Rushwa Elimu ya msingi yawagharimu watoto wasio na hatua Wilayani Tunduru

Watunduru

Senior Member
Dec 29, 2011
170
39
Ni majonzi na masikitiko makubwa kwa wazazi/walezi wilayani Tunduru baada ya watoto wetu kufutiwa matokeo ya mtihani wa Darasa la Saba kwa sababu ya kile kinachosemekana kubainika kwa udanganyifu katika mtihani.

Jambo hili linasikitisha zaidi kwa kuwa wanaadhibiwa wasiohusika huku wahusika ambao ni walimu na wasimamizi wa mitihani wakiachwa bila kuchukuliwa hatua yoyote.

Rushwa hii ya mitihani ya Darasa la Saba ni rushwa maarufu sana nchi nzima ambapo shule hutenga fungu kwa ajili ya kuhonga wasimamizi wa mitihani na kisha kumwandaa mwalimu mmoja wapo ili aweze kufanya mtihani kwa niaba ya wanafunzi na kisha wanafunzi hupelekewa majibu.

Jambo hili huwa linafanywa na walimu wa shule husika kwa lengo la kujipatia sifa binafsi ya kuonekana wameweza kufaulisha watoto wengi zaidi bila kushirikisha wazazi na wanafunzi hupewa kama agizo au maelekezo.

Hali hii hupelekea hata wanafunzi wenye uwezo darasani kuingia katika mkumbo wa kukosa au kufutiwa matokeo kwa sababu tu walifuata maelekezo waliyopewa na walimu wao.

Tatizo hutokea pindi Waalimu walioandaliwa kutoa majibu wanapoamua kuwakosesha watoto aidha kwa makusudi au kwa lengo la kukomoana wao kwa wao kisha msalaba na hasara yote anaachiwa Mzazi masikini asijue wapi anampeleka mtoto wa miaka 12&13 baada ya matokeo yake kufutwa.

Inasikitisha zaidi kuona vyombo husika ikiwemo takukuru vimeshindwa kubaini rushwa hii maarufu katika mitihani ya shule za msingi kiasi tunahofu wale wanaoratibu wataendelea kufanya jambo hili baya na kisha kupoteza ndoto za watoto wetu.

Hivyo tunaomba ufanyike uchunguzi wa kina juu ya jambo hili ili wote waliohusika waweze kuwajibishwa badala ya kuwaadhibu watoto kwa kuwafutia mitihani wakati waliopanga na kuratibu jambo hili wakiachwa kuendelea na majukumu yao bila kuchukuliwa hatua zozote.

Tunamuomba Mheshimiwa Rais wa Tanzania aingilie kati jambo hili ili haki za watoto wetu kupata elimu zisipotee kwa kuadhibiwa wao kwa makosa ya walimu pamoja na wasimamizi wa mitihani kupokea rushwa.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Watunduru pole sana serikali ya ccm haina lengo la kuwaendeleza watoto wa kitanzania lengo lao ni kuwaumiza tu ili waendelee kutawala milele ,kuanzia awamu ya Kikwete hali hii ya walimu kuwafanyia watoto ilishamiri maeneo mengi nchini lakini ukiangalia ni kuwa wanasiasa wote diwani,mbunge na Rais wanatoa maagizo kwa walimu wakuu "lazima mufaulishe kwa mbinu zozote zile kama hufaulishi hicho chuo tunakupora hivyo mwalimu mkuu anafanya upuuzi wowote ili tu wanasiasa wafurahi na wananchi kwa ujinga wao wanakubali hili "lakini ukweli ni kuwa WANASIASA ndio wanaoangamiza Elimu ya Tanzania mbaya zaidi sababu za kufeli waziri anasema kwa kuwa mwalimu amekaa muda mrefu kituo kimoja ,kwa kweli ni hatari
 
Kama elimu yetu inaendeshwa katika Mazingira hayo hilo ni tatizo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sijui umemsikia Jafo leo...

kifupi CCM haina muda na Elimu ya masikini fukara.

pambaneni.
 
Back
Top Bottom