Rushwa CCM yafika kwa watoto;MTOTO WA NYOKA NI NYOKA ;KIKWETE UNA KAZI KWELI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rushwa CCM yafika kwa watoto;MTOTO WA NYOKA NI NYOKA ;KIKWETE UNA KAZI KWELI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Jan 5, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,580
  Likes Received: 5,762
  Trophy Points: 280
  Rushwa CCM yafika kwa watoto


  na Mwandishi Wetu


  [​IMG]
  TUHUMA za rushwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake, sasa zimefikia pabaya baada ya kubainika kuwa baadhi ya watoto wa vigogo waliowania nyadhifa mbalimbali katika uchaguzi wa vijana wadogo wa chama hicho (chipukizi), uliofanyika wiki iliyopita, wameshinda kwa nguvu ya rushwa.
  Uchaguzi wa chipukizi wa CCM, ambao ni sehemu ya umoja wa vijana wa chama hicho (UVCCM), ulifanyika katika Chuo cha Ualimu Kigurunyembe Morogoro, Desemba 29, mwaka jana.
  Tanzania Daima iliyokuwapo katika uchaguzi huo, ilishuhudia baadhi ya watoto wa vigogo wa chama hicho kupitia wapambe wao wakitoa rushwa kwa watoto wenzao waliokuwa wajumbe na wapiga kura, siku moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo.
  Wajumbe wa mkutano huo walikuwa ni wenyeviti wote wa chipukizi wilaya ambao ni watoto wa miaka 10 hadi 13, na makatibu wa chipukizi na uhamasishaji wa wilaya ambao huwa ni vijana wakubwa.
  Miongoni mwa wapiga debe walioshuhudiwa wakitoa rushwa kwa wajumbe ili wagombea wao washinde, ni wale waliokuwa wakiwapigia debe watoto wa vigogo hao.
  Wapiga debe hao walishuhudiwa wakigawa rushwa za kuanzia sh 20,000 hadi 35,000 kwa wapiga kura wa mkutano huo, usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi (Desemba 28), kwa kuzingatia msimamo wa wapiga kura.
  Wapiga kura waliokuwa tayari wana mgombea wao wanaowaunga mkono walikuwa wakihongwa dau la sh 35,000 ili wabadilishe msimamo, ilhali wale waliokuwa hawana mgombea maalum waliokuwa wanawaunga mkono, walikuwa wakihongwa sh 20,000 ili washawishike kuchagua watoto hao wa vigogo.
  Awali jina la mtoto wa kigogo mmoja halikuwekwa wazi kwa wanahabari na mwandaaji na msimamizi mkuu wa uchaguzi huo, Ester Bulaya, alipoyataja majina ya wagombea wote kwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi ndogo ya makao makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salam, Desemba 24 mwaka jana.
  Hata hivyo, katika hali iliyoonyesha dhahiri nguvu ya rushwa kufanikiwa, mtoto huyo wa kigogo aliyekuwa akishindana na wagombea wengine 10, alishinda nafasi hiyo kwa kishindo.
  Wagombea wawili kati ya hao waliokuwa wapinzani wa mmoja wa watoto wa vigogo hao walisema waliagizwa na wenyeviti na makatibu wa UVCCM wa mikoa wanayotokea kuwa watangaze kujitoa kwa sababu ambazo hawakuzielewa.
  “Nimejitoa kwa sababu yule mwenyekiti wangu wa mkoa (wa UVCCM) aliniambia nisigombee tena nitagombea wakati mwingine. Aliniambia ukifika wakati wa kujieleza nitangaze kujitoa,” alisema mgombea mmoja aliyejitoa aliyetokea katika mkoa mmoja wa ukanda wa Nyanda za Juu Kusini.
  Aidha, siku moja kabla ya uchaguzi huo Tanzania Daima alishuhudia baadhi ya makada na vigogo wa juu wa CCM na serikali yake, waliofika Morogoro wakikutana na baadhi ya wajumbe na wahamasishaji wa chipukizi hao.
  Miongoni mwa walioonekana katika eneo la uchaguzi ni pamoja na Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Emmanuel Nchimbi na Katibu wa Fedha na Uchumi, Amos Makalla.
  Wengine ni Nape Nauye, Januari Makamba, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita na wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machbya.
  Hali haikuwa shwari sana hasa pale wajumbe waliposikika wakisema ni lazima wagawe nafasi hizo kwa watoto wa maskini na si nafasi zote ziende kwa watoto wa vigogo hao, kwani maamuzi ya haki yatakuwa hayatendeki katika vikao.
  “Sisi sio wajinga, haiwezekani nafasi zote wapate watoto wa vigogo tu. Je, watoto wa mafukara waende wapi? Kwa namna hii si tutakuwa tunanyonywa kila siku?” walihoji wajumbe hao.
  Aidha, mkutano huo wa chipukizi uligeuka kuwa uwanja wa kampeni za ubunge wa vijana huku baadhi ya wagombea wanaotarajia kujitokeza kugombea ubunge kupitia UVCCM wakionekana kupigana vikumbo kugombea wajumbe ili kupata fursa ya kuzungumza na wapiga kura. Baadhi ya wagombea hao walikuwa wakijinadi kwa wajumbe kuwa wametumwa na vigogo wa chama na serikali kugombea nafasi hizo za ubunge hali iliyoonyesha kuwepo kwa mtandao fulani unaoandaliwa.
   
 2. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Miongoni mwa walioonekana katika eneo la uchaguzi ni pamoja na Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Emmanuel Nchimbi na Katibu wa Fedha na Uchumi, Amos Makalla.
  Wengine ni Nape Nauye, Januari Makamba, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita na wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machbya.


  Nape una kesi ya kujibu.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,580
  Likes Received: 5,762
  Trophy Points: 280
  Dk. Emmanuel Nchimbi

  MKUU MPAKA KIELEWEKE EMBU TUTAKE RADHI NA HILO JUU
  DK KAPATA KWENYE KAMBI YA JESHI AMA??WAMESHAONDOA HIKO CHEO FEKI MZUMBE BAAADA YA KUSHTUKIWA WALIINGIZWA MKENGE
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,580
  Likes Received: 5,762
  Trophy Points: 280
  anaitwa emanuel nchimbi
  ccm kazi ipo sasa shule wanadanganya sembuse vyeo loh si waanakutoa roho
   
 5. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2010
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Mimi nimequote kutoka habari ya Tz Daima sasa radhi ya nini?
  Kama Nape anajipambanua kuwa anapinga ufisadi anapaswa kutoka hadharani na kusema kilichojiri ,la sivyo naye atakuwa kwenye kundi la wanafiki daima.
   
Loading...