Rusahunga - Nyakanazi,Barabara Haipitiki toka jana na hakuna msaada wowote toka kwa wahusika!

alexelias

JF-Expert Member
Sep 1, 2017
2,032
3,198
Toka mapema jioni jana Barabara hiyo haipitiki maroli yamefunga njia!Hii ni kwa kifusi kilichomwaga na Mkandarasi Strabag bila kushindiliwa (COMPACTION)na Roller na kusababisha magari kukwama.

Ajabu ni,SI TANROADS,STRABAG AMA JAPO ASKARI TU WALIOPO HAPO KWA MINAJILI YA KUWASAIDIA WAHANGA!

Waziri wa Ujenzi pengine uje wewe kutatua tatizo hilo!
 
Barabara ya rusahunga/nyakanazi si inalami au infanyiwa ukalabati?.
 
Toka mapema jioni jana Barabara hiyo haipitiki maroli yamefunga njia!Hii ni kwa kifusi kilichomwaga na Mkandarasi Strabag bila kushindiliwa (COMPACTION)na Roller na kusababisha magari kukwama.

Ajabu ni,SI TANROADS,STRABAG AMA JAPO ASKARI TU WALIOPO HAPO KWA MINAJILI YA KUWASAIDIA WAHANGA!

Waziri wa Ujenzi pengine uje wewe kutatua tatizo hilo!

Hicho kipande kina lami, imekuwaje yatokee hayo, kama maroli pekee yamekwama je mabasi yaendayo Bukoba na Rwanda yanapita wapi
 
Kuna ukarabati mkubwa unafanyika na Mkarandasi Strabag.
 
Habari hii bila picha inaleta ukakasi kidogo kupata nguvu ya kusaidia kupaza sauti,maana unaweza ukatokwa povu kumbe ni fitina/chuki tu za mleta uzi...ngoja tukutazame tu hadi utakavyojiongeza na kukarabati vizuri habari yako..
 
Toka mapema jioni jana Barabara hiyo haipitiki maroli yamefunga njia!Hii ni kwa kifusi kilichomwaga na Mkandarasi Strabag bila kushindiliwa (COMPACTION)na Roller na kusababisha magari kukwama.

Ajabu ni,SI TANROADS,STRABAG AMA JAPO ASKARI TU WALIOPO HAPO KWA MINAJILI YA KUWASAIDIA WAHANGA!

Waziri wa Ujenzi pengine uje wewe kutatua tatizo hilo!

Wawataja polisi? Hao ni kwa minajili ya faini tu. Waje kwenye maslahi yasiyo yao? Thubutu!
 
Back
Top Bottom