Rushwa imeifikisha pabaya TAMISEMI. Je, hawa viongozi wanaoiongoza wanapaswa kuwepo hapo?

Tangazo lilikuwa lipo sana applicant yeyote atakae jaza invalid numbers,Application yake itakuwa nullfied and will not be processed(rejected). Sasa imekuwa hizo application ziwe proccessed wakati applicant amejaza invalid index number .Mmepokea rushwa namba zilizokuwa zinatumika kupokelea rushwa ntaziweka hapa na miamala yake
Kweli kabisa inabidi watumbuliwe hawa, haiwezekani wakafanya madudu kwa kiwango kikubwa na kuwawekea bond watoto walio maliza 4m mwaka jana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali yatoa ufafanuzi wa hoja, ajira mpya za waalimu.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimeti ya utumishi wa umma na utawala bora Dkt. Laurean Ndumbaro na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo wametoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizojitokeza kwenye ajira mpya za waalimu...
Hayo majina Inawezekana ni fake kuwadanganya watu kuwa serikali imetoa ajira Kumbe hakuna kitu.
 
Kwanza naomba nianze kwa kutoa masikitiko yangu juu ya wizara ya Tamisemi.

Tamisemi ipo chini ya ofisi ya Rais kwa maana hiyo ndicho kioo cha Rais. Wizara ikiboronga maana yake inamchafua Rais na ikifanya vizuri na Rais anakuwa amefanya vizuri.

Kwahiyo, Kitendo cha katibu mkuu kutoa majibu mapesi kwenye hoja nzito zilizo ibuliwa na wadau kuhusu madudu kwenye ajira za ualimu ni kitendo kinacho tia mashaka juu ya weledi wa watendaji katika hiyo wizara.
Hili pia naomba mheshimiwa Rais aliangalie kama ikimpendeza kwenye baraza jipya la mawaziri atakaloteua, hii wizara ipewe waziri mwingine. Hii itasaidia kuwepo kwa uwajibikaji na kuepusha tabia ya watendaji kufanya kazi kwa mazoea.

Sasa Turudi kwenye mjadala wetu wa majibu ya tamisemi kutolea ufafanuzi wa madudu kwenye ajira za walimu. Press conference hiyo ya kujibu madudu ili hudhuriwa na makatibu wakuu watatu siku ya jana.
1. Eng. Joseph Nyamhanga- katibu mkuu tamisemi
2. Dkt. Laurean Ndumbaro- katibu mkuu utumishi
3. Dkt. Leonard Akwilapo- katibu mkuu wizara ya elimu.

1. HOJA YA KWANZA: kuhusu jina la ABDALLAH SHONDE kujirudia mara 196.
-katika kutetea hoja hiyo, katibu mkuu alisema hilo jina kujirudia halikuongeza idadi wala kupunguza ajira za walimu wengine bali iliongeza wingi wa majina tu. Hapa naomba aliyemwelewa katibu mkuu anifafanulie. Na kufuatia utetezi huo naomba nimuulize katibu mkuu swali moja;
(i) kama jina hilo kujirudia kila ukurasa halikuwa na madhara. Kwanini mlifanyia marekebisho na baada ya marekebisho hayo baadhi ya majina mapya ya walimu wakaongezewa na kurasa za majina kuongezeka toka kurasa 196 hadi kurasa 197?

HOJA YA PILI: kuhusu waliomaliza kidato cha nne 2019
- katika utetezi wake katibu mkuu alidai wamepitia majina hayo upya na kubaini kuwa walimaliza kidato cha nne 2013.
Utetezi huo wa katibu ni dhaifu kwa sababu zifuatazo;

(i) katibu mkuu hakuwa na uhakika wa kulithibitisha hilo hivyo aliishia kutoa ufafanuzi kwa hisia na kubahatisha. Ili kuthibitisha ninacho kisema nimefanya uchunguzi wa matokeo ya walimu watatu wenye index za kidato cha nne za 2019 na kubaini yafuatayo;

(a) WINNIE ELIAS MBISE
-huyu ametumia index: S0687-0124/2019. kutokana na kauli ya katibu mkuu kuwa wenye hizi index za 2019 wamemaliza 2013 nimefanya utafiti mdogo wa matokeo ya mwanafunzi huyu kwa mwaka 2013 kwa kutumia index:S0687-0124/2013) nimegundua kuwa shule aliyohitimu inaitwa KIKATITI SECONDARY na kwa mwaka huo ni watahiniwa 116 tu waliokuwa wamesajiliwa kufanya mitihani na hivyo namba ya mtahiniwa wa mwisho ilikuwa S0687-0116/2013. Je, hii index: S0687-0124/2013 ambayo katibu anataka kutuaminisha inatoka wapi?

(b) BAKARI LAUZI BAKARI
-huyu ametumia index: S3678-0064/2019. Kwa mujibu wa maelezo ya katibu mkuu kuwa wamemaliza 2013, nilipofuatilia matokeo ya index hiyo kwa mwaka 2013 nimegundua kuwa mwalimu mwenye namba hiyo (S3678-0064/2013) alipata divisheni sifuri. Kutokana na matokeo hayo, je katibu mkuu anakubaliana na mimi kwamba wameajiri mwalimu aliyepata divisheni zero kidato cha nne?

(c) DAVID LAMECK NDOSSA
- huyu ametumia index: S1943-0147/2019 ameajiriwa kama fundi sanifu wa maabara. Lakini kwakuwa katibu mkuu alisema wamemaliza 2013 nilipofuatilia matokeo yake nimegundua kuwa mtahiniwa mwenye namba hiyo (S1943-0147/2013) alipata F ya biology na wala hakusoma somo la fizikia au kemia. Kutokana na matokeo hayo, je katibu mkuu anakubaliana na mimi kwamba wameajiri mtu ambaye hakusoma masomo ya sayansi kwenda kufundisha practicals?

(ii) utetezi wa katibu mkuu ni dhaifu kwa sababu siku ya kutangaza ajira alisema moja ya kigezo cha kuwapangia watu ajira walizingatia ulinganifu wa taarifa zilizopo kwenye vyeti na taarifa zilizojazwa kwenye mfumo. Kama kweli walizingatia ulinganifu huo, kwanini wameajiri walimu ambao taarifa zao za kwenye mfumo haziendani na taarifa zilizopo kwenye vyeti mfano hawa wenye index za 2019?

(iii) utetezi wa katibu mkuu ni dhaifu kwa sababu mfumo ulikuwa na uwezo wa kuthibitisha index za waombaji. Katika kuthibitisha hilo nanukuu sehemu ya maelezo yaliyokuwepo kwenye mfumo " Your form four index number and any other used certificate should be valid as they will be verified before you are selected. Invalid number will lead to rejection of your application". Kama mfumo uliweza kutambua index za waombaji kwanini watu wenye index zenye utata wameajiriwa?. Katika hili usikimbilie kwenye kichaka cha matatizo ya kwenye mfumo kwa sababu majina ya waombaji mlikaa nayo kwa zaidi ya mwezi mmoja na mlifanya zoezi kwa umakini kwa kuzingatia ulinganifu wa taarifa.

Pia kufuatia utetezi huo naomba katibu mkuu atoe ufafanuzi wa walimu walio ajiriwa kwa namba hizi za kidato cha nne;
(i) S0660-0541/2019
(ii) S0566-1215/2019
(iii) S0151-0785/2015
(iv) S1380-1058/2019
(v)S1380-0852/2019
(vi) S0440-0963/2019

(a)katibu mkuu atwambie majina ya shule ya center namba zilizo tumika kwenye hizo index na ni shule gani hizo amabazo wanafunzi wa kidato cha nne walikuwa wanahitimu ndani ya mwaka mmoja kwa idadi kubwa hiyo ya 800+, 900+ na 1000+

(b) katibu mkuu aseme kwanini waajiriwa hao namba zao za kidato cha nne hazitambuliki na baraza la mitihani(NECTA)


HOJA YA TATU: kuhusu idadi ya ajira
Katika kujitetea katibu mkuu amekiri wazi ya kuwa ajira zilizotolewa siyo 13000 bali ni ajira 8000. Sasa najiuliza siku zilipotangazwa katibu mkuu alisema ni ajira 13000 alidanganya umma kwa maslahi ya nani na je, hiyo ndio ilikuwa ahadi ya Rais Magufuri kuajiri walimu 8000?

Katika press conference hiyo, katibu mkuu amekwepa kujibu madudu ya kuajiri walimu waliotumia namba za wanafunzi wa kidato cha tano wanaoendelea na masomo. Hili nalo linahitaji ufafanuzi

Mwisho, kutokana na utetezi mwepesi uliotolewa na katibu siku ya jana tunaomba tamisemi ijipange upya ije na utetezi ulioshiba na wenye uthibitisho wa majibu ya madudu yote usio na mashaka au watoe orodha mpya ya majina ambayo madudu yote yaliyoibuliwa yawe yamefanyiwa kazi.
 
1.Eng. Joseph Nyamhanga- katibu mkuu tamisemi
2. Dkt. Laurean Ndumbaro- katibu mkuu utumishi
3. Dkt. Leonard Akwilapo- katibu mkuu wizara ya elimu.
Hao TAMISEMI, wameingizwa chaka na wakurugenzi wa Halmashauri. Wakurugenzi walielekezwa watume majina ya walimu wanaojitolea kufundisha shule za awali, msingi na sekondari, ili wapewe kipaumbele katika ajira.

HAPO NDIPO KOSA lilipoanzia. Waliorodhesha ndugu zao hata wasiokuwa na sifa, waliwatafuta kwa TOCHI, kwa vile ndiyo ulikuwa mkakati matokeo yake hawajui asilimia kubwa ya wale wanaojitolea hawana sifa za kufundisha.

Hivyo katika kutoa ajira walianza na hao kwa damu na jasho ili wapate ajira. Linapotekea suala la sifa hapo ndipo wanashindwa kutoa majibu. NENDA KILA HALMASHAURI ULIZA MAELEKEZO WALIYOPEWA WAKUU WA SHULE TOKA KWA VIONGOZI WAO. utacheka aisee.
 
Mkuu basi inatosha naona umekomaa na hili jambo toka juzi kama wakuchukua hatua wangeshachukua hao hawana nia ya kutatua ajira nchi hii lengo lao watu waishi kama mashetan


#NASEMA UONGO NDUGU ZANGUUUU
Mkuu ukisema niliache hili kuna hewa nyingi itaingia serikalini. Acha niendelee kulisemea hata wasipo chukua hatua ukweli utakuwa umejulikana
 
Serikali yatoa ufafanuzi wa hoja, ajira mpya za waalimu.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimeti ya utumishi wa umma na utawala bora Dkt. Laurean Ndumbaro na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo wametoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizojitokeza kwenye ajira mpya za waalimu...
Ajira hizi zina ukakasi wa kutosha.
 
Kwanza naomba nianze kwa kutoa masikitiko yangu juu ya wizara ya Tamisemi.

Tamisemi ipo chini ya ofisi ya Rais kwa maana hiyo ndicho kioo cha Rais. Wizara ikiboronga maana yake inamchafua Rais na ikifanya vizuri na Rais anakuwa amefanya vizuri...
Mkuu Alwatan kamba ,Mwenyezi Mungu akubariki sana kwa uchanganuzi mahiri sana.

Hii ndio tunaita kuitendea haki elimu,vyeti,vitabu,vyumba vya madarasa na walimu ambapo kote umepitia.

Kongole sana na "keep it up".
 
Barua ya wazi kwa sekretarieti ya ajira na TAMISEMI

Ndg, Viongozi wenye dhamana inayohusiana na AJIRA hususani Ajira za ualimu Mimi kama Mtanzania wa kawaida mwenye akili timamu na ambae pia ni Mdau wa ELIMU Naiomba Ofisi yako iweze kutoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya majina ya waajiriwa wa Kada ya ELIMU Yaliyotolewa na Wizara yako pendwa na Nyeti ya TAMISEMI. Tarehe 27/11/2020 kuna baadhi ya majina ya waajiriwa yanaendelea kuwapatia watanzania TAHARUKI KUHUSU AJIRA ZAO...
Kongole sana mkuu na Mwenyezi Mungu akubariki sana "Prof Hans",

Mwalimu asiyekuwa na Kituo maalumu cha Kufundishia.
 
Hao TAMISEMI, wameingizwa chaka na wakurugenzi wa Halmashauri. Wakurugenzi walielekezwa watume majina ya walimu wanaojitolea kufundisha shule za awali, msingi na sekondari, ili wapewe kipaumbele katika ajira. HAPO NDIPO KOSA lilipoanzia. Waliorodhesha ndugu zao hata wasiokuwa na sifa, waliwatafuta kwa TOCHI, kwa vile ndiyo ulikuwa mkakati matokeo yake hawajui asilimia kubwa ya wale wanaojitolea hawana sifa za kufundisha. Hivyo katika kutoa ajira walianza na hao kwa damu na jasho ili wapate ajira. Linapotekea suala la sifa hapo ndipo wanashindwa kutoa majibu. NENDA KILA HALMASHAURI ULIZA MAELEKEZO WALIYOPEWA WAKUU WA SHULE TOKA KWA VIONGOZI WAO. utacheka aisee.
Mkuu OTTER ,haya uliyoyaandika ni kweli!???
Itakuwa vyema kila kitu kiwekwe hadharani ili tujue wapi tatizo la msingi limeanzia. Wengine tupo mbali na huko nyumbani,hivyo tungeona uthibitisho wa haya uliyoyaandika,tungeweza saidia nini cha kufanya.
 
Kwa sasa tuko kwenye matumizi ya katiba ya New Zealand, tunaomba mtuache. Sisi kule kwetu New Zealand ukushinda ubunge huruhusiwi kuingia ktk ukumbi wa bunge hadi uapishwe.
 
Back
Top Bottom