Uchaguzi 2020 Rushwa ilivokithiri Kura za maoni za CCM Jimbo la Kalenga

Jan 29, 2014
35
37
Tarehe 21 / 7 / 2020 Ulifanyika uchaguzi wa kura za maoni kupata mgombea atakayepeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 Jimbo la Kalenga mkoani Iringa.

Katika hali isiyotarajiwa RUSHWA ilikithiri sana kiasi cha wajumbe kupewa pesa eneo la uchaguzi kilipo chuo cha mafunzo cha CCM eneo la Ihemi pembeni kidogo ya barabara kuu ya Tazam.wagombea vinara wa ukiukwaji huu;

1.JACKSON GIDEON KISWAGA

Huyu ndiye aliyeongoza ktk uchaguzi ule na ndiye kinara wa RUSHWA ambapo anatajwa kutoa kati ya shilingi elfu 70 mpaka 100,000/- kwa kila mjumbe.Taarifa za ndani zinaeleza ndugu kiswaga aliuza nyumba yake iliyopo Iringa mjini na fedha yote akatumia kuhonga wajumbe.Kupitia wapambe wake akiwemo Bw.nganyagwa anayetajwa kua diwani wa kata mojawapo na Bw.Yangi anayetajwa kua kampeni meneja wake walitoa pesa hizo asubuhi wajumbe wakiwa njiani kwenda eneo la uchaguzi na eneo la uchaguzi ambapo bw.Nganyagwa alikamatwa na maafisa usalama akitoa rushwa kwa wajumbe wa kata yake



2.LEO MARTIN MAVIKA

Huyu ni alishika nafasi ya pili.anatajwa kua mtumishi wa TAMISEMI.ametajwa kwa kuanza kampeni mapema tangu mwaka 2017 alipowasafirisha makatibu wa kata zote za jimbo kwenda Dodoma kama sehemu ya mkakati wa kupanga safu.Pia ametajwa kukopa fedha ya sehemu ya kiinua mgongo kiasi shilingi milioni 120 aliyoitumia kuhonga wajumbe

3.BRYSON KIBASA

Huyu alikua mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Hanang aliyetenguliwa uteuzi wake baada ya kutia nia ya ubunge.Bwana Kibasa kwa kutambua amepoteza ukurugenzi alitafuta ubunge kwa gharama yoyote kwa kutoa fedha kati ya shilingi elfu 50 mpaka elfu 70 kwa kila mjumbe.Siku ya uchaguzi kinyume na utaratibu wa chama alisafirisha wajumbe wa kata anayotoka kwa usafiri wake mpaka eneo la uchaguzi na aliposhindwa uchaguzi aliwatelekeza wajumbe akiwatuhumu wamemsaliti

Watatu hawa waliendesha siasa za ukanda na kukigawa chama ambapo bwana mavika aliwashika makatibu kata zote.Bwana kiswaga aliwashika wenyeviti wa kata zote. Na Bwana Kibasa aliwashika makatibu wenezi wa kata hali iliyopelekea kudhoofisha utendaji kazi wa chama kutokana na mivutano baina ya viongozi hao


Tunatambua dhamira ya Mwenyekiti na Rais wetu Dr.John Pombe Magufuli ni ya dhati sana.Matamko ya Katibu mkuu Dr.Bashiru Ally Kakurwa na Mwenezi Taifa Mh.Humphrey Polepole yanakinzana na haya yaliyotokea Kalenga na maeneo mbalimbali nchini


Ni Imani yetu haki itatendeka na kila mmoja atapata anachostalihili

CCM BILA RUSHWA INAWEZEKANA !
 

Attachments

  • IMG-20200811-WA0001.jpg
    IMG-20200811-WA0001.jpg
    68.9 KB · Views: 1
Mta semana sana. Ila huwezi kuitenganisha Ccm na rushwa. Kama hata kiongozi wenu mkuu ali idhinisha pilisi wachue 5000 barabarani itakuwa wagombea kuchukua laki mkutane baada ya miaka mitano jamani??
 
Rushwa ni desturi yenu.

Iacheni halmashauri kuu ifanye kazi.

Hakuna aliye msafi CCM.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom