wafanyabiashara na kila mwenye kutaka urahisi wa mambo wote wanaangukia humo.

  kwa mantiki hiyo rushwa ipo kila sehemu na si CCM peke yake kama tutaichukua kauli hiyo kwa maana hiyo iliyokusudiwa na siyo kuichukulia kipropaganda za kisiasa. hakuna anaependa kwenda mahali asipate huduma haraka(mfano hospitali,NSSF,mahakamani au popote pengine) lakini akipewa option ya kufanyiwa huduma kwa kinachoitwa Fast-track basi hutoa kianchotakiwa na anapewa huduma ambayo mara nyingi haitofautiani na huduma wanaopewa wanaorudi hapo mara 3 au 4 kwa huduma hiyo hiyo. vilevile ukishikwa na trafiki na una kosa la kweli wengi huamua kumpa chochote ili asipoteze muda wa kuwahi mambo yake nae anapokea coz mshahara gani alionao akakataa 5000 ya bure na matatizo aliyonayo ni ya zaidi ya shilingi milioni moja,anapokea anaweka vocha,ananunua mboga na maisha yanaendelea.

  Mtazamo wangu ni kuwa tatizo ni la kimfumo wa kiutendaji zaidi ambao umeathiriwa na umaskini wa watendaji wengi ambao kipato chao ni kidogo hivyo kulazimika kutumia mbinu mbalimbali wajipatie namna ya kuendesha maisha yao. hawa wanaweza kuwa na itikadi ya chama chochote na sidhani kama Wa CCM pekee ndio watoaji na wapokeaji rushwa. viwango vya rushwa hutofautiana na nadhani hapa ndipo Takukuru inapigwa chenga na wajanja kwani mbinu hubadilika kutokana na kiwango, kuna wanaojifanya kuchangia harusi,kuna wanaolipia bidhaa dukani na kuchukua risiti bidhaa itafatwa na mpokeaji zote hizi ni mifano michache tu kati ya milioni iliyopo. kwa hiyo rushwa ipo kila sehemu si CCM peke yake.

  Nadhani ni wakati sasa Takukuru japo haipewi imani na walio wengi ikae sawa itazame mambo haya kwa upana zaidi na si kuishupalia CCM kwani watakaobainika ndani ya CCM watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na Makamba ameahidi hawatatetewa na chama. sheria ya matumizi katika uchaguzi nadhani imetafsiri makosa na aina za rushwa so nategemea tutahukumiana kwa mujibu wa sheria hii na tuichukue kauli ya mzee msekwa kama changamoto kuwa rushwa ipo kila mahali na si kwenye CCM na tujue kuwa CCM ,TLP au CHADEMA ni vyama vinaundwa na wanachama ambao ndio hao hutoa/kupokea rushwa kwa ajili ya kutaka nafasi mbalimbali za uongozi. tukumbuke wakivua magwanda yao ya uanachama basi hurudi katika kazi zao za kawaida za uanasheria,udaktari,ualimu na kadhalika kwa hiyo ukiwazuia kwenye chama wakirudi mtaani (mfano trafiki, watakupiga bao na utatoa tu bila ubishi) watatoa/pokea kutokana na nafasi zao za kiutendaji au mamlaka waliyonayo.

  mi sina nia ya kuanzisha malumbano na wanaodhani kila kitu ni siasa katika kauli za viongozi ila naomba tuunge mkono jitihada za kutokomeza tatizo hili la rushwa kwa kubadilika sisi wenyewe ndani yetu na ndipo tutaweza kung'oa mibuyu. tukisema ni CCM pekee ndo wanatoa/pokea rushwa basi jamaa wa TRA(sorry wazee wa kodi!!) watazidi kutupiga gap huku mitaani coz hali ni ngumu na kila mtu anakula urefu wa kamba yake. tukifata maadili basi tamaa za madaraka hazitakuwepo ila kwa kuwa kila mtu anataka madaraka basi mbinu za hovyo zitatumika na hapa ndipo tatizo litaonekana kubwa katika vyama ila uchaguzi ukiisha utaona tatizo linaelekezwa sehemu tofauti.

  binafsi naunga mkono kauli ya mzee huyu kuwa si CCM peke yake,haihitaji kuwa na degree kujua kuwa tatizo liko kila mahali na ni kubwa..hii iwe ni eye opener kwa Takukuru na wengine wanaodhani kusema kuwa CCM kuna rushwa inatosha. imeshasemwa siku za nyuma,tuhuma hizo na ushahidi uletwe ili watuhumiwa wachunguzwe ila hakuna ushahidi wa kutosha ulioweza kutolewa kwani hatujasikia Takukuru wakisema lolote na CCM wanakubali wamepokea malalamiko kwenye chaguzi za kura za maoni kwa hiyo kama kuna ushahidi wa kutosha basi watashughulikiwa kichama na kisheria(Takukuru,natumaini itakuwa hivyo) manake tuhuma haimfungi mtu bali ushahidi wa kuaminika.

  najua kuna watu wataguswa na kutaka kunishambulia kwa kusema haya lakini naomba watu wasimsome vibaya mzee huyu nia yake ni njema kuonesha kuwa rushwa ipo ndani ya CCM na hata nje pia ipo ila kwakuwa ni kipindi cha uchaguzi basi kauli nyingi zitageuzwa kisiasa zaidi ili kushawishi watu wapigie kura chama flani. sidhani kama ni sawa, watu waachwe wachambue pumba na mchele coz wagombea wakipitishwa na NEC ya CCM ndo tutajua nani ni nani coz kuna rufani nyingi inasemekana zimepokelewa so wanaCCM wana jukumu la kujiweka safi kwa kurudisha majina yanayouzika na walioshindwa wakubali matokeo coz kama walizidiana ujanja kwenye kura za maoni basi mtu asilie kuwa kuna rushwa na ubaya huu na ule.

  Mabadiliko huletwa na watu na tuanze kubadilika ndani yetu na hapo ndipo tutaliondoa tatizo hili katika siasa zetu,so tuanze kurejea miiko na maadili ya uongozi ndipo tujue wakumchagua..ila mzee msekwa yuko sawa kusema kuna rushwa kila mahali kwa hiyo watu wasiitazame CCM kama sehemu ya mfano unapozungumzia rushwa hapa nchini.
   
 16. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #16
  Aug 11, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160


  rushwa inayoongelewa kwa sasa na ambayo imezua haya yote ni ktk kura za maoni za ccm ambayo imefanyika miongoni mwa wanachama wa ccm. Ni kati ya wagombea udiwani na ubunge kama watoa rushwa na wanachama ambao hawagombei nafasi yoyote bali ni wapiga kura.

  chama ni viongozi na wanachama, hakuna kiumbe kinachoitwa CCM ambacho ni tangible, ila tunasema wale ni wa CCM tukiwaona viongozi wao na wanachama na majengo yao wakiwa na magwanda ya kijani na njano.
   
 17. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #17
  Aug 11, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,454
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Si mnakumbuka ya mwenyekit wake na Vitochi....
   
 18. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #18
  Aug 11, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Imani yangu imekuwa ni kwamba hawa wanaoshiriki ktk kutafuta ubunge na udiwani, ni wanachama ambao wamekuwa wakitumika siku zote kuiba kura au kuhonga ili mambo ya chama yaende vizuri.

  Mchezo huu wanaufahamu na wana uzoefu ndo maana hawakuogopa. Sikuona sababu ni kwa nini Chama chenye viongozi wenye nguvu waseme hawataki rushwa na wanachama waliochini yao wafanye hayo bila hata woga. Finally naona viongozi wenyewe wanakubali kwamba ni kawaida.
   
 19. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #19
  Aug 11, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  du.. CCM inawatoa wapi hawa watu !!
   
 20. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #20
  Aug 11, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Rushwa inayoongelewa ni ile iliyotokea wakati wa Uchaguzi wa CCM. waliohusika ni wana chama wa CCM ambayo ndiyo iliyounda serikali ilyoongoza nchi hii takribani miaka 50. Nina maswali mawilli.

  (a) Rushwa ni kosa la jinai kama iliyvo kosa la mauaji. Chombo kinacholinda sheria za nchi ni serikali ambayo ni ya CCM. Iweje mwenyeketi wa CCM azungumze kama vile rushwa ni halali, huoni kuwa anakidhalilisha chama chake kuwa serikali yake haiwezi kulinda sheria za nchi, hivyo chama kmeshindwa kuongoza?

  (b) Chama ni kitu gani, si ni muungano wa watu au wanachama wenye imani na lengo moja? Kama wanachama hao ni watojai na wapokeaji wa rushwa huoni kuwa ina maana chama chao ni cha watoa na wapokea rushwa?
   
Loading...