Rushwa Barabarani

Aug 5, 2019
62
87
Kumekuwa na tabia ya Askari wa Usalama Barabarani kusimamisha mabasi ya abiria maeneo ya Kibamba kwa Mangi pamoja na eneo la Magari Saba, Askari hao mara nyingi wamekuwa wakipokea pesa kuanzia shilingi 2000/= kutoka kwenye mabasi hayo.

Kuna nyakati ni kweli magari huwa na makosa na kuna nyakati mabasi hayo huwa hayana makosa ila husimamishwa na kuombwa rushwa hizo.

Jambo hili limekuwa kero hasa kwa wasafiri kupotezewa muda wao pindi wakiwa safarini
 
Hawa jamaa kila asubuhi wapo rodi hakuna daladala au tipa ya mchanga inayopita bila kuoa hela yaani ni laivi laivu kama ni halali kabisa. yaani hadi tushawazoea wakipiga mkono konda anashuka na buku mbili anampa laivu gari inaachiwa.
 
Yupo mwingine huwa anatega njia ya kutokea mabibo karibu na maeneo ya ubungo kwenye daraja linaloendelea kujengwa. Huyu ukimuona tu unajua kuwa ni mlevi anatafuta hela ya bia..
 
Back
Top Bottom